Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Video za droni zilizorushwa na Hezbollah zaonesha jinsi kundi hilo lilivyobadili mfumo wa kuishambulia Israel
Kundi la Hezbolla limeongeza matumizi ya aina ya ndege isiyokuwa na rubani yaani Droni ambayo inajulikana kama {First Person View – FPV}kuishambulia Israel.
Droni hizo ndogo, zimetumiwa sana na wapiganaji wa Kundi hilo la Hezbollah, katika operesheni zao dhidi ya Israel na zinatumia mfumo wa mawasiliano unaotegemea nyaya za fibre optiki ambazo zina uwezo wa kukwepa mfumo wa ulinzi wa angani wa Israel.
Kitengo cha uchunguzi na kuthibitisha data na taarifa cha BBC Verify kimefanya tathmini ya kina kuangazia video 35 ambazo zimechapishwa na Kundi hilo la wanamgambo kutoka Lebanon tangu Machi 26.
Katika video hizo, Kundi hilo limeonyesha jinsi ilivyotekeleza mashambulizi dhidi ya wanajeshi, magari ya kijeshi na mfumo wake wa ulinzi wa angani, katika eneo kuu la Kusini mwa Lebanon na Kaskazini mwa Israel.
Wataalamu wameiambia BBC Verify kwamba Jeshi la Israel {IDF} kwa sasa halijaweza kubuni mpango dhabiti wa kukabiliana na mbinu hii mpya ya Kundi la Hezbollah, kwani Droni hizo ambazo ni ndogo mno zinaweza kukwepa kutambuliwa kwa urahisi na mifumo ya ulinzi.
End of Unaweza kusoma
Matumizi ya droni hizo za FPV ambazo zinanunuliwa kwa bei ya chini, imeongezeka sana hasa katika vita vingine kati ya Urusi na Ukraine, na vimebadili mfumo wa kisasa wa vita.
Japo jeshi la Israel halijachapisha wala kutangaza idadi ya wanajeshi wake waliouawa katika mashambulizi hayo ya Hezbollah, vyombo vya habari nchini Israel vimeripoti kwamba wanajeshi wanne wa IDF na raia mmoja waliuawa katika shambulizi la droni ya FPV, huku wengine wengi wakijeruhiwa.
Jeshi la Israel, limeiambia BBC Verify kwamba linatambua tishio ambalo droni hizo linatoa kwa wanajeshi na operesheni zake na limetaja kwamba lina 'wekeza' katika silaha na mbinu muhimu zitakazo isaidia kudhibiti mfumo wake wa ulinzi, kubuni pia mfumo wa kisasa wa kutahadharisha dhidi ya hatari na kuwapa wanajeshi wake mafunzo kuwatayarisha vyema kutambua tishio na kukabiliana nalo.
Kulingana na tasisi ya mafunzo ya usalama wa kitaifa {NSS}, Jeshi la Israel pia limekuwa likitumia Droni hizo za FPV kwa miaka mingi , na wanajeshi wake bado wanazitumia katika operesheni yake kusini mwa Lebanon na pia dhidi ya Kundi la Hamasa huko Gaza.
Hisham Jaber, mchambuzi wa masuala ya Kijeshi, na aliyehudumu kama Jenarali kwenye Jeshi la Lebanon, ameiambia idhaa ya Kiarabu ya BBC kwamba
Droni za FPV 'sio rahisi kutambuliwa kwenye rada,' na idadi kubwa yazo zilizo mikononi mwa Kundi la Hezbollah zimetumika kuharibu injini za magari ya kivita – zikiwemo vifaru.
Hezbollah imekuwa ikutumia aina kadhaa ya ndege hizo zisizo na rubani zilizokubwa kidogo , dhidi ya shabaha kadhaa ilizolenga Kaskazini mwa Israel kwa miaka mingi. Jaber pia amesema kwamba matumizi ya FPV ni mbinu mpya kabisa.
BBC Verify imepata video za takribana mashambulizi 100 yanayooenekana kutekelezwa na Droni za FPV. Video hizo zimechapishwa katika chaneli ya mtandao wa kijamii wa Telegram ya Kundi hilo la Hezbollah, tangu Machi 26.
Video 35 kati ya hizo, zimeshathibitishwa. Hezbollah hainonekani kama imechapisha picha nyinginezo kuhusu vita ambavyo vilianza Machi 2.
IMAGE:
Maeneo yaliyothibitishwa kuwa Hezbollah ilitekekeza mashambulizi kwa kutumia Droni za FPV.
Video moja iliyothibitishwa na iliyochapishwa siku ya alhamisi, inaonyesha droni nne zilishambulia kituo cha kijeshi kilichoko karibu na Kryat Shmona kwenye mpaka wa Lebanon. Magari kadhaa ya kijeshi yalilengwa katika shambulio hilo huku mbili zinaonekana kuharibika kabisa kwenye video hiyo.
BBC Verify, pia imefuatilia mashambulio kama hayo ya droni yaliyotokea kusini mwa Lebanon, ikiwa ni pamoja na mashambulizi mawili yaliyotekelezwa Aprili 26 katika mji wa Taybeh.
Video hizo, zinaonyesha wanajeshi wakilengwa, ikifuatwa na shambulizi lililolenga ndege aina ya Helikopta ya jeshi la Israel, ambalo lilikuwa likitekeleza operesheni ya kuwaokoa wanajeshi waliojeruhiwa na kuchukuwa maiti ya mmoja aliyeuawa.
Ndege nyingi aina hizo zisizo na rubani hupeperushwa kwa kutumia Nyaya za fibre – otiki badala ya kutegemea mawimbi ya radio au ain nyingezo za pasiwaya – hali hii inazifanya kuwa ngumu kutambuliwa zinapopaa na kukabiliwa na mifumo ya Kieltroniki ya Israel.
Dkt Andreas Krieg, ambaye ni mtaalamu wa usalama kutoka Chuo cha King's London, ameiambia BBC Verify kwamba nyaya za Fibre optiki zinatatiza uwezo wa jeshi la Israel kutambua , kusambaratisha mawasiliano kati ya droni na wanayezipeperusha na kufanya uwezo wa anayeziendesha kuwa ngumu.
Athari za hali hii kulingana na Krieg, ni wanajeshi wa Israel kulazimika kuchukuwa tahadhari kubwa kabisa katika mipango yake hasa ikiwa itailazimu kubadili operesheni yake ya makabiliano , na ile ya kujilinda kama vile kutumia neti za vyandarua na vizimba, na kuzingatia zaidi ulinzi wa karibu wa eneo hilo.
Krieg aidha aliongezea kuwa Hezbollah ina uwezekano mkubwa wa kutengeneza ndege zisizo na rubani ndani ya nchi kutoka kwa vifaa vinavyopatikana kutoka maeneo kama China kwa gharama ya kati ya Dola 300 na 500 za Marekani.
Leone handavi ambaye ni mpelelezi mkuu na mtalaamu wa matumizi ya silaha katika kituo cha {Centre for Information and Resilience} amesema kwamba vipande vya kutengeneza droni hizo zinazouzwa katika soko la viungo vya silaha zinatumiwa kwa pamoja na vipande ambavyo vimechapishwa kwa kutumia mfumo wa mashine za printa za 3D.
Kutambua vilipotoka viungo vya vipande hivyo muhimu kumekuwa changamoto kubwa sana kwa sababu ya jinsi kuna urahisi mkubwa wa kuvipata katika masoko ambayo sio ya kijeshi. Mara nyingi, droni za FPV zinabeba mabomu aina ya makombora aina ya RPG {Rocket propelled grenade} au mengine aina ya {WAR HEAD} yenye uwezo wa kusababisha hasara kubwa ambayo kwa sasa yapo kwa wingi kusini mwa Lebanon.
Handavi ameiambia BBC Verify kwamba ' madhara ya kisaikolojia' ya kuongezeka kwa mashambulizi ya FPV inajidhihidrishwa kwa ukubwa miongoni mwa wanajeshi wa Israel, kutokana na uwezo wa droni hizo kulenga magari ya kijeshi ambayo kwa kawaida huwa chini ya ulinzi mkali.
Makabiliano ya kivita kati ya Israel na Hezbollah yalianza machi 2, siku mbili baada ya Marekani na Israel kuanzisha mashambulizi ya anga nchini Iran, na kumuua kiongozi Mkuu wa taifa hilo Ayatollah Ali Khamenei.
Kufuatia, kifo cha Khamenei, Hezbollah ilirusha makombora ndani ya Israel – na jeshi la Israel likajibu kwa kutekeleza mashambulizi makubwa ya anga nchini Lebanon na pia kufanya operesheni ya ardhini katika eneo la kusini mwa Lebanon.
Wizara ya afya ya Lebanon imesema kwamba takriban watu 2,896 wameuawa tangu kuanza kwa vita hivyo, ikiwa ni pamoja na wengine 400 waliouawa katika muda ambapo kumekuwa na kusitishwa kwa vita – hali iliyotangazwa na Rais wa Marekani Donald Trump mwezi Aprili. Takwimu za wizara ya afya hazijatofautisha kati ya idadi ya raia waliofariki kutoka kwa idadi ya wapiganaji waliouwawa kwenye makabiliano hayo.
Watu zaidi ya milioni moja, wamekimbia makazi yao nchini Lebanon, tangu mzozo huo uanze.
Israel inasema wanajeshi wanne na raia 18 wameuawa katika mzozo huo.