Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Malkia Elizabeth II: Maisha ndani ya Land Rovers
Katika maisha yake yote, Malkia alipigwa picha akiwa anaendesha gari aina ya Land Rover. Magari haya yalikuwa maalum kwa familia ya kifalme, ambayo hata ilitumika kubeba jeneza la Mwanamfalme Philip alipokufa.
Uhusiano wa kudumu wa wanandoa hao na magari ya Jaguar Land Rover (JLR) ulikuwa kama "sehemu ya DNA ya Familia ya Kifalme," mwandishi wa habari wa magari Quentin Willson alisema.
Kampuni hiyo ilishikilia idhini ya kifalme tangu mwaka 1951 baada ya kutoa Land Rover kwa mara ya kwanza kwa Mfalme George VI.
"Kulikuwa na uhusiano huu mkubwa kati ya Jaguars na Land Rovers na R familia ya Kifalme," Bw Willson alisema.
Mara tu baada ya kutawazwa kwake, Malkia na Mwanamfalme Philip walionekana wakifanya shughuli za kifalme kwa kutumia Land Rovers zilizobadilishwa maalum "na unaweza kuona kwamba ilikuwa upendeleo kwao," Bwana Willson alisema.
Magari yaliyobadilishwa "labda yalikuwa na muundo uliopendekezwa na Mwanamfalme Philip," alielezea. "Siku zote alikuwa akiyapenda sana (magari haya)."
Magari ya Land Rovers yaliyobuniwa na kutengenezwa West Midlands, yalitumika kuwabeba wanandoa hao katika ziara yao ya miezi sita ya Jumuiya ya Madola mnamo 1953, wakienda Bermuda, Jamaika, Fiji na Australia.
"Sio tu gari zuri, lakini hili ndilo gari ambalo watu wengi walimwona Malkia wao kwa mara ya kwanza," Stephen Laing, afisa katika Makumbusho ya Magari ya Uingereza, huko Gaydon, Warwickhire, alisema.
"Mimi na wenzangu tunapita kila siku kwenye gari hizi, na tunajua kuwa ni za kipekee kwa sababu ni gari za Malkia. "Ni sehemu muhimu sana ya historia ya uhusiano wa Malkia na tasnia ya magari ya Uingereza."
"Katika maisha yao yote ungeweza kuona kuwa haya hayakuwa magari ya sherehe tu, bali yalikuwa magari ambayo waliendesha wenyewe kwenye mashamba," alisema Bw Willson. Malkia aalikuwa akionekana kwenye picha mara kwa mara kwenye magari haya "na ilikuwa wazi kuwa alikuwa akiyapenda sana." "Walipenda magari na walipenda West Midlands," alielezea, na walitembelea mara kwa mara viwanda vya kampuni hiyo kwenye huko Coventry na Solihull.
Mtangazaji huyo wa zamani wa Top Gear alisema alikuwa na bahati ya kujaribu kuendesha moja ya magari hayo mazuri ya Malkia, P5B kwenye jumba la makumbusho la magari ya Uingereza.
"Nilijua malkia alikuwa na gari hili zuri la kijani kibichi, ilikuwa yake ya binafsi ambayo alizunguka nalo na ambalo lilikuwa llimetengenezwa mahsusi kwa ajili yake. "Ujumbe ulitumwa kwa familia ya kifalme, na kurudi kwamba Malkia atafurahi ikiwa ungeendesha gari lake kuu la zamani," Bwana Willson alisema.
"Kwa hivyo niliruhusiwa kuendesha gari hili barabarani na kupiga nalo picha, ilikuwa jambo zuri tu."
Duke wa Edinburgh, ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 99 mnamo Aprili 2021, alishiriki katika uundwaji wa gari la kubeba maiti la Land Rover liliboreshwa ili kubeba jeneza lake.
Alianza kuliunda kwa ushirikiano na JLR mnamo 2003, akirekebisha sehemu ya juu ya nyuma ambapo jeneza lake liliwekwa.
Magari haya yalizidi kupata umaarufu lilipoonekana likiwabeba Barack na Michelle Obama kwenye gari lake la Range Rover wakati wa ziara yao huko Windsor mnamo 2016.
Pamoja na Jaguar, Land Rover ilikuwa mtengenezaji pekee wa magari aliyekuwa anawajibu wa kutoa huduma ya magari kwa warantii kwa Malkia, Duke wa Edinburgh na Mkuu wa Wales.
Chapa hiyo ilikuwa "sahihi kabisa" kuonyesha enzi ya Malkia, Bwana Willson aliongeza. "Alifanya vitu kwa kudumu, alivihifadhi kwa muda mrefu, hiyo ni sehemu ya tabia yake, hakuwa na fujo. "Na nadhani huo ni ujumbe mzuri, na unaonyesha mtazamo wake kwa nchi yake na jukumu lake kama mtu huru."
Katika taarifa yake, JLR ilisema kifo cha Malkia kiliacha kila mtu kwenye kampuni hiyo "amehuzunishwa sana". "Uhusiano wetu na Malkia umekuwa chanzo cha kujivunia kwa wote."