Hadithi kuhusu upara: Je wanasayansi wanasemaje?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Watu wengi duniani wanasumbuliwa na upara duniani, na tatizo hili limekuwa likifanyiwa utafiti na wanasayansi ili kulitatua kwa karne nyingi.

Takriban miaka 200 iliyopita, Mwanasayansi Mgiriki, Hippocrates ,anayefahamika kama baba wa tiba ya kisasa, kwanza alitenganisha utafiti wake wa kisayansi na imani za kidini.

Je ni vipi nywele zake zitamea nyakati zile? Kutoka wakati huo tafiti nyingi zimekuwa zikifanyika . wanasayansi wakitafuta ni vipi nywele zinaweza tena kumea kwenye kichwa cha mtu aliyepoteza nywele.

Kutokana na matokeo ya tafiti hizi tunaweza vyema kuelewa siri nyuma ya nywele zetu leo.

Tuna uwezo pia wa kuelewa kwa urahisi zaidi sababu zinazosababisha upara, kuanzia athari za urithi hadi atahari za mazingira.

Hatahivyo kuna dhana potofu miongoni mwa watu kwamba hizi ndio sababu za kupoteza nywele.

"Kuwa na upara sio kitu kibaya," anasema Carolyn Goh, daktari wa Ngozi katika Chuo kikuu cha California, Los Angeles (UCLA) ambaye amebobea katika elimu ya kupotea kwa nywele na matatizo ya nywele.

Dkt. Goh anasema bado kuna dhana potofu kuhusu upara.

Kulingana na maelezo aliyoyapata, ngoja sasa tuelewe dhana potofu tatu kuhusu upara.

Getty

Chanzo cha picha, MIKROMAN6

1: Upara ni wa kurithi

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Unawasikia marafiki na watu wa familia wakisema, mara nyingi upara mtu huupata kutoka kwa mtu katika familia yake. Lkaini ukweli halisi ni zaidi ya hilo .

Katika jarida la PLOS Genetics lililochapishwa mwaka 2017 nchini Uingereza, kikundi cha watafiti Waingereza kilisema kwamba kilifanyia utafiti kuhusu upara wa kurithi wanaume 52,000.

Utafiti huo pia ulibaini kuwa walau wanaume 78 walikuwa na matatizo ya urithi ya kupoteza nywele. Kundi hili la watafiti lilisema kuwa asilimia 40 ya vipara husababishwa na kasoro katika Kromosomu X –(Kromosomu inayohusika na jinsia)

Inamaanisha kuwa huku jeni moja inaridhiwa kutoka kwa mama, nyingine zinaweza kuwa katika jeni zote.

Huku ni ukweli kwamba jeni hizo imara huridhishwa kutoka kwa mama na familia yake, Goh anasema kwamba jeni moja tu haisababishi upara.

Inasemekana kwamba upara husababishwa na jeni zaidi ya moja. Jeni ambazo husababisha upara hutoka pande zote mbili , upande wa baba na upande wa mama.

Lakini upara haumo kwa wanaume na wanawake. Tunahitaji kujua ni kwanini upoteaji nywele sio sawa kwa wanaume na wanawake.

Tunahitaji kujua ni nini hasa wanachosema wanasayansi kuhusu upoteaji wa nywele unaofahamika kwa lugha ya kisayansi kama 'Androgenetic Alopecia' ambao ni wa urithi which is hereditary alopecia.

Kulingana na Goh, Jeni ambazo husababisha aina hii ya upoteaji wa nywele hufahamika kwa kuwa inaathiriwa na homoni za kiume - testosterone.

Hutokea kwa wanaume na pia kwa wanawake. Lakini kuna mabadiliko ndani yake.

Upara sio wa kawaida miongoni mwa wanawake. Lakini pia wanawake hupoteza nywele kwenye kichwa chao.

Wanawake hawana homoni nyingi za testosteroni kama wanaume.

Ili kuwa na uwiano wa hili uwiano wa hili , Goh alisema kuna kiwango cha juu cha homoni za estrogen.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

2: Upara husababishwa na uvaaji wa kofia

Je unaoga mara ngapi kwa wiki? Kila siku, a mara tatu kwa wiki? Je unavaa kofia kila mara ?

Haya ni maswali mhudumu wako wa saluni atakuuliza . Hii ndio maana nywele zako zinang’oka.

Lakini hakuna moja ya mambo haya inaweza kusababisha kupotea kwa nywele zako. Goh anasema hakuna ushahidi kwamba kofia husababisha mtu kupoteza nywele zake.

Kichwa ni shehemu yenye mafuta zaidi ya mwili wetu. Hatahivyo, hii sio sehemu inayoweza kuathiriwa zaidi.

Ukilinganishwa na sehemu nyingine za mwili, baadhi ya aina za mizio hutokea katika vichwa vyetu, anasema mtaalamu.

Getty

Chanzo cha picha, UCLA

3: Hakuna tiba ya upara

Kwa sasa kuna suluhu tatu za tiba mbadala zilizothibitishwa za kuzuia upara. Lakini hakuna hata moja inayoweza kukupa hakikisho la kupona asilimia 100.

Upoteaji wa nywele unatokana na sababu ngumu za kikemikali na kibaiolojia. Hatahivyo, juhudi za kuzuia au kutibu tatizo hili zinaweza kupunguza upoteaji wa nywele. Husaidia kukuza tena nywele zilizopotea.

Minoxidil  huuzwa kama mafuta ya majimaji na unaweza kuipaka moja kwa moja kichwani.

 Tafiti chache ndogo zimeripoti ukuaji wa nywele mpya baada ya kutumia dozi ndogo ya maji au vidonge vya minoxidil .

Finasteride.. Ni dawa ambayo inaweza kumezwa. Ilikuwa ikitumiwa asilia kama dawa ya kupanua tezi dume, na sasa inatumiwa kuzuia upoteaji wa nywele . 

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Upandikizaji.. Wakati wa upandikizaji…nywele huchukuliwa kutoka mahali ambapo nywele inakua na kuwekwa mahali ambapo hakuna nywele.

 Aina nyingi za upasuaji wa upandikizaji zimekuwa zikifanyika katika miaka ya hivi karibuni.

Lakini Dk. Goh anasema kwamba kulikuwa na dhana nyingi potofu kuhusu upandikizaji wa nywele miaka iliyopita. Lakini alifichua kuwa upandikizaji unatoa matokeo mazuri katika nyakati za hivi karibuni.