Nyoka atumiwa kufunika uso kama barakoa
Msafiri huyo aliyekuwa amevaa barakoa yake ya nyoka alikuwa amejizungushia katika shingo na mdomoni, alionekana katika basi lililokuwa linatokea Swinton kuelekea mji wa Manchester nchini Uingereza siku ya Jumatatu.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Misri yaondolewa matumaini ya urais wa Shirika la biashara duniani

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Amina Mohamed wa Kenya na Ngozi Okonjo-Iweala wa Nigeria ni miongoni mwa wagombea Raia wa Misri Abdel-Hamed Mamdouh ameshindwa katika azma yake ya kugombea urais wa Shirika la biashara dunaini (WTO), na wagombea wa Mexico na Moldova wameondolewa katika kinyang’anyiro hicho.
Wagombea wengine wa Afrika ni Ngozi Okonjo-Iweala wa Nigeria na Amina Mohamed wa Kenya.
Watashindana katika awamu ya pili ya mchuano huo wenye wagombea wengine kutoka Korea Kusini, Uingereza na Saudi Arabia.
Rais mpya anatarajiwa kuchukua wadhifa huo mwezi wa Novemba.
Shirika The WTO hupanga sheria za biashara na kutatua mizozo ya kibiashara baina ya nchi. Na kama inavyoonesha katika blogi yake, kazi yake ni pamoja na "Kufungua milango kwa mipango mipya kwa kila mtu mmoja".
Virusi vya corona: Idadi ya waliopata maambukizi duniani yapita milioni 30

Chanzo cha picha, EPA
Takwimu kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani zinaonesha kuwa virusi hivyo viliwaua zaidi ya watu 940,000 kote duniani tangu mlipuko ulipoanza nchini China mwaka jana.
Marekani, India, na Brazil bado ndio nchi zilizoathiriwa vibaya zaidi na janga la Corona.
Takwimu pia zinaonesha kwamba kumekuwa na ongezeko la maambukizi katika wiki za hivi karibuni miongoni mwa mataifa ya Ulaya.
Nyoka atumiwa kufunika uso kama barakoa

Chanzo cha picha, PA Media
Maelezo ya picha, Mamla ya usafiri ya Greater Manchester imesema kuwa nyoka hakubaliki kufunika uso kama barakoa Msafiri huyo aliyekuwa amevaa barakoa yake ya nyoka alikuwa amejizungushia katika shingo na mdomoni, alionekana katika basi lililokuwa linatokea Swinton kuelekea mji wa Manchester nchini Uingereza siku ya Jumatatu.
Abiria mmoja, alisema anadhani abiria huyo alikuwa amevaa barakoa ya kisasa tu mpaka alipomuona nyoka huyo akiteleza katika chuma cha kushikia mikono.
Mkuu wa usafirishaji wa Manchester amethibitisha kuwa alikuwa ni nyoka na sio barakoa halisi.

Chanzo cha picha, PA Media
Shuhuda wa tukio hilo, ambaye alitaka kutofahamika alisema, ameona kuwa tukio hilo lilikuwa la kuchekesha na kustaajabisha,
Aliongeza kusema kuwa nyoka huyo hakuwasumbua abiria wenzake.
Msemaji wa usafiri wa Manchester alisema: "Muongozo uliotolewa na serikali umesema wazi kabisa kuwa barakoa zinazoruhusiwa sio lazima zile za upasuaji bali abiria anaweza kutengeneza barakoa yake anayoridhika nayo na kuivaa akiwa huru.
"Ingawa kuna kiwango kidogo tu tafsiri kamba inaweza kumaanisha hili, hatuamini maagizo hayo yalifikia kiwango cha mpaka kuruhusu ngozi ya nyoka-hususan wakati imeambatana na nyoka ."
Serikali ya Kenya yafunga hoteli iliyokwamisha kuhama kwa wanyama

Maelezo ya picha, Tukio la kuhama kwa wanyama kati ya mbuga za wanyama za Kenya na Tanzania ni maarufu sana Nchini Kenya maafisa wameifunga hoteli ya kifahari iliyojengwa katika mbuga ya wanyama , ambayo ilionekana kufunga mapito ya wanyama wanaohama katika hifadhi ya wanyama maarufu ya Maasai Mara Game wiki iliyopita.
Tukio la kuhama kwa wanyama wa mbugani kati ya mbuga za wanyama za Maasai mara nchini Kenya na Serengeti nchini Tanzania ambalo hutokea kila mwaka katika eneo hilo ni maarufu sana na watalii wengi huenda kulishuhudia kila mwaka.
Wiki iliyopita video ilionesha wanyama wakiwa wamekwama katika mto, huku hoteli hiyo ikiwa imefunga njia yao, na wafanyakazi wa hoteli wakiwafukuza wanyama, iliibua hasira miongoni mwa Wakenya hususan mitandaoni wakiitaka serikali kuchukua hatua na sasa waziri wa utalii ameagiza ifungwe.
Wanyama hao huhama kila mwaka kwa ajili ya kutafuta malisho na kuzaliana.
Wasanii Susho na Kenzo waelezea changamoto za mahusiano na ndoa zao

Ni watu tunaowaona na kujivunia. Ni waimbaji, waigizaji ama hata wanahabari maarufu. Lakini licha ya umaarufu huo, wengi wao wanakabiliwa na changamoto kubwa; kudumisha mahusiano yao, ama kuwa na ndoa za kudumu.
Utafiti uliofanywa na jarida la Huffpost unaonesha kuwa takribani asilimia 52 ya ndoa za waigizaji maarufu wa Hollywood huishia kwa talaka na kwa wanawake hali ni mbaya hata zaidi, kwani karibu asilimia 62 ya waigizaji wanawake wa Hollywood wamepewa talaka.
Sababu kadha wa kadha zimetolewa kujaribu kueleza ni kwa nini ndoa za watu maarufu ama mahusiano ya wapenzi miongoni mwa watu mashuhuri huishia kwa majonzi.
Hii imewaacha wengi na majonzi. Huku jamii inayotazama ikijiuliza maswali mengi, pasi na kuwa na majibu. Ni kwa nini watu ambao walionekana kupendana sana na kuwa na matumaini ya siku za usoni wakosane na kuachana? Ni kwa nini mara nyingi mahusiano ya watu mashuhuri yanasambaratika? Je, ni kweli kwamba haiwezekani kuwa na umaarufu na bado ufaulu kuwa na ndoa yenye furaha? Hayo ndio maswali yetu ya leo...

Ili kupata jibu la maswali hayo, ungana nae Roncliffe Odit na Hamida Aboubakar katika ukurasa wa Facebook wa BBC Swahili inapotimu saa tano na nusu asubuhi. Watakuwa pamoja na Christina Shusho ambaye ni muimbaji wa nyimbo za injili kutoka Tanzania, pamoja na familia ya Navy Kenzo, ambao ni Nahreel na mke wake Aika, wote ni wanamziki kutoka Tanzania.
Maseneta wamaliza mzozo juu ya mgawanyo wa mapato Kenya
Maseneta nchini Kenya wamefikia mkataba ambao umetatua mzozo wa muda mrefu juu ya mpango wa kugawanya fedha zilizotengewa kaunti 47 za nchi hiyo.
Mkataba huo umefikiwa siku moja baada ya magavana wa kaunti kukubaliana kusitisha huduma zote isipokuwa za lazima baada ya kukwama kufikia maafikiano kuhusu mgawanyo huo jambo lililochelewesha kutolewa kwa fedha za mishahara ya kuwalipa wafanyakazi katika kaunti zote nchini humo.
Rais Uhuru Kenyatta alilazimika kuingilia kati jumanne na kuahidi kwamba waziri wa fedha ataongeza kiwango cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya kaunti kutoka kiwango cha sasa cha dola bilioni 2.9 hadi takriban dola bilioni 3.4 katika mwaka ujao wa fedha.
Mpango huo iliidhinishwa na seneti Alhamisi mchana, na hivyo kumaliza miezi kadhaa ya mkwamo wa shughuli za kaunti, seneti na serikali ya kitaifa ambayo ilikataa kutoa fedha kwa kaunti hadi mpango utakapoidhinishwa.
Makampuni ya Somalia 'yalitumiwa kuwalipa wauzaji wa silaha’

Chanzo cha picha, Getty Images
Ripoti kuhusu mifumo maarufu ya usafirishaji wa fedha imebaini kuwa dola milioni 3.5 taslimu zimekuwa zikisafirishwa kati ya watu wanaoshukiwa kuwa wauzaji wa silaha katika miaka ya hivi karibuni.
Ripoti hiyo ya shirika la kimataifa la mapambano dhidi ya usafirishaji wa pesa za ugaidi - The Global Initiative Against Transnational Organized Crime, inadai kwamba msambazaji maarufu wa silaha wa Yemen aliweza kupokea maelfu ya dola kwa njia ya malipo au zawadi , licha ya kuwekewa vikwazo na Marekani.
Ufichuzi wa ripoti hiyo unaweza kuzuia zaidi majaribio ya makampuni ya usafirishaji wa fedha ya Kisomali kufanya kazi na benki za kimataifa ambazo zina hofu ya kuvunja sheria za usafirishaji wa fedha.
Yakijibu ripoti hiyo, makampuni ya Kisomali yameliambia shirika la habari la Reuters kwamba walifanya kila wawezavyo kutekeleza sheria za kimataifa za udhibiti.
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara ya leo Ijumaa tarehe 18.09.2020
