'Nilikua mama nikiwa na miaka 46 bila ndoa na mtoto wangu hana baba'

Chanzo cha picha, COURTESY OF M. BARRAU
Uso wake unang'aa kwa furaha anapozungumza kuhusu kuwa mama.
Akiongea na BBC kuhusu mwanawe, Maria Barau alisema, "Nina furaha sana kwamba ninazunguka kuambia kila mtu kuhusu furaha ninayopata kutoka kwa mwanangu."
Mwanamke huyu, mwenye asili ya Extramadura, ambaye ameishi Seville kwa miaka saba iliyopita, anaelezea furaha yake ya kuwa mama akiwa na umri wa miaka 46.
Kulingana na takwimu za 'Taasisi ya Kitaifa ya Takwimu', wanawake 1,652 walio na umri wa zaidi ya miaka 45 wamekuwa mama mnamo 2021 nchini Uhispania, na Maria ni mmoja wa wanawake hao.
Sifa zikilimbikiziwa mbinu za kisasa za kusaidia uzazi katika kugandisha na kutoa mbegu za kiume, wanawake zaidi na zaidi wanakuwa akina mama katika umri mkubwa.
Siku hizi nchi nyingi zimehalalisha njia mbadala za kusaidia watu kupata watoto.

Chanzo cha picha, COURTESY OF M. BARRAU
Maria, alikuwa kabisa kutoka ndani ya moyo wake ametamani kuwa mama. Ingawa alifikiri ni lazima angekuwa na mwanaume upande wake ili ndoto yake hiyo ifanikiwe lakini haikuwa hivyo.
Kwa hiyo baada ya kuhangaika kwa miaka mingi hatimaye aliamua akiwa na umri wa miaka 45 kuchukua hatua.
Na sasa anashuhudia faida zote za kuwa mama.
“Ndiyo, kuwa mama katika umri mkubwa kumeniletea faida kwa sababu nimeishi sehemu kubwa ya maisha yangu na kuwa na uelewa tofauti wa maisha katika hatua hii kuliko tunavyokuwa katika miaka ya 20 au 30,” anasema Maria ambaye anatimiza miaka 48 mnamo mwezi Septemba. Ninaangalia maisha kwa mtazamo tofauti. Sina wasiwasi ikiwa mtoto ataanguka au hatakula. Umri unatupa mtazamo mpya."
Kufanya uamuzi
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
‘’Siku zote nilitaka kuwa na familia. Nilitaka kuwa baba pamoja na mama, lakini sikufanikiwa.
Miaka 10 hivi kabla ya kupata mimba ndio niligundua kuwa naweza kupata ujauzito bila kuolewa iwapo ningetaka mtoto.
Siku zote nilitaka kuwa na mwanaume katika maisha yangu pia.
Nilipofikisha umri wa miaka 45, nilikutana na mtu ambaye sasa ni rafiki yangu mkubwa na alikuwa jirani yangu wakati wa janga la covid.
Yeye alikuwa na binti yake mmoja. Nadhani kumuona kuliimarisha azimio langu.
Nilikuwa na wasiwasi si kwa sababu ya umri, lakini kama ningeweza kumzaa mtoto wangu.’’
Alikuwa na wasiwasi sio tu juu ya kuzaa mtoto, lakini pia juu ya malezi yake, na mahitaji yake.
‘’Hali hiyo ilionekana kunitisha.
Hofu pekee katika akili yangu, ilikuwa ikiwa ningeweza kumlea mtoto peke yangu.
Nilifikiri sikuwa na uwezo huo.
Nilikutana na mwanamke jirani yangu na kujifunza kutoka kwake jinsi ya kulea watoto.
Wakati huo nilikuwa na mashaka juu ya umri wangu.
Siku moja tulipokuwa tukizungumza, alisema, "Sasa una umri wa miaka 45. Unapaswa kufikiria kama unataka watoto au la. Unasema hutaki watoto, lakini hiyo si kweli.."
Kisha akaniambia, "Fikiria juu ya hilo. Jipe muda wa kufikiria, kisha ufanye maamuzi." Kwa hivyo nilijipa nikifikiria hili wakati wa Krismasi 2020 na mwishowe niliamua kuzaa mtoto.
Njia niliyotumia kupata ujauzito

Chanzo cha picha, COURTESY OF M. BARRAU
Baada ya kufanya uamuzi huo, ikawa wazi kuwa hakuna kitu cha hakika, lakini ningechagua chaguo salama zaidi.
Wakati ulipofika, daktari wa magonjwa ya wanawake aliniomba niingizwe mbegu za kiume, lakini nilikataa.
Matibabu ya kutungisha mimba ilikuwa chaguo salama zaidi na nilitaka kujaribu chaguo hilo.
Nilikuwa na bahati ya kupata mimba mara ya kwanza.
Nilipokea manii na mayai kupitia kwa mwanamume tusiyejuana. Kama nilivyosema hapo awali nilichukua njia salama.
Daktari wa magonjwa ya wanawake aliniambia kuwa umri wangu wa kibaolojia ni mdogo kuliko umri wangu wa kimwili na kwamba vipimo vinaonyesha kuwa kifuko cha mayai kinaweza kuanguka lakini niliamua kujaribu mara mbili.
Nilikuwa nimeshuhudia watu wakipoteza miaka ya maisha yao. Na mimi sikutaka hilo linitokee.
Aliamini kwamba kulikuwa na majaribio mara mbili tu.
Na, Namshukuru Mungu kwa kuwa mara ya kwanza nilipopata mimba hakukuwa na matatizo yoyote.
Ilikuwa ni ujauzito mzuri, nikazaa vizuri na mtoto alikuwa na afya njema. Sikuwa na malalamiko.

Chanzo cha picha, COURTESY OF M. BARRAU
Wakati huo niliamua kwamba ningeendelea na mchakato wa kupata mtoto.
Ilikuwa dhahiri ningepata mimba. Sikutaka kufikiria kitu kingine chochote.
Nilifikiria tu jinsi mimba ingeenda vizuri na kujifungua salama.
Umri wangu ungeweza kusababisha tatizo, lakini wakati huo sikufikiria chochote kibaya kingeweza kunitokea.
Kulikuwa na uwezekano kwamba kitu kitaenda vibaya, lakini kwa nini nifikirie juu ya hilo? Ikiwa kuna tatizo ambalo litatokea tutasuluhisha.
Isitoshe, daktari wangu wa magonjwa ya wanawake alinitia moyo kila wakati.
Walinifahamisha kuhusu hatari inayoweza kutokea na hilo lilinipa utulivu mwingi wa akili.
Walikuwa wakiniambia nisiwe na wasiwasi. Alifuatilia afya yangu kila wakati.
Nilikuwa na tatizo kidogo la sukari kwenye damu, lakini alilidhibiti.
Mwisho wa ujauzito, alinitunza sana kwa kuzingatia umri wangu na kila kitu kikaenda sawa.
Katika wiki za mwisho za ujauzito, daktari aliniambia kuwa hakuna maji maji kwenye tumbo na mtoto haongezi uzito, lakini ana afya nzuri.
Bila shaka, hii inaweza kutokea kwa mtu yeyote. Haikuwa na uhusiano wowote na umri wangu. Ikiwa maji yataisha, mtoto lazima atoke.
Kipindi cha baada ya kujifungua kilikwenda vizuri, nilishonwa nyuzi tatu na siku hiyo hiyo nilishuka kutoka kitandani nikatembea.
Mtoto wangu alizaliwa tarehe 4 Desemba 2021. Niliruhusiwa kutoka hospitali mnamo Desemba 6.
Siku ya saba nilitembea dakika 45 hadi hospitali kuomba kuandikiwa ruhusa ya kupata likizo na nikarudi nyumbani.
Nilikuwa na afya njema. Sijui ikiwa ilitokana na maumbile au kujishughulisha na mambo mengi, lakini nilikuwa sawa. Pia sikupata uzito mwingi wakati wa ujauzito.
Mvumilivu na subira zaidi

Chanzo cha picha, COURTESY OF M. BARRAU
Nafkiri kama ningepata ujauzito miaka 10 iliyopita, nisingekuwa na tabia kama hii, kwa sababu nimebadilika sana.
Mimi ni mtu mwenye wasiwasi kweli. Nilijaribu kwa muda mrefu kutatua hilo.
Ikiwa ningepata mimba miaka 10 iliyopita, uzoefu ungekuwa tofauti sana, labda mbaya zaidi.
Nilikuwa na wasiwasi sana juu ya masuala mengi tu.
Mara kwa mara nilikula glucose ili kupata nguvu. Ndio maana nadhani nimeweza kuishi. Nilishinda kwa msaada wa mtaalamu.
Pia kusema kweli, ilinisaidia sana kuwa karibu na dini.
Sikuwahi kuhisi kwamba kuna mtu yeyote alifikiria vibaya kunihusu.
Wakati huo, watu wengi waliniambia kwamba ulikuwa wakati unaofaa, kwa sababu ndani ya nafsi yangu nilitaka kuwa mama.
Kuna wengi pengine ambao watakuwa wanazungumza juu yangu, lakini sijawahi kuhisi kwamba wananifikiria vibaya.












