Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 16.12.2022

Chanzo cha picha, Getty Images
Shirika linalomwakilisha kiungo wa Fiorentina Sofyan Amrabat, 26, linamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Morocco kujiunga na Liverpool. (Football)
Chelsea wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Ivory Coast David Datro Fofana, 19, kutoka klabu ya Molde ya Norway kwa zaidi ya euro 10m. (Fabrizio Romano, Twitter)
Arsenal ni miongoni mwa vilabu kadhaa vinavyofanya mazungumzo kuhusu mpango wa kumnunua winga wa Ukraine Mykhaylo Mudryk lakini Shakhtar Donetsk wanasisitiza kuwa rais wao ndiye atakayeamua mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 - mara watakapopokea ofa yoyote rasmi. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool italazimika kulipa euro 150m (£130m) kwa kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham, 19, na karibu euro 100m (£87m) kwa kiungo wa kati wa Benfica na Argentina Enzo Fernandez, 21. (Mundo Deportivo – In Spanish).
Wakati huo huo, mipango ya baadaye ya Manchester City ya uhamisho inahusisha kujaribu kumsajili winga wa Bellingham na Arsenal na Uingereza Bukayo Saka, 21. (90min).
Mshambulizi wa Atletico Madrid na Ureno Joao Felix, 23, ambaye amepewa ofa ya kujiunga na vilabu vya Premier League vikiwemo Arsenal na Manchester United, anataka kuchezea Paris St-Germain. (Gianluca di Marzio Via Soccernews)

Mshambulizi wa Ujerumani Youssoufa Moukoko, 18, anakaribia kusaini kandarasi mpya na Borussia Dortmund licha ya Chelsea, Manchester United na Liverpool kumtaka. (Ruhr Nachrichten Via Metro)
Manchester United na Newcastle wanachuana na Real Madrid kuwania saini ya winga wa PSV Eindhoven na Uholanzi Cody Gakpo, 23. (Mirror)
Wolves italazimika kupambana na wapinzani wengi wa Premier League kuwania saini ya Atletico Madrid na mshambuliaji wa Brazil Matheus Cunha, 23. (90min).

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea watalazimika "kusukuma tena" kujaribu kumsajili fowadi wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, 23, huku meneja Graham Potter akitafuta kuchukua nafasi ya mshambuliaji wa Albania Armando Broja, 21. (Givemesport).
Everton wanasalia katika nafasi nzuri ya kumsajili fowadi wa Ajax Mohammed Kudus baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kucheza vyema katika michuano ya Kombe la Dunia akiwa na Ghana. (Sky Sports Via Liverpool Echo)
West Ham wanasonga mbele kwa lengo la mabeki wengine wa kulia baada ya kubainika kuwa hawana nafasi ya kuwashawishi Middlesbrough kumuuza beki wa pembeni wa Uingereza Isaiah Jones, 23. (Football League World)

Chanzo cha picha, Getty Images
Sevilla wameripotiwa kuweka bei ya pauni milioni 26 kwa mlinda mlango Yassine Bounou mwenye umri wa miaka 31 kufuatia uchezaji wake kwenye Kombe la Dunia kwa Morocco waliofuzu nusu fainali. (Estadio Deportivo – In Spanish )
Beki wa kati wa Napoli na Korea Kusini Kim Min-jae, 26, ambaye analengwa na Manchester United na Tottenham, anasema "amesikitishwa" na uwezekano wa kuhusishwa na Premier League. (Mail)
Kufuatia Uefa na Fifa kupata uungwaji mkono mkubwa katika vita vyao vya kuzuia kuundwa kwa Ligi Kuu ya Ulaya, imani miongoni mwa wawekezaji watarajiwa wa Liverpool imeongezeka na bei ya klabu hiyo pia imepanda. (Football Insider)












