'Dini kwanza kabla ya soka', maisha ya wanasoka kwenye mfungo wa Ramadhani

Chanzo cha picha, Getty Images
- Author, Ian Williams
- Nafasi, BBC Sport Africa
- Muda wa kusoma: Dakika 5
''Kwangu mimi, nimeipa dini yangu kipaumbele. Na ya kwanza kabla soka.''
Mshambuliaji kutoka taifa la Burkina Faso ni muumini wa dini ya kiislamu ambaye hufanya maombi mara tano kwa siku, kabla na baada ya mechi anazozicheza, akisema humsaidia kuishi ''na unyenyekevu''.
''Hunifanya mimi kujitathmini na kurejea kwa mola wangu, ambayo hujipima nilichofanya vizuri na nilichokosea,'' mwanasoka huyo wa miaka 23 aiambia BBC alipokuwa akifanya ibada katika msikiti ulioko Poole.
"Pia inaturuhusu kujisahihisha katika jamii pia. Inaturuhusu kukaa kwenye njia sahihi."
Wakati wa mazungumzo, Ouattara amependelea kutumia maneno kama ''utulivu'' na ''uthabiti'' kuelezea umuhimu wa dini ya kiislamu.
Mwanasoka huyo ambaye ana sifa bainifu, akionekana mwenye haya, ambaye hana matashtiti mengi.
Akiwa amefika mapema kwa mahojiano yetu naye, akiwa amevalia nguo nyeupe anatuomba tumpe muda afanye ibada kabla ya kikao chetu.
''Imani yangu uniruhusu kukabiliana na changamoto nyingi za maisha, kuheshimu watu, na pia kikubwa zaidi kuheshimu maamuzi na dini za wengine,'' anaelezea.
''Nikiwa uwanjani, nikitangamana na familia pamoja na marafiki, imani yangu hunifanya nikawa mtulivu katika maisha yangu ya kila siku.
''Unapaswa kuamini kabla ya kufanya jambo.''
'Jamii inakufanya ujihisi hauko mpweke'
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Msimu huu wa kandanda, Ouattara anaonekana mwenye kujiamini anachokifanya.
Licha ya kuwa hachezeshwi katika kikosi cha kwanza, ameshafunga mabao tisa katika mechi zake 30 alizocheza, ikiwemo mabao matatu (hat triki) dhidi ya klabu ya Nottingham Forest mwezi Januari.
Idadi ya mabao anayojivunia Ouattara imeongezeka ukilinganisha na msimu uliopita, ambao alifunga bao moja pekee.
Akiwa chini ya Andoni Iraola, Ouattara anasema timu hiyo ni '' ni raha'' kuichezea.
''Siri kubwa ya ufanisi wetu msimu huu ni kuwa tuna kikosi kile tulichokuwa nacho kwa muda mrefu, kuanzia wachezaji hadi Kocha.Ni muhimu kuwa na timu ambayo inaendelea kujifua Pamoja,'' anaongezea.
''Unaweza kuona jinsi wachezaji wanavyofurahia wakiwa uwanjani. Tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha tumefika mbali.''
Mwanasoka huyo ambaye amezaliwa katika kijiji cha Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso, safari yake inaweza kufuatilia alivyoingia pwani ya kusini ya Uingereza kupitia njia ya Ufaransa ya Lorient.
Akiwa amesajiliwa kwa dola milioni 26 alipoanza kandanda mwezi Januari mwaka 2023 na kuwa mzaliwa wa pili wa Burkina Faso kuchezea ligi ya Ulaya akifuata nyayo za nahodha wa timu yake ya kitaifa na aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Aston Villa anayefahamika kama Bertrand Traore.
Japokuwa anasitasita kuzungumza kiingereza kwa muda mrefu, anakiri kuwa changamoto za lugha zilikuwa kikwazo kikubwa alipofika nchini humo lakini dini ilimrahisishia utangamano wake.
Awali ilimpa shida kidogo, kwenye mawasiliano na hata pia namna ya kuishi kwa ibada kwa kuwa Misikiti sio mingi Uingereza kama ilivyo nchini kwake.
''Kwa usaidizi wa wakala wangu nilipata msikiti, kwahivyo nilianza kurejea shughuli zangu nilizokuwa nazo nikiwa nyumbani,'' anaelezea.
Na nilipoingia msikitini, kila kitu kilikuwa shwari haswa katika mishemishe zangu za michezo.
Kwahivyo nilikuwa katika mazingira sawa niliyoyaacha huko Lorient.
''Inasaidia haswa unapokuwa katika taifa geni, kuwa na jamii inakupa matumaini kuwa hauko pweke . Unapata fursa ya kufanya ibada na watu na pia kutangamana na watu wengine.Ina tusaidia kujikita zaidi katika dini''
Mkakati wa Ouattara kumudu mfungo

Mwaka huu, Mwezi mtukufu wa Ramadhan ulianza siku ya Ijumaa tarehe 28 mwezi Februari na unatarajiwa kukamilika Jumapili tarehe 30 mwezi Machi.
Mwezi huu unaaminika na waumini wa dini ya kiislamu kuwa ni wakati kitabu kitukufu cha Quran kiliteremshiwa Mtume Mohammad (s.a.w)
Ili kufuata maagizo ya mwezi huu, kufunga kula na kunywa kuanzia machweo hadi mawio ni lazima.
''Ningependa kusema kuwa mfungo wa Ramadan sio mgumu, yote ni akili haswa mimi nimezoea kufunga wakati huu,'' anasema Ouattara.
''Changamoto kuu huenda ni kukosa kunywa maji. Na pia kuamka katikati ya usiku kufanya ibada na kutia tonge mdomoni ambalo hilo ndio naliona linachokesha.''
Lakini ana njia za kuhakikisha hana machofu: nayo ni Kujipumzisha .
''Huamka kila asubuhi saa 4:30, najisafisha na pia tayari huwa nimechukua chakula kutoka kwa mpishi wa timu yetu.
'' Nala, kisha nafanya ibada alafu narudi tena kulala kama saa moja kabla ya mazoezi.
''Baada ya mazoezi nafanya maombi kisha nalala tena kwa saa moja. Kwakuwa najipumzisha kila nikipata nafasi inakuwa rahisi kutoshindwa kumudu funga yangu.''
Uhusiano na wachezaji wenzake
Licha ya kuwa anafunga, na pia kujipumzisha, ratiba ya Ouattara bado haijabadilika.
''Huwa rahisi zaidi iwapo unapata usaidizi kutoka kwa timu nzima, kuanzia wachezaji hadi wafanyikazi.
''Kila mmoja huniuliza 'naendeleaje? Uko sawa? Sio ngumu kwako?
''Hunielewa na pia kunipa motisha kuendelea na wajibu wangu kama muislamu,.''
Ingawa yeye ndiye muislamu pekee katika kikosi cha Bournemouth, Ouattara sio mchezaji pekee ambaye hufunga wakati wa Ramadhan katika ligi kuu ya Uingereza.
Msimu huu wa saumu ulipatiwa heshima zake tangu mwaka 2021 wasimamizi wa ligi walipoanzisha mtindo ambao unaruhusu marefa kusitisha mechi kwa muda ili kuruhusu wachezaji waliofunga kufungua saumu yao.
Ni jambo ambalo Ouattara analishabikia.
''Mkakati huu wa ligi ya Uingereza unapaswa kupigiwa upatu kwani sio rahisi kucheza kandanda huku umefunga.
''Natumai mkakati huo utaendelea siku z ausoni.''
Dango Ouattara ni mtu ambaye ni msikivu na anafuata dini, jambo ambalo limemsaidia kaa mchezaji wa Bournemouth ambao mashabiki wanamuaminia.
Imetafsiriwa na Mariam Mjahid












