Mzozo wa DRC: Congo yakaidi wito wa kufanya mazungumzo na M23

Mwanamgambo wa M23 katika mandhari ya kijeshi akiwa amebeba silaha begani mwake. Mpiganaji mwingine yuko kulia kwake na ameshikilia silaha chini ya mkono wake.

Chanzo cha picha, AFP

    • Author, Anne Soy
    • Nafasi, BBC News, Nairobi
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Licha ya shinikizo linalozidi kuongezeka kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekataa kufanya mazungumzo ya maridhiano waasi wa kundi la M23, ambalo limeteka maeneo makubwa mashariki mwa nchi katika miezi ya hivi karibuni.

Wiki iliyopita, serikali ya Uingereza ilitoa wito wa kuhusisha kundi la M23 katika "mazungumzo ya kujumuisha" kama sehemu ya juhudi za kupata suluhu ya kisiasa kwa mzozo huo.

Hata hivyo, katika mahojiano na BBC, Waziri Mkuu wa DR Congo, Judith Suminwa Tuluka, alisisitiza kuwa serikali yake inapendelea kuzungumza na Rwanda, nchi jirani ambayo inashutumiwa kwa kuuunga mkono M23.

Kwa mujibu wa mamlaka za Congo, zaidi ya watu 8,500 wamepoteza maisha tangu mapigano yalipoongezeka mwanzoni mwa mwaka huu.

Pia unaweza kusoma:

Mamia ya maelfu wamelazimishwa kuondoka makwao wakihofia usalama wao wakati wa vita, ambapo wataalam wa Umoja wa Mataifa na wengine wakiangazia Rwanda kama nchi inayopiga jeki vita hivi.

'' Cha muhimu ni kwamba anayeleta vurugu na kutishia uhuru wa DRC ni Rwanda,'' Suminwa Tuluka anasema akinukuu ripoti kutoka kwa wataalam wa Umoja wa Mataifa mwaka jana ambayo ilitaja vikosi kati ya 3,000 na 4,000 vya Rwanda vilivuka katika mpaka wa Congo na vilisaidia wanamgambo wa M23.

Mazungumzo ya amani yaliyokuwa yakiongozwa na Angola mwaka jana mwezi Disemba yaligonga mwamba baada ya Rwanda kutaka serikali ya Congo izungumze moja kwa moja na waasi wa M23.

Waasi hao baadaye walionekana kuzidisha nguvu na kuteka baadhi ya miji mkuu kama vile Goma na Bukavu mwezi Januari na Februari mtawalia.

Katika juhudi za pamoja za kutafuta suluhu zilizoanzishwa na mataifa ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, viongozi wake walitoa wito wa kusitisha mapigano, na kuondoka kwa '' vikosi vya kijeshi vya kigeni ambavyo havikualikwa'' kutoka Congo na pia kutaka pande zote mbili kukaa pamoja kusuluhisha.. wakijumuisha M23''.

Rais wa Rwanda hata hivyo hakukana uwepo wa vikosi vyake DRC alipoulizwa.

'' sijui hayo'', alisema katika mahojiano na shirika la CNN.

Mapigano ambayo yanaendelea nchi jirani yamesababisha taifa lake ambalo lilikuwa linapendelewa na mataifa ya Magharibi uhusiano wake kuyeyuka kwa haraka.

Shinikizo limezidi dhidi yake kuondoa vikosi vyake vya kijeshi nchini Congo.

''Lakini hili halijatekelezwa kufikia sasa,'' Suminwa Tuluka anasema.

Picha yakaribu ya Waziri Mkuu Judith Suminwa Tuluka

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Waziri mkuu Judith Suminwa Tuluka ailaumu Rwanda kwa kuwa kizingiti cha mazungumzo ya maridhiano kufanyika
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Waziri mkuu Suminwa amekaribisha vikwazo vya Marekani dhidi ya Rwanda akitaja hili litachochea '' kushinikiza wanaosumbua Congo''.

Kwa upande wa Rwanda wamepuuzilia mbali vikwazo hivyo wakivitaja sio vya msingi kwani havitatuliza mzozo uliopo.

Tume ya Ulaya kwa upande wake imesitisha 'ushauri wa ulinzi' na kuanza '' kutathmini upya'' mkataba wa maelewano ambao walitia saini mwaka jana na Rwanda kuhusu malighafi.

Waziri huyo wa Congo pia ameunga mkono uamuzi wa Tume ya Ulaya akisema ''uchimbaji wa rasilimali wa haramu ni moja ya sababu za mzozo kuendelea''.

DRC imelaumu Rwanda kwa kuchukua madini yake kwa njia isiyo halali katika eneo la Takihe, mashariki mwa Congo, dai ambalo Rwanda limekanusha.

Vikwazo zaidi dhidi ya Rwanda, ya hivi karibuni ni Uingereza kutangaza wiki jana kuwa mikakati yakudhibiti mzozo huu ni kusitisha msaada kwa Rwanda isipokuwa fedha zinazotegemewa na masikini na makundi yanayo uhitaji zaidi, hadi pale Rwanda itaondoa vikosi vyake DRC na kuingia katika mazungumzo ya amani na mapigano kusitishwa .

Rwanda ilielezea kuwa uamuzi huo ni kama 'maonevu' ikisema sio sawa kutarajiwa kuhatarisha usalama wake.

Waziri huyo wa Congo amesema Rwanda imekuwa ikipuuza wito wa kuondoa vikosi vyake nchini Congo.

''Sasa ni nani anakuwa kikwazo wa kutatua mzozo? sio serikali ya Congo,'' anaeleza.

Rwanda imekuwa ikikiri kutuma vikosi vyake '' ikijitetea vikali'' wakati vita vikiendelea, ikisema ina haki ya kulinda usalama wa nchi yake.

Pia imekuwa ikilaumu serikali ya Congo kwa kuhifadhi na kufanya kazi na kundi la wanamgambo la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), ambalo wanachama wake waliwahi kuwa wapiganaji wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Alipoulizwa kuhusu hilo, Suminwa Tuluka alikanusha kuwa jeshi la Congo linafanya kazi na waasi wa FDLR, lakini alisema nchi yake itashiriki katika mchakato wa "kuwazuia" wapiganaji hao.

Na suala la kutatua mgogoro uliopo iwapo mazungumzo ya maridhiano na M23 yataambulia patupu, waziri mkuu amesema kuingia kwa mazungumzo na Rwanda itakuwa ni jibu la haraka la kusitisha mapigano.

''Wahakikishe vikosi vya Rwanda vimeondoka Congo na waasi wa M23 wakome kuua raia wa DRC,'' anasema.

Mada zinazofanana:

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid na kuhaririwa na Ambia Hirsi