Nyoka na Chura:Kwa nini wanyama hawa wavamizi wameugharimu ulimwengu dola bilioni16?

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanasayansi walipohesabu uharibifu wa kiuchumi unaosababishwa na wanyama waharibifu kote ulimwenguni, waligundua kuwa viumbe wawili wanawajibika kwa madhara zaidi kuliko viumbe wengine wowote.
Chura wakubwa wa Marekani na nyoka wa mitini wa rangi ya kahawia kwa pamoja wamesababisha uharibifu duniani wa $16.3bn (£13.4bn) tangu 1986.
Mbali na madhara ya kiikolojia, viumbe hao wawili wavamizi wameharibu mazao ya shambani na kusababisha kukatika kwa umeme kwa gharama kubwa.
Watafiti wanaimani matokeo yao yatahimiza uwekezaji zaidi kusaidia kuzuia spishi vamizi katika siku zijazo.
Wakiandika katika Ripoti za Kisayansi, wanasayansi walimtaja nyoka huyo wa kahawia kuwa peke yake amehusika kufanya uharibifu wa jumla wa $10.3bn - kwa kiasi ameenea bila kudhibitiwa katika visiwa kadhaa vya Pasifiki.
Huko Guam, ambapo reptilia huyo alipelekwa kimakosa na wanamaji wa Marekani karne iliyopita, nyoka hao waemongezeka kwa idadi kubwa siku hizi na kusababisha kukatika kwa umeme sehemu kubwa kwa sababu wanateleza juu ya nyaya za umeme na kusababisha uharibifu wa gharama kubwa.
Zaidi ya nyoka hao milioni mbili wamejaa katika kisiwa hicho kidogo cha Pasifiki, huku kadirio moja likihesabu kuwa katika kila ekari moja ya msitu wa Guam kuna makazi 20 ya nyoka hao.
Mifumo ya ikolojia ya visiwa inadhaniwa kuwa hatarini zaidi kwa viumbe vamizi ambao husababisha tishio kubwa la kutoweka kwa wanyama asilia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Huko Ulaya idadi inayokua kwa kasi ya vyura wa Marekani wanahitaji mipango kabambe na ya gharama kubwa ya usimamizi.
Ili kuzuia kuenea kwa amfibia hao-ambayo inaweza kukua hadi 30cm (inchi 12) kwa urefu na nusu ya kilo (17.6oz) kwa uzito, maafisa wamelazimika kuweka uzio wa gharama kubwa kuzuia vyura kuzunguka maeneo yanayojulikana ya kuzaliana.
Kuweka uzio kwenye vidimbwi vitano tu ili kuwazuia wanyama hao kutoroka kuligharimu maafisa wa Ujerumani €270,000 (£226,300), utafiti wa zamani wa Umoja wa Ulaya uliotajwa na waandishi hao.
Inasemekana kwamba amfibia hula karibu kila kitu ikiwemo vyura wengine.
Aina nyingine ya chura wa kawaida wa coqui, alilaumiwa kwa kusababisha uharibifu wa kiuchumi kwa njia tofauti: Kelele za wimbo wao wa kupandiana zinaaminika kusababisha kushusha thamani ya mali katika maeneo ambayo wamevamia.
Waandishi wa utafiti wanaimani kuwa matokeo yao yatahimiza maafisa kuwekeza zaidi katika udhibiti wa wadudu na hatua zingine za usalama wa viumbe katika siku zijazo.















