Genge la Rochdale grooming: 'Nilibakwa zaidi ya mara 100 kuanzia nikiwa na umri wa miaka 12'

f
Maelezo ya picha, Ruby alizungumza na BBC Newsnight kuhusu jinsi alivyoandaliwa na kunyanyaswa na genge kwa miaka minne kuanzia alipokuw ana umri wa miaka 12.

Na Victoria Derbyshire, Sean Clare & Hollie Cole

BBC News

Muathiriwa wa genge la Rochdale grooming amesema alibakwa zaidi ya mara 100 kutoka akiwa na umri wa miaka 12 na alihisi "kuangushwa" na polisi.

Ruby pia alikiambia kipindi cha BBC Newsnight kuwa polisi walilichua kijusi chake baada ya kutoa mimba kwa ajili ya kukifanyia uchunguzi wa DNA bila kumwambia.

Aliyekuwa mpelelezi Maggie Oliver alisema kuwa miaka kadhaa baada ya unyanyasaji wa Ruby, unyanyasaji wa kingono kwa watoto bado ulikuwa ukifanyika kote nchini.

BBC imewasiliana na Polisi wa Greater Manchester (GMP) kutuhuma hizi.

Msemaji kutoka Halmashauri ya Borough ya Rochdale anasema "inasikitika sana" kwamba halmashauri hiyo "ilishindwa kuchukua hatua zinazohitajika kuwalinda watoto dhidi ya unyanyasaji" wakati Ruby aliponyanyaswa kingono.

Ruby alisema alitaka kuwasaidia watoto wengine walionyanyaswa ambao wanahitaji kusikilizwa "wahisi kuwa wanasikilizwa" wanaporipoti uhalifu huo kwa polisi. Ametaka ushauri utolewe baada ya mahojiano na polisi.

Mnamo mwezi Januari, uchunguzi ulibaini wasichana "waliishi kwa rehema " ya magenge ya ubakaji wa watoto kwa miaka mingi kwa sababu ya kushindwa kazi kwa wakuu wa polisi na wakuu wa baraza.

Uchunguzi huo visa 111 katika mji huo kuanzia mwaka 2004 hadi 2013 kubainisha wazi kushindwa kazi kwa GMP, na kuelezea kuwa kuwatambua wanaume 96 walioshukiwa kwa ubakaji huo kungeweza kuleta hatari kwa watoto.

Tahadhari: Baadhi ya wasomaji wanaweza kuhisi ripoti ifuatayo kuwa ya kuhuzunisha

Ruby, ambaye jina lake halisi haliwezi kutajwa kwa sababu za kisheria, alisema unyanyasaji huo ulianza baada ya baadhi ya wanaume wenye umri mkubwa kumualika yeye na marafiki zake kwenye tafrija katika makazi ya gorofa kwa ajili ya chakula na vinywaji. Yote hayo yalifanyika kwa kipindi cha wiki kadhaa.

Lakini kwa siku siku moja "hawakuturuhusu kuingia chumbani" kwa sababu watu wengine walikuwa chumbani, alisema.

"Walitupa lita moja ya vodka kavu bila kuchanganywa na kitu chochote na sigara 10. Kwa hivyo wakati tunaingia kwenye chumba kingine, sote tulikuwa tumelewa."

‘Kufa ganzi’

Ruby alisema kulikuwa na "wanaume 30 hadi 40 waliokuwa wakitusubiri" na kisha "walinibaka... mfululizo".

"Mmoja angemaliza [kunibaka] na kisha mwingine akaingia na ilikuwa hivyo usiku kucha."

Alisema unyanyasaji huo uliendelea kwa sababu genge hilo lilimtishia na alihisi "hakuna njia ya kutoka".

"Walipata namba zetu, wakawa wanatujia shuleni, walifika karibu na nyumbani kwetu , walitutafuta kila mahali na kuhakikisha wanatupata."

Alisema alibakwa "pengine zaidi ya [mara] mia" na wanaume "kutoka kote nchini" kwa miaka minne.

"Kulikuwa na wanaume kutoka Bradford na Nelson na Birmingham, Blackpool… [genge] lilitupeleka kila mahali," alisema.

"Nilihisi kama mtu aliyekufa ganzi.", nilipokuwa ninabakwa

f
Maelezo ya picha, Unyanyasaji wa kingono kwa watoto bado unaendelea Rochdale na kote nchini Uingereza, Maggie Oliver anasema.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mnamo mwaka wa 2008, Ruby alienda kwenye kliniki ya afya ya ngono, ambayo anasema ilikuwa na mahala ambapo aliona anaweza kufikisha "kilio cha kuomba msaada kwa sababu hakukuwa na mtu mwingine wa kutusaidia".

"Tuliiambia shule, na huduma za kijamii zilijua kinachoendelea. Tena, hakuna kilichotokea, kwa hiyo tulikwenda huko, lakini tulipewa kondomu zenye ladha na kuambiwa tuondoke."

Uchunguzi ulithibitisha kwamba Ruby hapo awali alikuwa amefichua kwa Timu ya utatuzi wa migogoro kwamba alikuwa na marafiki wa kiume wakubwa wanaompa vodka na kumnyanyasa kingono.

Katika mwaka huo huo, aliwekwa kwenye mpango wa ulinzi wa watoto, na polisi walifahamu hali yake mwanzoni mwa mwaka 2009.

Ruby alitoa mimba alipokuwa na umri wa miaka 13 na polisi ilichukua umiliki wa kijusi ili kukichunguza kisayansi kwa uwezekano wa kulinganisha DNA na washukiwa katika uchunguzi.

Ukaguzi ulisema "haikubaliki" kwamba Ruby hakuambiwa polisi wamekichukua.

Alisema baadaye alifuatwa na jeshi kuulizwa iwapo angetaka mazishi ya kijusi kilichotolewa.

Mnamo 2010, Ruby alimwambia mfanyakazi wa huduma kwa kijamii kuhusu unyanyasaji wake unaoendelea na wanaume sita wakubwa wa jamii ya Asia, uchunguzi ulisema.

Pia alifizifichulia huduma za kijamii kuhusu unyanyasaji mkubwa wa watoto unaofanywa na hadi wanaume 60.

Miaka miwili baadaye, mmoja wa wanaume waliomdhulumu alihukumiwa kifungo cha miaka minane jela kwa kosa la ulanguzi kwa unyanyasaji wa kingono.

Lakini miaka minne tu kutoka hapo, Ruby alimwona kwenye duka la ndani ya eneo lake. Alisema hakuwa ameambiwa kuhusu kuachiliwa kwake kutoka jela.

"Mwanzoni nilimuangalia mara mbili kwa sababu sikuamini nilichokuwa nimekiona. Kisha, nilipohakikisha kuwa yuko pale, nilikimbia," alisema.

"Kisha nilienda tu nyumbani na sikuondoka nyumbani kwa kama miezi mitatu baada ya hapo."

Ruby alisema aliipigia simu polisi na "hawakufanya chochote", na kuongeza: "Nilishindwa la kufanya."

Tathmini ya uchunguzi wa polisi kuhusu unyanyasaji wa kingono kwa watoto kwa umri wa miaka tisa, iligundua kuwa jeshi hilo lilizingatia uhalifu huo kama kipaumbele cha hatari ya kiwango kidogo.

Maggie Oliver alijiuzulu kazi ya polisi mwaka wa 2012 kwa sababu ya ushughulikiaji mbaya wa kesi za unyanyasaji na kuanzisha shirika la kusaidia waathiriwa.

Alisema unyanyasaji wa kingono kwa watoto bado unaendelea Rochdale na taasisi yake ilisikika kutoka kwa wahasiriwa "nchi nzima".

"Waathiriwa leo wananiambia mambo yale yale ambayo Ruby na watoto hao waliniambia miaka 12 iliyopita," Bi Oliver alisema.

"Nadhani umma unajua kinachoendelea, lakini bado nadhani polisi na huduma za kijamii wanajifanya kuwa wamejifunza."

g
Maelezo ya picha, Aliyekuwa mpelelezi Maggie Oliver alijiuzulu kutoka polisi -GMP ili kufichua makosa ya kikosi hicho

Ruby ametoa wito wa msaada zaidi kwa watoto waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia na kusema wanapaswa kupewa msaada wa kisaikolojia baada ya mahojiano ya polisi.

“Nataka kila mtoto anayepitia milango ya kituo cha polisi na kuripoti unyanyasaji wa kijinsia ajisikie anasikilizwa,” alisema.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi