Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini maharage yanaweza kuwa suluhisho la matatizo mengi duniani?
Binadamu wanakabiliwa na vitisho vingi, kuanzia mabadiliko ya hali ya hewa, utapiamlo hadi kupanda kwa gharama ya maisha. Je, maharage yanaweza kuwa jibu la matatizo ya kimataifa?
Jamii hii ya kunde ni sehemu muhimu ya karibu kila utamaduni duniani, na kwa sababu nzuri.
Maharage yakiwa na takriban aina 40,000 tofauti, hizi ni aina nyingi sana, zenye lishe, na hayana gharama na ni rafiki kwa mazingira.
Ikiwa hauna uhakika wa kuyala kama mboga au protini kwenye sahani yako, jibu ni kwamba maharage yanaweza kuliwa kama mboga ua protini au zote mbili.
Kwa mfano, mbaazi na maharagwe ya snap huchukuliwa kuwa mboga za wanga, wakati maharagwe yenye rangi nyeusi yako katika makundi yote ya chakula kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha protini.
Katika ulimwengu ambao watu bilioni 2.5 wana uzito wam wili wa kupita kiasi, wanene au wana utapiamlo, maharagwe ni chakula chenye kila aina wa lishe.
Sio tu kwamba ni mbadala wa bei nafuu kwa bidhaa za wanyama, lakini pia huwa hayana mafuta na yana virutubisho vingi, pamoja na protini, chuma, zinki na nyuzi nyuzi (fibre).
Zaidi ya hayo, yana kabohaidreti zisizoweza kuyeyushwa ambazo hulisha bakteria kwenye utumbo mpana, hivyo kuwafanya bakteria hawa kuwa bora kwa matumbo yetu yetu.
Mikunde yote ina mchanganyiko wa amino asidi muhimu, na kati yake soya hujitokeza kwa kuwa na uwiano bora kwa afya zetu.
Jamii hizi nyingne za kunde huwa hazina uwiano sawa, lakini duniani kote ni jambo la jadi kuliwa na vyakula vingine ili kuifanya lishe kwenye sahani iwe kamili.
Fikiria maharagwe, wali wa dengu, mbaazi na couscous na chapati.
Gesi
Wakati maharagwe yanajulikana kwa jukumu lake katika, utoaji wa gesi, yanaweza pia kufanya kinyume chake.
Mimea hii ina jukumu la kipekee na muhimu katika mifumo ikolojia muhimu kama vile misitu, nyasi na ardhi yenye unyevunyevu.
Bakteria walioko kwenye mizizi yake hufyonza nitrojeni kutoka angani na kuihifadhi kwenye udongo.
Utaratibu huu, unaojulikana kama urekebishaji wa nitrojeni, sio tu hutoa virutubisho kwa miti na mimea mingine, lakini pia hufanya kazikama mbolea ya asili katika kilimo, kupunguza uchafuzi wa kemikali.