Chaneli ya WhatsApp ya BBC Swahili: Jinsi ya kujiunga na kupata taarifa bora za habari

Chanzo cha picha, Getty Images
Sasa unaweza kupata habari muhimu zinazochipuka, uchambuzi na makala maalum kupitia BBC News Swahili moja kwa moja kwenye WhatsApp yako.
Wanahabari wetu wanatarayarisha habari bora za ndani na za kimataifa katika maandishi na video hasa kwa wafuasi wa chaneli yetu mpya kwenye programu ya kutuma ujumbe ya WhatsApp.
Ilianzishwa mnamo 2023, Chaneli za WhatsApp huruhusu watumiaji kupokea sasisho kutoka kwa watu na mashirika wanayovutiwa nayo. Ilizinduliwa mnamo Septemba 2023,Chaneli ya WhatsApp ya BBC nchini Uingereza imefikia zaidi ya wafuasi milioni 1.3.
Sasa wasomaji wetu Afrika Mashariki na kote duniani wanaweza pia kupata maudhui bora zaidi ya BBC Swahili kwenye simu zao.
Bofya hapaili kujiunga na chaneli yetu ya WhatsApp ikiwa unatumia simu yako ya mkononi au Wavuti ya WhatsApp.
Ikiwa unasoma hili kwenye kompyuta yako, changanua tu msimbo wa QR iliyo hapa chini na itakupeleka moja kwa moja kwenye chaneli

Unaweza pia kutafuta BBC News Swahili chini ya kichupo cha "Sasisho" /Updates' kwenye WhatsApp.
Unaweza kupata kichupo cha "Sasisho" chini kushoto mwa skrini yako ikiwa unatumia iPhone, au juu ya skrini yako ikiwa unatumia Android.
Hapo ndipo ujumbe wetu wote utaonekana - tofauti na kichupo chako cha kawaida cha "Soga".
Bonyeza kengele juu ya Chaneli na uiwezeshe ili usikose masasisho yoyote. Unaweza kunyamazisha tena au kujiondoa kwenye chaneli wakati wowote.
Unaweza kuitikia taarifa zetu kwa kutumia emojis na kusambaza bora zaidi kwa watu unaowasiliana nao na vikundi vyako kwenye WhatsApp.
Meta, mmiliki wa WhatsApp, Facebook na Instagram, anasema kuwa hakuna mtu katika chaneli hiyo anayeweza kuona maelezo yako ya mawasiliano, picha, jina au nambari yako ya simu.
Fahamu zaidi kuhusu faragha yako kwenye Notisi ya Faragha ya Jumuiya ya WhatsApp ya BBC












