Kwa nini wanachama wapya wa NATO wanashiriki mazoezi makubwa karibu na mpaka na Urusi?

Mazoezi ya kijeshi

NATO ilifanya kila linalowezekana kuzuia kutaja Urusi kama adui wakati wa mazoezi. Na sio kwa sababu iliogopa uchochezi. Hatahivyo, uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine ulibadilisha kila kitu.

Haya ni mazoezi makubwa zaidi tangu kumalizika kwa Vita Baridi, na wanajeshi elfu 90 walishiriki.

Resilient Defender 2024 pia ni jaribio la kwanza la mipango mipya ya kijeshi ya NATO ya kusonga kwa kasi na kwa kiasi kikubwa askari na silaha ili kuimarisha mshirika yeyote anayeweza kushambuliwa.

Na huu ni uthibitisho wa lengo kuu la kuwepo kwa NATO: shambulio la mwanachama mmoja wa muungano litasababisha majibu kutoka kwa wote.

Donald Trump anaweza kuhoji hili, lakini nguzo kuu ya kanuni hii inabaki kuwa Marekani. Washington inatumia rasilimali nyingi kuthibitisha hili.

Hatua ya kwanza ya zoezi hilo inafanyika katika jangwa la Finnmark, eneo la kaskazini mwa Norway, karibu na mpaka wa Norway na Urusi wenye urefu wa kilomita 180. Hatahivyo, kulingana na hali ya mazoezi, adui wa hadithi Occasus anavamia Finnmark.

Kulingana na Eivor, mwanafunzi wa matibabu mwenye umri wa miaka 21 aliyegeuka kuwa mwanajeshi, babu na nyanya yake walilazimika kukimbia Finnmark wakati Wanazi walipovamia wakati wa Vita vya pili vya Dunia.

Eivor mwenye umri wa miaka 21 anashiriki katika mazoezi ya kijeshi kama sehemu ya Jeshi la Ulinzi la Wilaya

"Lakini afadhali nibaki na kupigana," Eivor anasema. Yeye hatarajii mashambulizi ya Kirusi, lakini "bila shaka, daima unapaswa kuwa macho."

Hili ni zoezi la kwanza kuu la NATO ambapo Uswidi na Ufini zinashiriki kama wanachama kamili tangu zijiunge na muungano huo.

Wanajeshi wa nchi hizo mbili wanafuraha wazi kuwa sasa ni sehemu ya kambi kubwa zaidi ya kijeshi duniani na wako tayari zaidi kubainisha ni wapi tishio hilo linatoka.

Mwanamaji mmoja wa Kifini anayejiandaa kutetea ufuo wa fjord alisema haikuwa na mantiki kwa nchi yake "kusimama dhidi ya Urusi peke yake," huku mwingine akiongeza: "Aina ya NATO inatisha Urusi."

Mwenzao, mwanamaji wa Uswidi, alikiri kwamba alihisi "salama kabisa" baada ya nchi yake kujiunga na NATO.

Boti

Mtazamo huu unashirikiwa na wanasiasa wa nchi hizo mbili.

Mawaziri wa ulinzi wa Uswidi, Finland na Norway walisherehekea muungano wao mpya wa Nordic kwa kutazama wanajeshi wakivuka mpaka kutoka Finland hadi Norway katika zoezi la kumfukuza adui wa uwongo.

Antti Kaikkonen, Björn Arild Gram na Paul Jonson walitabasamu kwa furaha walipokuwa wakipiga picha mbele ya zoezi la kurusha roketi.

Mawaziri wa ulinzi wa Finland, Norway na Sweden walipigwa picha mbele ya chombo cha kurusha kombora.

Waziri wa Ulinzi wa Uswidi Paul Johnson hakuogopa kumwaga chumvi kwenye majeraha ya Urusi, ambayo, hata hivyo, ilijiletea yenyewe. Aliita kuingia kwa Uswidi na Ufini katika NATO "matokeo muhimu zaidi ya yote yasiyotarajiwa" kwa Moscow.

Urusi, alisema, ilijaribu sana kuzuia nchi hizo mbili ambazo hazikuwa na uhusiano wowote hapo awali kujiunga na muungano huo, lakini ilishindwa.

Hatahivyo, kwa kweli, kuingia kwa Ufini katika muungano kumefanya NATO karibu zaidi na Urusi: urefu wa mpaka wa Urusi-Ufini ni kama kilomita 1,200 , na sasa washirika wanahitaji kuwa tayari kuilinda.

Tishio ni la kweli kiasi gani?

Hakuna anayebisha kuwa Urusi inatishia mara moja NATO. Na si haba kwa sababu wanajeshi wake wamezama nchini Ukraine. Hatahivyo, kuna maoni kwamba kwa muda mrefu, lengo la Urusi linaweza kuwa moja ya nchi mwanachama.

Mmoja wa maafisa wakuu wa kijeshi wa Uswidi hana shaka kwamba matarajio ya Moscow yanaenea zaidi ya Ukraine.

Takribani wanajeshi elfu 90 wanashiriki katika mazoezi hayo yanayofanyika kwenye mpaka wote wa mashariki mwa Ulaya.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wafanyakazi wa Pamoja wa Kikosi cha Wanajeshi wa Uswidi, Luteni Jenerali Karl-Johan Edström, ni suala la muda tu.

"Ndio, nina hakika kwamba Urusi ni tishio na tunahitaji kuwa na nguvu zaidi katika miaka 5 mpaka 10 ijayo," jenerali huyo alisema. NATO, inapaswa kutumia fursa hii kuunda vikosi vyake vya jeshi.

Viongozi wengine kadhaa wakuu wa kijeshi wa Ulaya na wanasiasa pia wanaonya kwamba Urusi inaweza kushambulia mwanachama wa NATO ndani ya muongo ujao.

Kama Naibu Admirali Doug Perry, mmoja wa maafisa wakuu wa jeshi la Marekani anayeongoza zoezi hilo, anasema, ni wazi kwake kwamba "bara la Ulaya tayari liko vitani."

Kwa sasa, kila kitu kiko Ukraine tu, lakini NATO, alisema, "lazima itathmini tabia ya Urusi na uwezo wake, kupata picha kubwa na kuwa tayari."

Anachukulia kujiunga hivi karibuni kwa Uswidi na Ufini katika NATO kama ushahidi wa ukweli wa tishio hili.

Nchi za Skandinavia, kama nchi za Baltiki, ni wazi huhisi hatari hiyo zaidi. Hii ni moja ya matokeo ya ukaribu wetu na Urusi.

Wanaongeza matumizi ya ulinzi kwa kasi zaidi kuliko wengine, na wakiwa wamepitia uchungu wa uvamizi hapo awali, wanajua vizuri zaidi kuliko mtu yeyote gharama halisi ya vita ni nini.

Muuguzi Elisabeth mwenye umri wa miaka 20 anahudumu katika Kikosi cha Ulinzi cha Eneo la Norway

Si kila mtu katika NATO amejiandaa vyema. Katika nchi nyingine za Ulaya, ikiwa ni pamoja na Uingereza, uandikishaji wa kijeshi haufanyi vizuri.

Miongoni mwa wanajeshi wa wataalamu wanaoshiriki katika mazoezi hayo pia ni washiriki wa Kikosi cha Ulinzi cha Norway, ambao ni, askari wa muda.

Wakati wa mazoezi haya, wanachukua nafasi ya askari wa adui, wakitembea haraka kwenye magari ya theluji kwenye tambarare zenye theluji na kulala usiku kwenye maeneo ya wazi kwenye baridi. Wengi wao ni vijana.

"Tuna watu wengi walio na uzoefu wa kijeshi, kwa hivyo inafanya kuwa salama zaidi kwa sababu tuko kila mahali," anasema mwalimu wa shule ya chekechea Josephine, 21.

"Ni muhimu kwa hisia zetu za usalama kwamba kuna watu ambao wanataka kutetea Norway," anasisitiza muuguzi mwenye umri wa miaka 20 Elisabeth.

Unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Lizzy Masinga