Mgogoro wa Sudan: Ruto hadi Sisi, viongozi wanahangaika kuleta amani

Chanzo cha picha, Getty Images
Ishara ya umakini wao wa kumaliza mzozo unaoendelea nchini Sudan, mataifa manne ya Afrika Mashariki, yakiongozwa na Kenya, yanashinikiza kutumwa kwa kikosi cha kikanda ili kulinda raia na kuhakikisha misaada ya kibinadamu inawafikia mamilioni ya watu waliokwama katika eneo la vita. .
Lakini kupata makubaliano ya pande zinazozozana itakuwa kazi mgumu, kwani hawajaonyesha nia yoyote zaidi ya ushindi wa kijeshi tangu mzozo huo ulipozuka katikati ya mwezi Aprili.
Jeshi, linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, linadhibiti sehemu kubwa ya mashariki na kati mwa Sudan, na linashikilia kambi za kijeshi katika mji mkuu, Khartoum.
Kikosi cha upinzani cha Rapid Support Forces (RSF), kinachoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagolo, anayejulikana kama "Hemedti", kimepiga hatua kuelekea Khartoum, wapiganaji wake wanatuhumiwa kwa mauaji, ubakaji na kukalia na kupora hospitali.
Wanajeshi hushambulia kwa mabomu maeneo ya RSF bila kuchoka katika mji mkuu, na kusababisha vifo vingi vya raia. Vilevile kwa mujibu wa vyombo vya Habari, vurugu za kutisha zinaendelea katika eneo la magharibi mwa Sudan la Darfur.
RSF imetawala sehemu kubwa ya Darfur. Pamoja na washirika wao wanamgambo wa Kiarabu, wapiganaji wa RSF wamewafukuza maelfu ya watu wa kabila la Masalit kutoka eneo la kihistoria magharibi mwa Darfur.
Walichoma jumba la sultani, kiongozi wa kimila wa kabila hilo. Gavana, Khamis Abubakar, alipoyaita ni "mauaji ya kimbari," wanaume waliovalia sare za RSF walimteka nyara na kumuua. Zaidi ya wakimbizi 160,000 wa Masalit wamekimbia na kuvuka mpaka kuelekea Chad.
RSF pia ilivamia jiji la Zalingei, nyumbani kwa jamii ya Fur, na kuzunguka miji miwili mikubwa katika eneo hilo, al-Fashir na Nyala.
Watu wengi wa Darfuri wanahofia huu ni mpango wa muda mrefu wa kubadilisha eneo lenye mchanganyiko wa kikabila kuwa eneo linalotawaliwa na Waarabu.
Jambo la dharura magharibi mwa Darfur ni ulinzi wa raia. Misheni ya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur ilikuwa na mamlaka ya kulinda amani. Lakini iliondolewa miaka miwili iliyopita katika uamuzi ambao sasa unaonekana ni mbaya.
Vikosi vya RSF pia vinauzingira mji mkuu wa jimbo la Kordofan Kaskazini, El-Obeid. Huko Kordofan Kusini, kundi la waasi, Sudan People's Liberation Movement-North, linaloendesha uasi wake kwa miaka 12 iliyopita, limesonga mbele kuelekea mji mkuu wa jimbo hilo, Kadugli, huku jeshi likipambana na RSF.
Mpango wa viongozi wa Afrika

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kuna msururu wa shughuli za kidiplomasia. Lakini hakuna makubaliano juu ya nani awe kiongozi. Tangu wiki ya pili ya mzozo huo, Marekani na Saudi Arabia zimekuwa zikiitisha mazungumzo ya kusitisha mapigano katika mji wa Saudi wa Jeddah. Lakini matumaini ya kusitishwa kwa uhasama - katika sikukuu ya Eid al-Adha - yamekuja na kupita bila kulegea kwa kasi ya vurugu.
Marekani na Saudi Arabia zimesema zitaleta pendekezo jipya katika siku zijazo. Pia wamefanya jitihada za kuleta Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwenye bodi, ambayo ni muhimu kwa sababu UAE inaonekana kama mfadhili mkuu wa RSF na, kulingana na baadhi ya ripoti, inaendelea kuwapa silaha. UAE haijatoa maoni yoyote kuhusu ripoti hizo.
Zaidi ya mwezi mmoja uliopita, viongozi wa Afrika Mashariki walizindua mpango wao wenyewe chini ya uangalizi wa chombo cha kikanda, Igad. Kikosi kilichoundwa na viongozi wa Kenya, Ethiopia, Sudan Kusini na Djibouti - kiliteuliwa kutafuta usitishaji vita, ufikiwaji wa watu wenye kuhitaji msaada na mazungumzo ya kisiasa ili kurejesha serikali ya mpito.
Rais wa Kenya William Ruto - ambaye anaongoza kundi hilo - amekuwa muwazi, akielezea vita hivyo "havina maana", na kulaani pande zote mbili zinazopigana kwa kutumia nguvu zao za kijeshi "kuangamiza nchi na kuua raia", na kuonya kwamba "tayari kuna dalili za mauaji ya kimbari" huko Darfur.
Ni kundi hili la viongozi, waliokutana katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa siku ya Jumatatu na walichukua hatua za kwanza za kuandaa kikosi cha uingiliaji kati wa kikanda.
Hatua yao ya pili ni kufanya kazi na Wamarekani na Saudi Arabia kuitisha mkutano wa ana kwa ana kati ya majenerali wanaopigana - Burhan na Hemedti - ili kupata usitishaji wa mapigano.
Hatua ya tatu ni "mchakato jumuishi wa kisiasa" utakaoanza ifikapo Agosti. Hilo linahitaji kuwaleta pamoja wawakilishi wa kiraia, na kuwapa uungaji mkono wa kutosha wa kisiasa ili wawe na sauti ya kweli katika mazungumzo, kama sehemu ya juhudi za kuhakikisha kuwa Sudan inarejea kwenye njia ya demokrasia.
Sudan inazidi kuyumba

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini Jenerali Burhan alikataa mpango huo, akidai kuwa Bw Ruto anaegemea upande wa RSF. Pia anawashutumu baadhi ya viongozi wa vyama vya kiraia kwa kuegemea upande wa Jenerali Hemedti. Kwanza alikubali, kisha akakataa, kuhudhuria mkutano wa Jumatatu. Mjumbe kutoka RSF alihudhuria.
Jeshi hakika lina madai makubwa ya ki serikali kuliko RSF, ambacho ni kikundi cha wanamgambo kinachoendeshwa na familia ya Dagolo, inayopata pesa kutokana na migodi yake ya dhahabu, kukodi mamluki na kufanya biashara. Imeungana na wakuu wa Kiarabu kutoka Darfur na nchi jirani.
Udhaifu wa Jenerali Burhan ni kwamba majeshi yake hayawezi kulinda taifa au watu. Kwa kweli hata hawadhibiti mji mkuu, kiwango cha chini cha kukubalika kama serikali halali barani Afrika.
Mzozo wa Sudan tayari unaiyumbisha Sudan Kusini. Jenerali Hemedti aliitaka Sudan Kusini kusitisha kuilipa serikali ya Sudan - ikimaanisha Jenerali Burhan - kwa matumizi ya bomba la mafuta hadi Port Sudan, njia pekee ya kuuza mafuta nje ya nchi na chanzo kikuu cha mapato cha nchi hiyo. Sudan Kusini bado haijatoa maoni yoyote kuhusu matakwa hayo.
Mwishoni mwa juma, Bw Ruto alisafiri hadi Chad kushauriana na Rais Mahamat Déby. Akiwa na hofu kubwa ya uwezekano wa mgogoro wa Darfur kuyumbisha nchi yake. Bw Déby alifanya mkutano na viongozi wa Darfuri, wakiwemo makamanda wa makundi ya zamani ya waasi.
Misri tayari inawahifadhi zaidi ya wakimbizi 250,000 wapya waliowasili kutoka Sudan. Inahofia kwamba uharibifu unaoendelea Khartoum unasababisha kuhama kusikoweza kuepukika kwa watu - Wamisri wanazungumza kuhusu milioni mbili na hata zaidi.
Rais Abdul Fattah al-Sisi alitangaza mpango wa pamoja na Qatar na anaitisha mkutano wake wiki hii. Misri iko upande wa Jenerali Burhan. Bw Sisi anaona Jenerali Burhan kama mshirika wake wa kutegemewa nchini Sudan.
Umoja wa Mataifa umetengwa. Mwakilishi wake maalum kwa ajili ya Sudan, Volker Perthes, alitangazwa na Jenerali Burhan kuwa mtu asiyestahili. Wasudan wengi wamesikitishwa na kushindwa kwa Umoja wa Mataifa nchini Sudan na hawataki kuiona ikiongoza juhudi za kidiplomasia.
Baadhi ya Wasudan wanalaumu EU kwa kuunga mkono RSF siku za nyuma kama sehemu ya mpango wa kudhibiti mipaka ya nchi - madai ambayo EU inapinga.
Changamoto ya amani nchini Sudan ni kubwa. Mpango wa viongozi wa Afŕika ni mzuri, lakini bado kuna vizuizi vingi katika njia ya amani – bila kusahau kukataa kwa pande zinazozozana kukubali kwamba hakuna suluhu la kijeshi kwa mzozo huo.












