Kanisa katoliki lina nguvu gani katika siasa za DR Congo?

DRC PRESIDENCY

Chanzo cha picha, IKULU YA RAIS DRC

    • Author, Rashid Abdalla
    • Nafasi, Mchambuzi

Februari 2023 inakadiriwa kuwa watu wapatao milioni walikusanyika katika eneo la wazi kwa ajili ya ibada katika uwanja wa ndege wa N'dole, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Ilikuwa ni zaidi ya miaka 37 tangu Papa kufanya ziara katika taifa hilo.

Asilimia kubwa ya raia wa Jamhuri ya Kimokrasia ya Congo ni watu wanaofuata dini.

Ukristo ukiongoza kwa kuwa na wafuasi wengi. Na zaidi ya asilimia 50 ya idadi jumla ya watu ni waumini wa dhehebu la Kikatoliti.

Inalifanya miongoni mwa madhehebu ya kiimani yenye nguvu katika taifa hilo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wiki hii Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi ameonya mtafaruku katika kanisa katoliki ambao unahatarisha umoja wa kitaifa kabla ya uchaguzi wa rais.

"Miongoni mwenu, kwa bahati mbaya kuna watu wachache ambao wamechukua mwelekeo hatari ambao unaweza kuligawa taifa letu. Siwezi kukubaliana na jambo kama hilo"

Katika taarifa yao wiki iliyopita, maaskofu wa kanisa katoliki DRC walisema, hali ya kisiasa ni ya wasiwasi na kuchukiza, ukandamizaji mbaya zaidi wa upinzani, vikwazo vya uhuru, ukandamizaji wa haki na watu kukamatwa kiholela" tangu Bw Tshisekedi achukue hatamu mwaka wa 2019.

Ukiwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huwezi kuepuka kusikia maoni ya kanisa katoliki kuhusu hali ya nchi.

Kanisa lina historia ya muda mrefu ya kutokaa kimya panapohusika shughuli za kisiasa za nchi hiyo.

Nguvu ya Kanisa

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mtafiti wa siasa na migogoro ya Afrika na mshauri wa zamani wa kisera juu ya sera na migogoro ya Afrika katika ofisi ya mambo ya nje na Jumuiya ya madola ya Uingereza, Ben Shepherd anasema katika mahojiano yake na Deutsche Welle:

"Chini ya mamlaka ya kikoloni Kalisa katoliki lililetwa kama mtoaji wa elimu, pia huduma za kiafya.

Wakati taifa la Congo linaporomoka, kanisa katoliki lilibaki kama taasisi ya kitaifa inayofikia watu na kutoa huduma kwa umma.

Wanapenda mipango, wana watu, na wana kamati zilizoundwa katika vijiji nchi nzima wakisaidia katika mambo kama kilimo.

Hivyo ni rahisi kueleza umuhimu wa kanisa katoliki DRC, na ndio maana wanaweza kusikaka katika siasa za nchi."

Kanisa katoliki halijawahi kuwa nyuma katika siasa za DR Congo, kiasi cha kuwa na waangalizi wake wakati wa chaguzi kuu za nchi hiyo.

Husambaza Mami ya waangalizi na hayimaye kutoa ripoti kuhusu chaguzi hizo.

Baada ya makumi ya watu kuuwawa katika maandamano ya kshinikiza Kabila asiendelee kukaa madarkani.

Desembaa 2016, Kanisa liliratibu makubaliano kati ya upinzani na serikali yaliomruhusu Kabila kusalia madarakani baada ya kumalizika kwa muhula wake hadi uchaguzi ukamilike.

Misukosuko na utata

Pia, zipo nyakati za mivutano kati ya kanisa na serikali. Ambazo hupelekea vifo au majeruhi. Bila ya kusahau nyakati za utata na kanisa kukosolewa.

Takribani watu wanane waliuwawa 2018 katika maandamano dhidi ya serikali ya Joseph Kabila.

Kanisa katoliki ndilo liliitisha maandamano hayo. Taarifa za vyombo vya habari vya ndani viliripoti maafisa usalama kuvamia makanisa, kurusha vito macho na kuwakamata wahubiri kadhaa.

Kanisa katoliki limesimama mara kadhaa kupinga rushwa na kupigia kampeni demokrasia na haki za binadamu.

Si sasa tu, hata wakati wa hayati Mobutu Sese Seko, ambaye Kwa wakati fulani alianzisha sera za kuingilia shughuli za kanisa Hilo.

Ni pale alipoanzisha sera za kutaka shughuli za kanisa - shule na vyuo, ziendeshwe kitaifa kuliko kidini. Sera ambayo ilileta mvutano kati ya serikali yake na kanisa hilo. Mvutano ambao haukuwepo hata wakati wa ukoloni.

Ni dhahiri ushawishi wa Kanisa katika siasa za Congo ni mkubwa.

Mara nyingi limejaza ombwe kwa Wacongo wengi katika taifa ambako mifumo rasmi imeshindwa kutimiza matarajio - kuanzia elimu, afya na chakula hadi kwenye maadili na msaada wa kiroho.

Ushawishi wake unatokana na kazi unazozifanya kwa raia wa Congo. Zinavutia wengi na kusaidia wengi, na kulifanya sauti ya kanisa kuwa kubwa miongoni mwa raia wa nchi hiyo.

Kuna nyakati zinazotazamwa kuwa za utata na za hatari. Baada ya uchaguzi wa Januari 2019, kwenye mkutano wa Kanisa na waandishi wa habari, liitangaza kuwa linamjua mshindi wa uchaguzi huo - lakini lilikataa kutaja ni nani hasa.

Kauli hii inaweza kuwa na lengo la kuhimiza matokeo ya uchaguzi yatangazwe.

Ila pia ni kauli ambayo wengine waliitafsiri inaingilia shughuli za Tume ya Uchaguzi nchini Kongo (CENI). Ni katika uchaguzi ambao baadaye ulimuweka madarkani rais wa sasa Félix Tshisekedi.

Rais Félix Tshisekedi anaielewa nguvu ya kanisa. Anaelewa kanisa linaweza kuwa chanzo cha utulivu wa kisiasa, vilevile likiamua kuhamasisha wafuasi wake linaweza kuiweka nchi patashika.