Ligi ya Premia: Mashtaka ya kifedha dhidi ya Manchester City yanamaanisha nini?

Chanzo cha picha, Getty Images
Uamuzi wa Ligi Kuu ya Uingereza kuishtaki Manchester City kwa kuvunja sheria zake za kifedha umeshtua mchezo wa soka nchini humo.
Mabingwa hao wa Premier League wamekuwa na nguvu kubwa katika soka la Uingereza katika miaka ya hivi karibuni, wakishinda mataji sita ya ligi tangu walipotwaliwa na Kundi la Abu Dhabi United mwaka 2008.
Lakini City wamefikaje hapa? Je, gharama yake ni kiasi gani? Na je ni kweli wanaweza kufukuzwa kwenye Ligi Kuu?
BBC Sport inajibu maswali muhimu.
Kwanini Man City wanashtakiwa?
Baada ya uchunguzi uliodumu kwa zaidi ya miaka minne, Ligi ya Premia ilitoa taarifa Jumatatu ikisema kuwa imeishtaki City kwa ukiukaji wa zaidi ya sheria 100 za kifedha kutoka 2009 hadi 2018.
"Kwa upande wa mashtaka, kuna maeneo mawili," mtaalam wa fedha wa kandanda Kieran Maguire aliiambia BBC Radio 5 Live's Monday Night Club.
"Kwanza, shutuma kwamba Manchester City waliingiza fedha kwa njia ya udanganyifu katika klabu, hasa kuhusiana na mikataba ya kibiashara na udhamini. Ligi ya Premia inaonekana kudai kuwa pesa hizo zilitoka kwa mmiliki wa klabu, jambo ambalo halihusiki na FFP. (financial fair play), lakini yalikuwa yanafichwa kama mapato ya ufadhili, ambayo yanahesabiwa kuelekea FFP.
“Mashtaka mengine yanahusiana na Manchester City kudaiwa kufidia gharama za uendeshaji wa klabu kwa kuwa na mameneja kwenye mikataba na kampuni nyingine iliyohusishwa na wamiliki ili waweke tu sehemu ndogo ya gharama halisi ya kusimamia klabu katika vitabu yake vya fedha ."
Je klabu ya City ilifikaje hapa?
Mnamo Novemba 2018, gazeti la Ujerumani Der Spiegel lilichapisha nyaraka zilizovuja zinazodai City iliongeza thamani ya mkataba wa udhamini na kuipotosha Uefa kimakusudi ili waweze kukidhi sheria za FFP ambazo zinahitaji vilabu kuwa na usawa.
Kufuatia madai hayo, Uefa ilianzisha uchunguzi na kuamua mwaka 2020 kwamba City ilifanya "ukiukaji mkubwa" wa kanuni za FFP kati ya 2012 na 2016.
lakini, hukumu ya marufuku ya miaka miwili kutoka kwa mashindano ya Uropa ilibatilishwa na Mahakama ya Usuluhishi wa masuala ya Michezo (Cas) baadaye mwaka huo.
Uchunguzi wa Ligi ya Premia ulianza Desemba 2018. City ilisema madai hayo ni "uongo kabisa" na kwamba madai katika Der Spiegel yalitokana na "udukuzi haramu na uchapishaji wa barua pepe za City nje ya muktadha".
Kwanini sasa?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
City ilisema hawakupewa onyo la mapema kuhusu Taarifa hiyo iliotolewa na ligi kuu ya England wiki hii.
Walihoji kuhusu wakati wake – hususana wakati ambapo serikali ya Uingereza inataka kuchapisha sheria kuhusu usimamizj wa soka mwezi huu. Inaonekana kwamba sababu ya ujio wa kesi hiyo ni kutumika na ligi ya premia kama Ushahidi kwa kukabiliana na matatizo ya usimamizi wa klabu badala ya kupendekeza usimamizi huru.
Itakuwa vyema kwa ligi kuonekana kuwa na makali na kukabiliana na mwanachama na mwanahisa
"It would be good for the league to be seen to have some - hivyobasi tunaingia katika mgumo wa kupiga kampeni na siasa . Inashangaza kwamba masuala haya mawili yanafanyika katika wakati mmoja , alisema Maguire.
"Kuna usanii mwingi wa kisiasa unaondelea gizani na soka inatumika kama chombo cha hili. Tumekuwa na kipindi cha kujidhibiti ndani ya soka na hiyo imetufikisha hapa tulipo."
Mhariri wa michezo wa BBC Dan Roan alisema: "Ni rahisi kuona ni kwa nini watu wa ndani wa City wanashuku kuhusu wakati.
"Wakati muda unatiliwa shaka , idadi kubwa ya mashtaka labda inaonyesha kwa nini imechukua muda mrefu kwa Ligi Kuu kufikia hapa.
"Hata hivyo, wengi watasema pendekezo kwamba hili linahusishwa na mdhibiti wa soka kucheleweshwa kama jambo lisilowezekana. Baada ya yote hayo, ukweli ni kwamba imechukua Ligi Kuu miaka minne kuleta mashtaka yanayoimarisha kanuni badala ya kuzidhoofisha.
"Zaidi ya hayo, kama Ligi Kuu ya Uingereza ingetaka kutuma ujumbe kwa serikali kwamba inaweza kujidhibiti, bila shaka ingechukua hatua hii muda mfupi uliopita, kabla ya mipango ya mdhibiti kukamilishwa."
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Je, hii ina umuhimu gani?

Chanzo cha picha, Getty Images
"Hii inaweza kuwa kashfa kubwa zaidi ya kifedha katika historia ya Ligi Kuu," Roan alisema. "Hakuna klabu iliyowahi kukabiliwa na orodha ya mashtaka kama hii.
"Iwapo udanganyifu utathibitishwa itakuwa hatari kwa nguvu kubwa katika mchezo wa Kiingereza, kwa wamiliki wake wa Abu Dhabi, kwa dhana ya klabu zinazomilikiwa na serikali na wazo zima hili ni ushindani wa haki.
"City pia inaweza kumpoteza Pep Guardiola, meneja huyo alionya mwaka jana kwamba angejiuzulu ikiwa itabainika kuwa klabu ilimpotosha kwa kukana kuvunja sheria.
"Hii inaweza kudumu kwa miezi kadhaa na kuleta wingu kubwa kwenye Ligi Kuu katika mchakato huo."
Maguire alisema: "Ikiwa Man City wana hatia, kumekuwa na shutuma dhidi ya vilabu vingine na je, hatua hii itafanya suala hilo kuongezeka nguvu?
"Vilabu vingine vimekuwa vikishawishi dhidi ya Man City. Je, hii sasa inaleta mfano mbaya katika ulimwengu wa Ligi Kuu ambapo kila mtu anamnyooshea mwenzake kidole."
City wamesema nini?
City wanasema "walishangazwa" na mashtaka hayo, kwa sababu ya kile wanachosema "ushirikiano mkubwa na nyenzo nyingi za kina" wanazodai zilitolewa kwa Ligi Kuu.
"Klabu inakaribisha uchunguzi wowote wa suala hili na tume huru, kwa kuzingatia bila upendeleo chombo kamili cha ushahidi usioweza kukanushwa ambao upo kuunga mkono msimamo wake," ilisoma taarifa.
"Kwa hivyo tunatazamia jambo hili lisitishwe mara moja na kwa wote."
City wanafahamika kujiamini katika nafasi yao, na hiyo inajumuisha mashtaka ambayo yalizuiliwa kwa muda katika kesi yao ya Uefa. Wanaamini walitoa ushahidi unaofaa kuhusu mashtaka hayo kwenye Ligi Kuu muda uliopita.
Je nini kitatokea kwa Man City?
Ligi ya Premia imeipeleka City kwa tume huru kwa madai ya ukiukaji wa kanuni.
Shughuli za tume hiyo - inayoongozwa na Murray Rosen KC - zitakuwa za siri na kusikilizwa kwa faragha.
Baada ya tume kufanya uamuzi wake rufaa inaweza kukatwa kwa bodi tofauti ya rufaa ndani ya Ligi Kuu, anasema wakili wa sheria za michezo Ashley Cukier.
"Wakati huo, kwa ujumla, hapo ndipo mchakato utaisha," Cukier alisema.
"Siyo kama Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (Cas) ambapo mambo yanaweza kuongezeka hadi kufikia kiwango cha Ulaya. Hili ni suala la Ligi Kuu ambalo litashughulikiwa ndani ya nchi."
Adhabu gani zinapatikana?
Iwapo City itapatikana na hatia ya kukiuka kanuni, tume inaweza kutoa adhabu kuanzia faini na kukatwa pointi hadi kufukuzwa Ligi Kuu.
"faini itakayopigwa haina kikomo," Maguire alisema.
"Inaweza kuwa kitu chochote kuanzia 'usifanye tena', faini, kukatwa pointi, kuwanyang'anya Man City mataji, hata kuwafukuza kwenye Ligi Kuu."
Mnamo 2011 QPR iliepuka kukatwa pointi lakini ikatozwa faini ya pauni 875,000 baada ya kupatikana na hatia kwa kukiuka kanuni za uhamisho, huku Leicester na Bournemouth zikipokea faini kwa kukiuka sheria za FFP zilipopanda daraja hadi Ligi ya Premia msimu wa 2013-14 na 2014-15 mtawalia.
Wakati Rangers inaingia katika utawala mwaka 2012, usajili wake na FA ya Uskoti na Ligi Kuu ya Uskoti ulikatishwa na kulazimika kuanza tena chini kabisa ya piramidi ya soka.
Mwezi uliopita Juventus ya Italia ilipandishwa kizimbani na kukatwa pointi 15 kwenye Serie A kufuatia uchunguzi kuhusu uhamisho wa wachezaji.
"Sioni kizuizi chochote katika kile wanachoweza kufanya katika suala la vikwazo," Cukier alisema.
"Swali kwa tume itakuwa ni adhabu gani inahisi inafaa."












