Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, Uingereza itaifuata Marekani na kuruhusu matumizi ya makombora yake ya masafa marefu?
Sasa kwa vile Marekani imeipa Ukraine rukhsa ya makombora ya masafa marefu yanayotolewa na Marekani nchini Urusi, Uingereza itaamua nini?
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekuwa akishinikiza kupata kibali kutoka kwa Washington cha kutumia Mfumo wa Makombora wenye Nguvu ulioundwa na Marekani, unaojulikana kama ATACMS, kutekeleza mashambulizi ndani ya Urusi.
Maafisa wa ulinzi wa Uingereza kwa upande wao wamekuwa wakitafuta kibali cha Marekani kwa Kyiv kutumia makombora ya Storm Shadow yaliyotolewa na Uingereza kulenga shabaha za kijeshi ndani ya Urusi.
Lakini London haikuwa tayari kuchukua uamuzi huo peke yake na ilikuwa ikisubiri Ikulu ya White House kubadili mawazo yake, ambayo ilifanya Jumapili.
Mabadiliko ya sera ya Marekani yanafungua njia kwa Ukraine kutumia Storm Shadow na vikwazo vichache - jambo ambalo Ukraine imekuwa ikiomba kwa miezi kadhaa.
Makombora ya Storm Shadow, na yale yanayofanana na yale ya Ufaransa yanayoitwa SCALP, yametumwa kwa idadi ndogo - kwa mamia na sio maelfu - kwa Ukraine na hadi sasa yametumika tu dhidi ya malengo ndani ya ardhi yake.
Ukraine tayari imezitumia dhidi ya Crimea inayokaliwa na Urusi - kwa mfano kushambulia makao makuu ya jeshi la wanamaji katika eneo la Bahari ya shamu huko Sevastopol.
Makombora haya, ambayo hurushwa kutoka kwa ndege, huruka karibu na kasi ya sauti na hubeba makombora yanalipuka na kuifanya kuwa silaha bora ya kupenya mahandaki ya Kirusi na magala ya silaha.
Majadiliano ya muda mrefu kuhusu kurusha makombora ya Storm Shadow hadi ndani kabisa ya Urusi yaliibuliwa wakati wa mkutano wa kilele wa Nato wa Julai mjini Washington.
Starmer alisisitiza kuwa makombora hayo yangetumika kwa ajili ya kujihami lakini akasema "ni Ukraine kuamua jinsi ya kuyatumia".
Katika ujumbe kwenye X wakati huo Zelensky aliandika "amejifunza kuhusu ruhusa ya kutumia makombora ya Storm Shadow dhidi ya shabaha za kijeshi katika eneo la Urusi", akiongeza kuwa yeye na Starmer walikuwa na "fursa ya kujadili utekelezaji wa uamuzi huu".
Lakini hakuna kilichotokea baada ya mkutano huo.
Zelensky aliweka wazi matumizi ya makombora ya masafa marefu niasehemu muhimu ya "Mpango wa Ushindi" wake.
Aliibua suala hilo tena alipoenda Downing Street kumjulisha Starmer mwezi uliopita, katika mkutano uliohudhuriwa na katibu mkuu mpya wa Nato Mark Rutte.
Hakukuwa na mabadiliko katika sera, lakini Rutte alisema hakuna sababu ya kisheria ya kuzuia Ukraine kushambulia Urusi ikiwa nchi zilizosambaza makombora zitakubali.
Waziri wa Ulinzi wa Uingereza John Healey ametumia kila njia kuonyesha kutokubaliana kwa umma na Washington. Alipoulizwa hivi majuzi kuhusu suala hilo katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, Healey alisema majadiliano hayo hadharani yangeisaidia Urusi pekee.
Hofu ni kwamba ingawa vitisho vya Rais wa Urusi Vladimir Putin vimegeuka kuwa vya upuuzi kwa kiasi kikubwa, kuruhusu Ukraine kulenga shabaha ndani ya Urusi na makombora yanayotolewa na nchi za Magharibi kunaweza kusababisha ongezeko kubwa la vita
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alionya Putin ameeleza kuwa hatua kama hiyo itaiweka Nato "katika vita" na Urusi - kwani mashambulio kama hayo hatimaye yatatekelezwa sio na Ukraine bali na nchi zinazotoa kibali cha matumizi hayo ya makombora.
Profesa Justin Bronk kutoka taasisi ya ulinzi ya Taasisi ya Royal United Services aliiambia BBC News kwamba "kuna uwezekano mkubwa" kwamba uamuzi wa kuchelewa wa Rais wa Marekani Joe Biden wa kuruhusu mashambulio ya makombora ya masafa marefu ya ATACMS pia utawezesha Storm Shadow kutumika angalau katika eneo hilo.
"Vitisho vya Urusi haviwezi kuchukuliwa kuwa kizuizi kikubwa katika hatua hii, kwa kuwa Urusi imetishia kuchukua hatua kali - ikiwa ni pamoja na dokezo la mashambulizi ya nyuklia - mara kwa mara katika vita katika kila hatua wakati vifaa vya Magharibi vimetolewa kwa Ukraine."
Aliongeza "malengo mengi muhimu zaidi kama vile ndege za kivita za Urusi kwenye vituo vya anga vya Urusi haviwezi kufikiwa na makombora hayo - na kutakuwa na idadi ndogo ya makombora yanayopatikana baada ya matumizi ya muda mrefu ya mapigano kuanzia tangu vita vilipoanza hadi wakati huu."
Imetafsiriwa na kuchapishwa na Seif Abdalla