Mambo 7 yanayoonesha kwa nini tetemeko la ardhi Uturuki na Syria ni baya zaidi katika miongo ya hivi karibuni

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tetemeko la ardhi

Huku maelfu ya watu wakipoteza maisha yao na kujeruhiwa na majengo na miundombinu kadhaa kuharibiwa, tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.8 lililokumba Uturuki na Syria mapema Jumatatu lilikuwa mojawapo ya maafa makubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Mchanganyiko wa mambo ulisababisha maafa hayo.

Mchanganyiko wa ukubwa wa tetemeko la ardhi, kina chake, eneo lake la kijiografia, aina ya hitilafu iliyolisababisha, urefu wake au nguvu ya mitetemeko ya baadaye, yote hayo yalisababisha msiba huo.

Hapa tunakuambia ni mambo gani yaliyozidisha uwezo wa uharibifu wa tetemeko hilo la ardhi.

1. Ukubwa wa 7.8

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Tetemeko la kwanza, lililosajiliwa mapema Jumatatu karibu na Gaziantep (Uturuki), wakati watu walikuwa wamelala, lilikuwa na ukubwa wa 7.8, ambapo linachukuliwa kuwa "kubwa" .

Ukubwa huo unakadiria "nguvu ambayo hutolewa katika tetemeko la ardhi" na, duniani kote, "kwa kawaida kuna takriban matetemeko mawili ya ukubwa sawa kwa mwaka, ingawa mengi hutokea chini ya bahari au katika maeneo yasiyo na watu," anaelezea Stephen Hicks, mtaalamu wa matetemeko katika Chuo Kikuu cha London (UCL).

Kiwango kikubwa zaidi kilichorekodiwa tangu matetemeko ya ardhi kupimwa ni yale yaliyotokea Chile mnamo 1960, ambayo yalifikia 9.5.

Kama mwanajiofizikia wa Chile Cristian Farías anavyoonyesha, "ukubwa ni kana kwamba unaenda kwenye tamasha na bendi inacheza kwa sauti isiyobadilika."

lakini, kulingana na mahali ulipo kwenye chumba, "utakuwa na uzoefu tofauti wa tamasha. Kitu kimoja kinatokea kwa nguvu. Ikiwa uko katika maeneo tofauti kuhusiana na ambapo tetemeko la ardhi lilitokea, utaenda kuhisi athari tofauti," anaongeza Profesa katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Temuco.

Hapa ndipo kipengele kipya kinapojitokeza: nguvu yake.

2. IX degree

Athari za tetemeko la ardhi kwenye uso wa dunia ndio tunaita intensity, ambayo hupimwa kwa kile kinachojulikana kama "kipimo cha tetemeko la ardhi cha Mercalli".

Kiwango hiki "hukadiria ukubwa wa tetemeko la ardhi kulingana na vitu kama vile ardhi iliosonga, kwa kasi gani ilisogea, ikiwa kuna majengo yaliyoanguka au la... kiwango cha uharibifu," anaelezea Farías.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika tukio la la kwanza siku ya Jumatatu, maeneo kadhaa nchini Uturuki, karibu na miji ya Osmaniye, Kahramanmaras, Adiyaman au Malatya, yalisajili nguvu ya IX, ambayo inachukuliwa kuwa "ya uharibifu mkubwa" na ina maana, kwa mfano, uharibifu mkubwa wa majengo ikiwemo kuanguka , kama ilivyoonekana.

3. Tetemeko lenye nguvu lililofuata

Ingawa matetemeko ya ardhi kwa kawaida hufuatwa na mitetemeko midogo ya baadaye, tetemeko la ardhi la pili lililosikika siku ya Jumatatu lilikuwa na ukubwa sawa na wa 7.5.

Hili ni jambo ambalo hutokea tu katika 10% ya matukio, anaelezea Stephen Hicks, ambaye anakumbuka kwamba haiwezekani kujua ni lini au wapi tetemeko la ardhi lifuatalo litatokea.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa hakika, tetemeko la pili la Jumatatu lilitokea kwenye tawi tofauti la Anatolia la Mashariki, ambalo linaanzia kusini-magharibi hadi kaskazini mashariki.

"Hii inaangazia ugumu wa kujaribu kufanya utabiri, kwa sababu unaweza kuwa haujajua dosari hiyo hadi kitu kikatokea nayo," anasema profesa wa UCL.

Hali tete ambayo majengo mengi yalikuwa yameachwa ilichangia kubomoka kwake baada ya kupigwa na tetemeko lililofuata, hatua ilioongeza na janga.

4. Kina cha kilomita 18

Tetemeko la ardhi, wanasayansi wanakubali, lilikuwa la juu juu sana kwani lilitokea kilomita 18 tu kwenye kina cha dunia.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kilichotokea hapo ni kwamba "mitetemo iliyotoka kwa tetemeko hilo haikupoteza nguvu ya kutosha kabla ya kufika juu ya uso wa dunia, na ambayo ilisababisha mtikisiko mkubwa katika eneo ambalo majengo mengi, haswa ya jadi ya Mashariki ya Kati, hayakuwa tayari kustahimili." Hicks anasema.

5. Mwanya wa kilomita 150

Ukubwa wa mwanya wenye urefu wa kilomita 150 na unene wa kilomita 25 ni sababu nyingine iliyochangia uharibifu huo.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

"Mtu anaweza kufikiria kuwa kadiri mwanya wa tetemeko unapotokea ndivyo upana wake unavyokuwa lakini katika tukio hili kulikuwa na mwanya mmoja mrefu na mwembamba, suala linalomaanisha kwamba nguvu yote ilikuwa imejilimbikiza katika sehemu za juu juu, na hivyo kuwa vigumu sana kwa ujenzi wowote kustahimili ", anaeleza Cristian Farías.

6.Mwanya uliosababishwa na tetemeko pia ulisababisha madhara

Aina ya mwanya iliyotokana na tetemeko la ardhi nchini Uturuki na Syria, pia ilichangia kuongezeka kwa uharibifu.

Ili kuwa na uharibifu mkubwa , Farías anaonyesha, "si lazima uhitaji tetemeko la ardhi lenye ukubwa mkubwa sana."

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hakika tetemeko la Jumatatu, lenye ukubwa wa 7.8, si kubwa sana ukilinganisha na matetemeko mengine makubwa ya ardhi yaliyowahi kutokea duniani, kama lile la Japan mwaka 2011, lenye ukubwa wa 9; lile la Alaska a 1964, la 9.2; au lile la Chile mwaka 1960, la 9.5.

"Kwa kuwa kipimo kinachopima ni cha logarithmic, ni matetemeko makubwa zaidi ya ardhi, lakini mara nyingi huwa hayana nguvu katika baadhi ya maeneo ambayo yalifanyika ikilinganishwa na tetemeko la Uturu na Syria," anaongeza mtaalamu huyo wa Chile.

Jinsi tetemeko hili lilivyotokea, na mianya iliotokea kwa muda mfupi, iliongeza uharibifu zaidi.

Ili kuelezea aina hii ya mianya, Hicks anapendekeza kufikiria karatasi ambayo imechanika: "ni harakati ya usawa, kama vile unavyofanya wakati wa kurarua karatasi. Fikiria ukiichana karatasi hiyo kilomita 400, matokeo yake ni kwamba hutoa mitetemo inayosikika mbali sana. . kutoka kwa kitovu kwa njia kali sana".

Maelezo kuhusu tetemeko la ardhi lililosababishwa na hitilafu ya moja kwa moja.

Tatizo lililopo ambapo mtaalam wa jiografia anasema, "sio tu kwamba tetemeko la ardhi huanza juu juu, lakini harakati nzima ni ya juu juu, inafikia karibu hata chini. Na, basi, ikiwa mtu anaishi karibu, kama ilivyotokea Uturuki, uharibifu unaotokea juu ya ardhi unakuwa mkubwa sana. Athari unayohisi ni kana kwamba umepokea nguvu zote za mawimbi, kwa mpigo kana kwamba upo katika safu ya mbele kwenye tamasha la vyuma vizito."

7. Aina ya majengo

Na hapa, wataalam wanakubaliana, inakuja sehemu ya pili ya uharibifu: uwezo wa majengo kustahimili matetemeko ya ardhi.

Ingawa katika nchi kama Japan au Chile kanuni za ujenzi ni kali sana kutokana na matukio mingi ya matetemeko ya ardhi yenye nguvu, inawezekana kwamba nchini Uturuki na Syria majengo mengi hayakufuata kanuni hizo.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

"Katika picha ambazo tumezipata kutoka kwa tetemeko hilo la ardhi, unaweza kuona majengo ambayo yameporomoja kabisa huku majengo yalio karibu nayo yakionekana yamesimama. Hii hutokea kwa sababu, kwa hakika, yale yaliyosimama yalijengwa kwa kuzingatia kanani, kutafakari matukio yote, ", anaongezea Farías.

Kuna changamoto ya mara kwa mara katika nchi ambazo zina matetemeko makubwa ya ardhi kuelewa hali hizi na kujiandaa kwa ajili yao "kwa sababu tunagharamika kimaisha."

"Majanga si ya asili," anamalizia Farías, "yanategemea jinsi mtu anavyojitayarisha kwa tishio."