BBC Africa Eye: Ushelisheli , kisiwa kilichotekwa nyara na dawa za kulevya

BBC Africa Eye: Ushelisheli , kisiwa kilichotekwa nyara na dawa za kulevya

Kisiwa cha Ushelisheli kinajulikana kama paradiso ya kitropiki chenye mamilioni ya watalii. Lakini zaidi ya hoteli zenye viwango vya juu na fukwe za azure ni nchi iliyo katika machafuko.

Kulingana na idadi ya watu, Ushelisheli ina tatizo kubwa zaidi la matumizi ya dawa ya kulevya ya heroin duniani huku karibu 10% ya Washelisheli wanategemea dawa hiyo.

Fady Banane, ambaye ameishi visiwani maisha yake yote, alikuwa mmoja wao.

Baada ya kuishi bila kutumia heroin kwa muda, Fady anachunguza janga la siri hiyo ambalo limefichwa ndani ya starehe.

Alikutana na watumiaji wa dawa za kulevya, wauzaji, polisi na jamii ambazo zimejipata katika uraibu huo. Fady anakabiliana na maisha machungu ya zamani na anajaribu kuungana tena na wapendwa wake…na nusura angeangamia kwa dawa hiyo.