Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwanini vijana wa kiarabu wanageukia dawa za kuongeza nguvu za kiume?
Na Hossam Fazulla BBC Arabic
Katika duka lake la dawa katika kitongoji cha kihistoria cha Bab al-Shaaria katikati mwa Cairo, mtaalamu wa mitishamba Rabea al-Habashi anaonyesha kile anachokiita "michanganyiko yake ya kichawi".
Bw Habashi amejipatia umaarufu kwa kuuza dawa za kusisimua mwili na viboreshaji asili vya ngono katika mji mkuu wa Misri. Kwa miaka michache iliyopita, hata hivyo, ameshuhudia mabadiliko katika kile ambacho wateja wake wanataka zaidi.
"Wanaume wengi sasa wanakwenda kutafuta tembe za rangi ya samawati (blue pills) ambazo wanapata kutoka kwa makampuni ya Magharibi," anasema.
Kulingana na tafiti kadhaa, vijana wa kiume wa Kiarabu wamekuwa wakitumia zaidi dawa za za kisasa za kuongeza nguvu za kiume kama vile sildenafil (inayojulikana kibiashara kama Viagra), vardenafil (Levitra, Staxyn), na tadalafil (Cialis).
Licha ya ushahidi huo, pengine haishangazi vijana wengi ambao BBC ilizungumza nao katika mitaa ya Misri na Bahrain walikanusha kutumia dawa kwa matatizo ya uume au hata kuzifahamu. Wengine hata walikataa kuzungumzia suala hilo hapo mwanzo, kwani waliona kuwa ni "kinyume na maadili ya jamii".
Kwa kweli, kulingana na utafiti wa 2012 Misri ilikuwa ya pili kwa watumiaji wa dawa za kuongeza nguvu za kiume kwa kila mtu katika ulimwengu wa Kiarabu. Saudi Arabia iliongoza kwenye orodha hiyo.
Al-Riyadh, gazeti la Saudi lililochapisha ripoti hiyo, lilikadiria wakati huo Wasaudi walitumia $1.5bn (£1.23bn; €1.43bn kwa kiwango cha ubadilishaji cha leo) kila mwaka kwa tembe za kuongeza nguvu za kiume. Matumizi ya Saudi Arabia yalikuwa juu mara 10 zaidi ya Urusi, ambayo idadi ya watu wake wakati huo ilikuwa kubwa mara tano, ilisema.
Hivi majuzi, matokeo ya utafiti wa Jarida la Kiarabu la Urology yalionyesha kuwa 40% ya vijana washiriki wa kiume wa Saudi walikuwa wametumia dawa inayofanana na Viagra wakati fulani maishani mwao.
Misri bado inashika nafasi ya juu. Kulingana na takwimu za serikali kutoka 2021, mauzo ya dawa za kuongeza nguvu za kiume huko yanafikia takriban $127m kwa mwaka, ambayo ni sawa na 2.8% ya soko zima la dawa la Misri.
Shinikizo za kiume
Bila shaka, wengine wanataka kuonja matokeo ya kinachofanyika .
Mnamo mwaka wa 2014, dawa ya kuzuia upungufu wa nguvu nguvu za kiume iitwayo Al-Fankoush ilionekana katika maduka ya vyakula ya Misri kwa namna ya kipande cha chokoleti. Al-Fankoush iliuzwa kwa pauni moja ya Misri, ($0.05; £0.04; €0.04 kwa kiwango cha ubadilishaji cha leo). Muda mfupi baada ya kuingizwa sokoni, usambazaji wa Al-Fankoush ulisitishwa na mtengezaji wake kukamatwa na vyombo vya usalama baada ya vyombo vya habari vya ndani kuripoti kuwa ilikuwa imeuzwa kwa watoto.
Matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za kiume yanajulikana kuwa yameenea zaidi kati ya wazee kuliko wanaume wachanga. Nchini Yemen, hata hivyo, data kutoka kwa wizara ya afya inaonyesha hutumiwa zaidi na wanaume kati ya umri wa miaka 20 na 45.
Ripoti za ndani zinaonyesha matumizi ya Viagra na Cialis kama dawa za burudani imekuwa jambo la kawaida miongoni mwa vijana tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya vuguvugu la waasi la Houthi na serikali inayoungwa mkono na Saudi Arabia mnamo 2015.
Mohamed Sfaxi, profesa wa Tunisia wa magonjwa ya mfumo wa mkojo na upasuaji wa uzazi, alisisitiza katika mahojiano na BBC kwamba dawa hizo "sio vichocheo" na zilikuwepo kutibu hali ambazo mara nyingi "zinawatesa wazee".
Wakati huo huo, mtaalam wa masuala ya kujamiiana katika Mashariki ya Kati anapendekeza vijana wa kiume wa Kiarabu kugeukia tembe za kuzuia upungufu wa nguvu za kiume kwa sababu ya utamaduni uliopo.
"Sababu inaweza kumaanisha suala kubwa zaidi ambalo vijana wa Kiarabu wanakabiliana nalo," anaelezea Shereen El Feki, mwandishi wa habari wa Misri na Uingereza na mwandishi wa Sex and the Citadel: Intimate Life in a Changing Arab World.
Akijibu matokeo ya uchunguzi mkuu wa mwaka 2017 ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa kuhusu usawa wa kijinsia katika Mashariki ya Kati, Bi El Feki anaeleza: "Takriban washiriki wote wa kiume walikuwa na hofu ya siku zijazo na jinsi watakavyohudumia familia zao. Wanaume wengi walizungumza juu ya hali hiyo kubwa. shinikizo la kuwa mwanamume huku wanawake wakieleza "jinsi wanaume si wanaume tena".
"Kwa vile maana ya kuwa mwanaume ni chini ya shinikizo na nguvu za kijinsia zimeunganishwa katika utamaduni wa uume, kuna mkazo zaidi juu ya utendaji wa ngono," anasema.
Bi El Feki anahusisha mkazo wa utendakazi kwa kiasi fulani na imani potofu na matarajio yaliyokithiri yanayotokana na ponografia "ambayo hubadilisha mawazo ya vijana kuhusu kile kinachojumuisha 'kawaida' inapokuja suala la uanaume".
Maoni na dhana za kihistoria
Ingawa matumizi ya dawa kwa ajili ya mahitaji ya ngono yanaweza kuchukuliwa kuwa jambo la kisasa katika jamii za Waarabu, utumiaji wa dawa hizi umekuwa sehemu ya utamaduni maarufu katika historia ya Waarabu.
Ibn Qayyim al-Jawziyya, mwanazuoni na mwandishi muhimu wa Kiislamu wa Karne ya 14, alijumuisha katika mfululizo wa kitabu chake Masharti ya Akhera mkusanyiko wa mapishi ya mitishamba yenye lengo la kuongeza hamu ya ngono.
Shereen El Feki anapendekeza kwamba katika mila za Kiarabu na turathi za Kiislamu "wanawake wanaonekana kihistoria kuwa na nguvu zaidi na wana ari zaidi ya ngono kuliko wanaume", wakati wanaume wanahisi haja ya "kuboresha utendaji wao wa ngono ili kuendelea".
Wazo hili linaonyeshwa katika kipindi cha Milki ya Ottoman, wakati mwandishi Ahmed bin Suleiman alipoandika kitabu cha Kurudi kwa Ujana kwa Sheikh kwa ombi la Sultan Selim wa Kwanza, aliyetawala kuanzia 1512 hadi 1520 kuhusu magonjwa na kuchochea hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume na wanawake.
Mamia ya miaka baadaye vijana wengi wa Kiarabu bado wanageukia tiba, na soko la tiba hizo ni zuri.