Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 04.01.2023
Manchester United bado wanaweza kumuuza beki wa Uingereza Aaron Wan-Bissaka mwezi huu wa Januari, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kuonyesha mchezo mzuri hivi majuzi. (Athletic- usajili unahitajika - kupitia Mail)
Chelsea wanajipanga kufanya jaribio la mwisho kuteka nyara ombi la Arsenal la kununua winga wa Shakhtar Donetsk naUkraine Mykhailo Mudryk, licha ya The Gunners kuafikiana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Sun)
Chelsea wanasita kufikia euro 120m (£105.8m) katika mkataba wa kiungo wa kati wa Argentina Enzo Fernandez na Benfica, 21, ambao wanataka ada hiyo ilipwe kikamilifu ili kukubali kuhama. (Telegraph - usajili unahitajika)
Kiungo wa kati wa Uholanzi Memphis Depay amekuwa akihusishwa na kurejea Manchester United lakini mkufunzi wa Barcelona Xavi anataka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 abaki Nou Camp. (Metro)
Newcastle United wamemaliza harakati zao za kumnunua mshambuliaji wa Borussia Monchengladbach na Ufaransa Marcus Thuram, 25, huku mkufunzi wa Magpies Eddie Howe akitanguliza nyadhifa zingine. (Football Insider)
Bayern Munich, Newcastle, Paris St-Germain na Liverpool wanatazamiwa kuwania saini ya kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach Mfaransa Manu Kone, 21. (Fabrizio Romano)
Chelsea, Newcastle United na Bayern Munich wanavutiwa na kipa wa Leeds United Illan Meslier, lakini klabu hiyo ya Elland Road haitaki kumuuza Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 22. (RMC Sport - kwa Kifaransa)
Kocha wa Leicester City Brendan Rodgers bado anatumai kuwa klabu hiyo inaweza kufikia mkataba mpya na kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 25, ambaye mkataba wake unakamilika msimu wa joto. (Goal)
Brentford wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Kevin Schade kwa pauni milioni 22 kutoka Freiburg baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kufaulu vipimo vya afya. (Times - usajili unahitajika)
Mshambulizi wa Brentford mwenye umri wa miaka 21 kutoka Scotland Aaron Pressley amekubali mkataba wa kujiunga na Accrington Stanley kwa mkopo. (Football Insider)
Arsenal wako tayari kumuuza beki wa kulia wa Ureno Cedric Soares, lakini uhamisho wa kwenda Fulham unazuiliwa na matakwa ya mshahara ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31. (Evening Standard)
Middlesbrough wako kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa Muingereza Cameron Archer, 21, kwa mkopo kwa muda wote uliosalia. (TeamTalk)
Southampton wanakaribia kufikia makubaliano ya pauni milioni 7.5 kumnunua kiungo wa kati wa Dinamo Zagreb na Croatia Mislav Orsic, 30. (Sun).