Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 07.12.2022

Barcelona wanamfuatilia winga wa Arsenal na Brazil Gabriel Martinelli, 21, kwa nia ya kumnunua katika dirisha la uhamisho la Januari. (Sport - kwa Kihispania)

Liverpool, Chelsea na Arsenal wanavutiwa na kiungo wa kati wa Valencia na Marekani Yunus Musah, 20. (90min).

Borussia Dortmund itakuwa tayari kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 19, msimu ujao wa joto kwa euro 100m-150m (£86m-£129m).(Sky Sports)

Rais wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi anasema "kila mtu" anataka kusaini Bellingham "ya kushangaza" na klabu hiyo ya Ufaransa itapitia Dortmund kwanza ikiwa wanataka kumnunua. (Sky Sports)

Mshambulizi wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, bado hajafanya uamuzi kuhusu ofa ya kujiunga na klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia. (ESPN)

Tottenham wameibuka kuwa wanaopigiwa upato kumsajili kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie mwenye umri wa miaka 25 kutoka Barcelona. (Sport)

David Moyes atatimuliwa kama meneja wa West Ham huku kukiwa na uhusiano mbaya kati yake na mwenyekiti mwenza wa klabu David Sullivan. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa England James Maddison, 26, na kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 25, wamehusishwa na tetesi za kuhama Leicester City lakini Foxes watakataa kuruhusu mchezaji yeyote kuondoka Januari. (Leicestershire Live)

Real Madrid wanatazamiwa kuipiku Chelsea katika kumsajili mshambuliaji wa Palmeiras Endrick, 16, ambaye anaweza kuhama tu atakapofikisha miaka 18 mwaka wa 2024. (UOL Sport - kwa Kireno).

Kiungo wa kati wa Italia Marco Verratti, 30, atatia saini mkataba mpya na Paris St-Germain. (Fabrizio Romano)

Aston Villa watapewa ofa ya beki wa kati wa Leicester City na Denmark Jannik Vestergaard, 30, wakati wa dirisha la usajili la Januari. (Football Insider)