Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mji ambao ni marufuku wanawake kukaa viti vya mbele kwenye magari makubwa
Mapema mwaka huu, katika jiji la Lira, Kaskazini mwa Uganda, sheria ndogo ilipitishwa ambayo ilipiga marufuku wanawake kukaa kwenye vyiti vya mbele vya malori. Muungano wa madereva wa lori unaamini kuwa abiria wa kike huwasumbua madereva na wanaweza kusababisha ajali za barabarani. Mwandishi wa BBC Grace Kuria alitembelea mji huo na kuandaa taarifa hii.