Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nyayo za binadamu mwezini zinaweza kuishi kwa miaka zaidi ya milioni
Nasa inapojiandaa kupeleka kizazi kipya cha wanaanga kwenye Ncha ya Kusini ya Mwezi, huenda ikapata seti nyingine ya nyayo zinazoashiria alama yake isiyofutika katika ziara yake mwezini.
Bila shaka kama mojawapo ya nyayo za kwanza ambazo mwanadamu amewahi kuacha kwenye ulimwengu mwingine, ni ishara yenye nguvu ya jitihada za binadamu.
Nyayo hiyo ni moja tu ya mamia iliyoachwa na wanaanga 12 waliotembelea Mwezini kati ya mwaka 1969 na 1972.
Na, kama tujuavyo, nyayo hizo bado zipo hadi leo. Bila upepo au mvua kuziondoa, zitabaki katika anga hizo za mbali kwa mamilioni ya miaka.
Lakini nyayo za kwanza kwenye uso wa mwezi katika miaka 50 zitaonekanaje?
Na je, viatu vinavyotengeneza sasa vitatofautiana vipi na vile vilivyovaliwa na wanaanga wa awali wa Apollo?
Ili kujibu maswali haya wataalamu wa wa anga za juu wanasema viatu vitakavyovaliwa na wanaanga kwenye misheni ya Artemis vitahitajika kuwalinda wavaaji dhidi ya mazingira magumu na halijoto kali, lakini jukumu lao la kukumbukwa zaidi litakuwa nya watazoziacha nyuma.
Kwa kuzingatia ushauri huo Nasa na washirika wake wa kibiashara wametumia miaka mingi kubuni na kuweka sawa nyenzo za kizazi kijacho cha viatu vya mwezini.
Wanaanga hao wapya wanne watakapotua Mwezini mwaka wa 2025 wakiwa na Mpango wa Artemis, viatu vyao vitahitajika kufanya kazi kwa njia ambayo viatu vya Apollo havijawahi kufanya ili kuwafanya wavaaji kufurahia katika misheni yao.
Vitu hivyo vitatahitaji kuwalinda wanaanga kwa muda mrefu katika halijoto ya chini kama -225 (-373°F), pamoja na kuwaweka sawa kwenye eneo la Ncha ya Kusini ya mwezi lenye volkeno nyingi.
Kando na kujumuisha nyenzo na teknolojia za kibunifu kwenye viatu hivyo, wahandisi pia wanaelekeza mawazo yao kwenye chapa ambazo zitaashiria uso wa Mwezi kwa milenia ijayo. Nyayo za viatu hivi hazitahitaji tu kuonekana vizuri juu ya uso wa Mwezi, lakini zitakuwa tofauti na zinazotambulika moja kwa moja kama zile zilizoachwa na watembea wa kwanza mwezini.
"Hakika kuna baadhi ya sifa za utendaji ambazo zinapaswa kujumuisha kwenye viatu hivi," anasema Zach Fester, mhandisi wa suti ya anga za juu katika Kituo cha Anga cha Nasa Johnson ambacho kimekuwa kikiongoza utafiti wa kiatu kipya kitakachovaliwa na wanaanga kwenda mwezini.
"Uwezo wa kushikilia chini vizuri ni muhimu sana- unaangazia soli ya buti kwa vipengele mbalimbali vya msingi, kwa hivyo inahitaji kuwa na uwezo kujishikilia chini vizuri mvaaji akitembea na viatu hivyo juu ya mwamba mgumu au vitu vingine kama vile magari, ngazi na rova, kuwa imara dhidi ya uchakavu. Lakini uzuri ni sehemu yake pia, kwa sababu picha hizo [za nyayo] ni za kuvutia sana."
Kandarasi ya muundo wa suti za wanaanga zitakazotumika katika misheni ya Artemis imepewa Axiom Space, kampuni ya anga za juu ambayo mapema mwaka huu ilifanya kazi yake ya pili ya kibinafsi ya wanaanga katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.
Sehemu muhimu ya suti mpya za anga, ambazo zilifichuliwa Machi 2023, zitakuwa moonboot yenyewe. Lakini, muundo halisi wa viatu hivyo bado haujawekwa wazi.
Lakini utafiti uliochapishwa na Nasa kuhusu mahitaji yanayopaswa kufikiwa na viatu hivyo ni pamoja na kufanyia majaribio ya awali baadhi ya miundo ya viatu vilivyotolewa mapema.
Labda changamoto kubwa itakuwa halijoto ambayo wanaanga watakabiliana nayo ikilinganishwa na misheni ya Apollo, ambayo ilifanywa hasa katika maeneo tambarare ya kutua katika maeneo ya ikweta ya Mwezi.
Wakati chombo cha Artemi III kinapotua kwenye Mwezi, wafanyakazi wake watakuwa katika mazingira tofauti sana katika Ncha ya Kusini ya mwezi.
"Katika Ncha ya Kusini, tunatazamia hali ya joto zaidi," anasema Fester.
Eneo hilo linajulikana kuwa na maeneo ambayo hayajawahi kufikiwa na mwanga wa jua.
"Hayajashuhudia mwanga wa jua kwa maelfu ya miaka," Fester anasema.
Hii inamaanisha ni eneo lenye baridi ya ajabu. Kwa hivyo kuwa na mavazi ya kuhimili baridi kali itakuwa muhimu.
Nasa na Axiom zimekuwa zikijaribu aina mpya za povu za kuhami joto na mafuta maalum ya kusaidia kuweka halijoto ndani ya viatu hivyo.
Wataalamu Fester na Ralston wanasema kuwa bado haijaamuliwa ikiwa viatu vya kutembea mwezini katika misheni ya Artemis vitatumia mbinu sawa kwa kutumia overboot, lakini wanasema itaendeshwa na mahitaji ya hali ya mazingira.
Viatu vya kwanza vilizojaribiwa na Nasa zinaonekana kuashiria hii inaweza kuwa chaguo linalopendelewa.
Na nyayo zenyewe zinaonekana tofauti kabisa na zile zilizotumiwa wakati wa Apollo.
Nguo moja ya silikoni ilikuwa na maumbo ya chevron, huku nyingine ikiwa na nyayo tata kama ya kiatu cha kupanda mlima ili kushika vizuri zaidi sehemu ya volkeno ya Ncha ya Kusini.
Ingawa Ralston hajafichua maelezo ya jinsi mwendo wa mwisho unavyoweza kuonekana, alitoa kidokezo kimoja: "Tuna mipango ya muundo maalum wa nyayo ambayo inaweza kujumuisha nembo au picha zingine zinazoashiria umuhimu wa kurudi mwezini."
Jambo moja ambalo liko wazi - nyayo zijazo Mwezini zitakuwa muhimu kama za mwisho, kuashiria enzi mpya katika uchunguzi wa anga za mbali.