Ni ‘makombora’gani hayawezi kuua mara moja, yanaweza kuua baada ya muda

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 6

Ingawa wanadamu wamehusika katika vita kwa maelfu ya miaka, majadiliano juu ya athari za wanadamu kwa mazingira ya asili, hasa kutokana na vita hivi yameanza kusambaa katika miaka michache iliyopita.

Vita vya kwanza vya Ghuba wakati visima vya mafuta 700 vilipowaka moto huko Kuwait mapema 1991 - ilikuwa moja ya matukio muhimu zaidi ya kuonyesha gharama ya mazingira ya vita vya silaha.

Moshi ulifuka na kuenea umbali wa maili 800, na mapipa milioni 11 ya mafuta yasiyosafishwa yalimwagika katika Ghuba, na kuunda mstari wa maili tisa baharini.

Katika ardhi, maziwa 300 ya mafuta yaliundwa jangwani, na kuuharibu udongo kwa miongo kadhaa, kulingana na taarifa ya Umoja wa Mataifa.

Zaidi ya miaka 30 baada ya vita, "athari za moto huo bado zipo, na zaidi ya asilimia 90 ya udongo uliochafuliwa bado upo wazi na hewa kutoka kwenye udongo huo inaweza kusambazwa."

Lakini kwa "mara ya kwanza" mtu yeyote amejaribu kutoa maelezo kamili ya uzalishaji wa gesi chafu kutokana na vita ilikuwa ni baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, kwa mujibu wa Doug Weir, mkurugenzi wa shirika la uangalizi wa migogoro na mazingira lenye makao yake nchini Uingereza.

Nchi za Magharibi zinapendelea "kuzungumza kuhusu jinsi mabadiliko ya hali ya hewa yanavyoathiri usalama wao, badala ya jinsi uchaguzi wao wa kivita unavyoathiri mabadiliko ya hali ya hewa," mtaalamu huyo anaelezea katika mazungumzo na BBC Idhaa ya Kiarabu.

Wengine wanaweza kufikiri kwamba athari za vita ni ndogo kwa maeneo ambayo vita hufanyika, lakini kiwango cha athari za operesheni za kijeshi ni zaidi ya kile tunachofikiria.

Unaweza pia kusoma:
g

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Mashamba ya mafuta ya Kuwait yalichomwa moto mwaka 1991 wakati wa Vita vya Kwanza vya Ghuba

Dag Weir anasema kuwa matokeo ya mazingira ya vita vya silaha mara nyingi hudumu "kwa miongo kadhaa, kwasababu kuna machache , kama yapo yanayofanyika katika kujitolea kwa upande wa nchi kushughulikia uharibifu huu."

Kwa mfano, anasema, athari za Vita ya Kwanza ya Dunia bado zinaweza kuonekana kwenye mandhari ya kaskazini mwa Ufaransa karne moja baadaye, ikiwa ni pamoja na uchafuzi wa mabaki ya mabomu na sumu za vita.

Pia anasema kuwa mazingira asili ya nchi nyingi za Mashariki ya Kati bado yana makovu ya migogoro, na kwamba mabaki ya migogoro hii hayajaathiri tu eneo ambalo mapigano yalitokea, lakini pia yameenea katika maeneo mengine "kutokana na ukosefu wa usimamizi mzuri wa mazingira."

Wanyama na ndege pia wanateseka

f

Chanzo cha picha, REX/Shutterstock

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wakati wa makabiliano ya sasa kati ya Israel na Hezbollah nchini Lebanon, maeneo ya kijani katika miji ya mpakani ya kusini mwa Lebanon yaliharibiwa vibaya na moto ambao wakati mwingine ulidumu kwa siku kadhaa, na kwasababu timu za ulinzi wa raia hazikuweza kuzifikia, ziligeuka kuwa ardhi tupu isiyo na miti au mimea.

Nadim Farajallah, ambaye ni mhandisi wa mazingira na afisa mkuu wa uendelevu katika Chuo Kikuu cha Amerika cha Lebanon huko Beirut, anaelezea kuwa tatizo kuu na athari za vita kwenye udongo linahusiana na mabomu ya angani au ya silaha zinazotumiwa, harakati za kijeshi na moto unaotokana na milipuko ya mabomu.

Anasisitiza kuwa matumizi ya silaha na moto yana athari halisi kwa ardhi, mazingira na wanyama kwa njia isiyo ya moja kwa moja.

Anatoa mfano wa hili: "Misitu pia ni nyumbani kwa mamalia wengi, wadudu, ndege, na viumbe wengine wengine. Ikiwa maeneo ya kijani yataharibiwa na mabomu au moto, viumbe wataangamia au watakimbilia mahalI mbali zaidi ambayo hayafai kwa maisha yao na watakufa kwa njaa baadaye."

Vipi kuhusu mabomu ya phosforasi?

Mabomu ya fosforasi kawaida husababisha kuwaka kwa moto mkubwa.

Shirika la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch lilisema mwezi Juni mwaka jana kwamba limethibitisha matumizi makubwa ya fosforasi nyeupe yaliyotumiwa na Israel kusini mwa Lebanon, katika miji 17 tangu Oktoba 2023.

Jeshi la Israel linasema mabomu yake ya fosforas "yamepangwa kwa ajili ya kutoa moshi sio kwa ajili ya mashambulizi au kwa madhumuni ya kuvamia."

Je, fosforasi nyeupe ni nini na hutumiwa vipi katika vita?

Mtaalamu Dag Weir anaelezea kwamba silaha nyingi "zina kiwango fulani cha sumu, na hii ni pamoja na vilipuzi na cheche za vyuma vizito ."

Hatahivyo, "kwa sasa, hatuna data ya kutosha juu ya uchafuzi wa moja kwa moja wa mazingira kwa silaha za kawaida na hatari zinazoweza kutokea kwa watu au mazingira," anaelezea.

g

Chanzo cha picha, PA-EFE/REX/Shutterstock

Maelezo ya picha, Israel ilishambulia kwa bomu mji wa Merkebah kusini mwa Lebanon

Mashambulizi ya Israel katika mji wa Markaba kusini mwa Lebanon Mhandisi Nadim Farajallah anasema kuwa mabomu ya fosforasi ambayo imepigwa marufuku kimataifa kama silaha ya moja kwa moja dhidi ya raia yanaendelea kuwaka kwa muda mrefu yanapokutana na hewa ya oksijeni, hata kama yanawasiliana nayo baada ya muda mrefu, hadi kiwango chote cha phosphorous kuungua.

Aliongeza: "Baadhi ya aina ya ndege kama vile kuku, hula changarawe ambayo huwasaidia kuyeyusha, ambayo wakati mwingine huwafanya kula chembe za mabomu ya fosforasi, na kuwaua wakati mabaki ya bomu yanaungua ndani yake."

Baadhi ya aina za mabomu yaliyotumika pia huathiri mazingira ya asili na watu kwa njia zisizotarajiwa.

Mabomu yasiyolipuka pia yamewaua wachungaji wengi na kondoo wao kwa miaka kadhaa baada ya vita kumalizika. Baadhi ya wachungaji wanaweza kulazimishwa kuhamia maeneo mengine kwasababu ya misitu iliyojaa mabomu ambayo hayajalipuka.

Uchafuzi wa maji na unawauwa samaki

Uchafuzi wa udongo ni mwanzo wa mlolongo wa uchafuzi wa baadaye.

Faraj Allah anasema kuwa kutokana na mabomu, moto na upotevu wa mimea hufunika, "mchanga unaosombwa kwa nguvu na kumwagwa kwenye mifereji na mito, na kusababisha kupungua kwa viwango vya maji ardhini."

Udongo uliosombwa kwenye mito "huathiri maisha ya samaki, vyura na mimea ya majini kutokana na mabadiliko ya joto la maji na mkusanyiko wa safu ya mchanga juu ya uso wake, kwahivyo samaki hula vifaa ambavyo havipaswi kula kwa sababu ya ukosefu wa kuonekana."

Farajallah anaendelea kusema kuwa mabadiliko ya joto la maji "huathiri mchakato wa uzazi wa wanyama wa majini, kwani joto la maji huamua jinsia ya samaki na vyura wanapozaliwa.

Kama joto la maji litabadilika, wote wanaweza kuzaliwa kiume au, ambayo itasababisha kupungua kwa idadi yao kwa muda na inaweza hata kusababisha kutoweka kwao."

Utaratibu huo huo unarudiwa baharini baada ya udongo kufikiwa na maji ya mto, "ambao pia huathiri samaki, kaa, na kila kitu kinachoishi kwenye miamba na kusoma mchanga wa pwani, na hivyo kuathiri mazingira ya baharini."

Mtafiti wa mazingira anathibitisha: "Mazingira hutegemea usawa, na usawa wowote katika sekta au mfumo wa kiikolojia husababisha usawa katika mifumo mingine."

g

Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock

Vipi kuhusu afya ya moyo?

Wanaikolojia wengi huwachukulia wanadamu kuwa sehemu muhimu ya mazingira na kwahivyo haiwezi kutenganishwa na vitu vingine vinavyounda mazingira asilia.

Tunaweza kuelewa kutokana na tafsiri hii kwamba usawa wowote katika mazingira ya viumbe vingine hai bila shaka utasababisha usawa katika maisha ya binadamu.

Farajallah anasema kuwa uchafuzi wa hewa unaofanyika katika vita unatokana na uchafuzi na uzalishaji kutoka kwa milipuko, ambayo hutoa "chembe chembe zisizoweza kuvutwa" ambazo tunaona kama vumbi.

Aliongeza kuwa chembe hizi, mbili hatari zaidi ambazo ni PM 2.5 na PM 10, zinabaki hewani kwa muda mrefu na kuunda utando wa hewa unaodumu kwa siku kadhaa kabla ya kukaa kwenye nyuso.

Utafiti uliofanywa na Shirika la ulinzi wa mazingira la Marekani umegundua kuwa yatokanayo na kuongezeka kwa viwango vya PM2.5 kwa masaa machache tu kunaweza kusababisha mshituko wa moyo na kifo. Ufichuaji wa muda mrefu huongeza hatari ya kifo kinachotokana na moyo na mishipa na hupunguza umri wa kuishi.

Kulingana na Chama cha moyo cha udhibiti wa magonjwa ya moyo cha Marekani, "uchafuzi wa hewa pia unaweza kuchangia shinikizo la damu na ugonjwa wa kisukari."

h

Chanzo cha picha, REX/Shutterstock

Maelezo ya picha, Uvamizi wa Israel katika kitongoji cha kusini mwa Beirut

Farajallah pia anasema kuwa athari isiyotarajiwa ya uharibifu wa mazingira unaosababishwa na vita ni kunyauka kwa mimea na miti ambayo wanakijiji kawaida hutegemea, angalau kwa sehemu, kama rasilimali ya ziada.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi