Kush: Dawa mpya haramu nchini Sierra Leone

Filamu hii ina matukio ya kutamausha, matumizi ya dawa za kulevya na vitendo vya kujidhuru na kujiua.

Kush - dawa mpya haramu ya bei nafuu, inaharibu jamii nchini Sierra Leone.

BBC imesikia taarifa za vijana kujiua au kujidhuru wao na wengine.

Matabibu katika mji mkuu Freetown wanasema kuwa 90% ya wanaume waliolazwa katika wodi kuu ya wagonjwa wa akili ni kutokana na matumizi ya Kush.

Polisi wanapambana kushinda vita dhidi ya dawa za kulevya.

Huku matumizi ya Kush yakienea kwa kasi, watumiaji ambao ni wachanga zaidi wakikabiliwa nayo, mwanahabari wa Africa Eye, Tyson Conteh, anachunguza dawa hiyo na kuhoji kama Sierra Leone inaweza kukomesha uraibu huo wa hatari.