Nazi Soldau: Majivu ya waathiriwa 8,000 yapatikana katika kaburi la halaiki nchini Poland

Msalaba wa mfano umesimamishwa kwenye eneo la kaburi la halaiki

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kielelezo cha msalaba kimesimamishwa katika eneo la kaburi la halaiki

Kaburi la halaiki lenye tani 17.5 ya majivu ya watu imepatikana kaskazini mwa Poland, karibu na iliyokuwa kambi ya Soldau ya Wanazi kutesa watu.

Kambi hiyo ilijengwa mwaka 1939 kwa ajili ya kusafirisha, kuzuilia na kuangamiza watu katika kipindo chote cha uvamizi wa Wanazi.

Hadi watu 30,000 wanasadikiwa kuuawa katika kambi hiyo na watafiti wanamatumaini ya kufanyia mabaki hayo uchunguzi wa chembe chembe za vinasaba DNA, kupata maelezo zaidi kuhusu waathiriwa. Miongoni mwa Wapoland waliouawa ni makasisi na maafisa wa ujasusi.

Wanaakiolojia wamepata mamia ya mabaki ya nguo na vifungo lakini hakuna kitu cha thamani kilicopatikana kuashiria kuwa watu hao waliporwa kabla ya kuua wa na miili yao kuteketezwa.

Bw.Jankowski alisema shimo mbili zilipatikana karibu na Soldau, ambayo sasa inafahamika kama Dzialdowo, na shughuli ya ufukuaji utaendelea ili kutafuta mabaki zaidi.

Makadirio ya waathiriwa 8,000 iyanayotokana na uzito wa mtu unakisiwa kufikia kilo mbili.

Kwengineko Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki siku ya Jumatano alisema kuwa ripoti ya kina inayoangazia uhalifu wa kivita wa Wanazi na hasari iliyotokana na uvamizi huo kwa thamani ya sasa imeandaliwa.

 Alisema Ujerumani imesababisha madhara makubwa kwa watu wa Poland na haijawahi kulipa fidia. Ujerumani imesema suala la fidia lilifungwa kisheria katika miaka ya 1950.