Faida za aiskrimu na mitindo ya utengenezaji wake

Four children in sitting position, each holding a waffle cone filled with a scoop of ice cream in their hand

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Watoto wanne wakiwa wamekaa, kila mmoja akiwa ameshika koni iliyojaa aiskrimu
Muda wa kusoma: Dakika 3

Watafiti wameangalia manufaa ya aiskrimu na madhara yake ya kiafya kwenye miili ya binadamu. Pia kuna masomo kuhusu jinsi aiskrimu inavyoweza kubadilisha hisia zetu.

Mwaka 2021 taasisi ya Psychiatry huko London iligundua, kuwa sehemu ya ubongo inayohusika katika mchakato wa utambuzi na kufanya maamuzi huamka baada tu ya ladha ya kwanza ya aiskrimu.

Tafiti zingine zinaonyesha virutubisho kama vile protini na mafuta, ambavyo vinapatikana kwa wingi katika aiskrimu, huinua viwango vyetu vya hisia na kuongeza viwango vyetu vya kemikali zinazobeba taarifa katika neva.

Machapisho mengi ya upishi, ikiwa ni pamoja na Oxford Companion juu ya Sukari na Pipi, yamebainisha kuwa aiskrimu haikujuulikana kwa Wazungu hadi Karne ya 16.

Mara tu majokofu yalipopatikana kwa bei nafuu katika nusu ya pili ya Karne ya 20 huko Magharibi, utengenezaji wa aiskrimu ulianza kubadilika na kuwa biashara ya kiviwanda.

Pia unaweza kusoma

Ni biashara kubwa

A small wooden spoon dipped into an earthen pot of Indian frozen dessert kulfi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Aiskrimu ya India huja katika ladha nyingi

Leo, aiskrimu ni biashara ya kimataifa inayozalisha dola za kimarekani bilioni 103.4 hadi 2024, kulingana na jukwaa la biashara la Statista.

Vionjo vinavyotumika vinazidi kuwa vingi, na vinatokana na vanila na chokoleti ya kawaida, na vingine vinafanywa kuakisi tamaduni za vyakula vya kienyeji.

Tapiwa Guzha, ambaye anaendesha mgahawa huko Cape Town nchini Afrika Kusini, alivutia mitandao ya kijamii mwaka 2022 kwa kutumia samaki waliokaushwa kwa chumvi na pilipili kutengeneza aiskrimu.

Yeye ni mzaliwa wa Zimbabwe, na mwanabiolojia wa molekuli, anasema anapenda chakula na hutumia akili ya kisayansi.

Aliiambia BBC: "Sikuwa na nia ya kutengeneza ladha za ajabu au tofauti, nilikuwa nikitengeneza tu ladha zinazoakisi mfumo wa vyakula vya ndani katika bara [la Afrika].

"Lengo la chakula changu ni kuonyesha aina tofauti na za kawaida katika makabila tofauti barani."

Aina mbalimbali

Tapiwa Guzha holding a red cup with ice cream in it

Chanzo cha picha, YouTube @tapiwaguzhamade

Maelezo ya picha, Tapiwa Guzha akiwa ameshikilia kikombe chekundu chenye aiskrimu ndani yake
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Na mtindo mwingine tofauti wa aiskrimu unapatikana huko Poland.

Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha West Pomeranian huko Szczecin walifanikiwa kutengeneza aiskrimu ya maziwa ya farasi ambayo ina mwonekano sawa na aiskrimu ya maziwa ya ng'ombe.

Utafiti waliochapisha mwezi Agosti pia unasema maziwa ya farasi jike yanaweza kusaidia kuboresha afya ya utumbo wa binadamu, lakini utafiti zaidi unahitajika.

Maziwa ya farasi yaliyochacha yamekuwa yakitumiwa Asia ya kati kwa muda mrefu, lakini kutengeneza aiskrimu iliyogandishwa kwa kutumia maziwa hayo ni jaribio jipya.

Kitty Travers amejaribu kuonja aiskrimu ya watafiti wa Kipolandi, lakini akakuta ladha yake hakuipenda na kwake haikuwa nzuri.

BBC ilipomtembelea mwishoni mwa Agosti, alikuwa ametengeneza aina nyingine ya aiskrimu kwa kutumia ngozi ya tunda la pea, chavua ya shamari na mbegu ili kutia ladha maziwa ya farasi jike.

Wiki moja baadaye, alitoa ladha mpya kwenye karamu na akapokea dole gumba kutoka kwa marafiki zake.

Kwa hivyo subiri ladha mpya na aina mpya za aiskrimu zinazokuja kwenye chumba kilicho karibu nawe!

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abdallah