Makundi ya watu kadhaa wateketea na moto kiwandani

Taarifa kutoka jimbo la Rivers kusini mwa Nigeria zinasema makumi ya watu wameuawa katika mlipuko uliotokea kwenye kiwanda cha kusafisha mafuta ambacho hakijasajiliwa kisheria.
Baadhi ya ripoti zinaonyesha kuwa idadi ya waliofariki inaweza kufikia 100 huku baadhi ya wakiwa wameteketea kiasi kisichoweza kutambulika.
Sababu halisi ya mlipuko haijajulikana bado.
Maafisa waliambia BBC kwamba idadi ya waliofariki inaweza kuwa kubwa zaidi huku uokoaji wa waathiriwa ukiendelea.
Mamlaka ya jimbo la Imo inasema mlipuko ulitokea wakati viwanda viwili vilivyo karibu vya kusafisha mafuta ambavyo viko kinyume na sheria, katika mji wa Egbema.
Mamia ya watu wanaofanya kazi katika kiwanda pamoja na wakazi wa maeneo ya jirani wameathirika na moto huo.
Shirika la habari la Reuters lilimnukuu kamishna wa mafuta katika jimbo hilo, Goodluck Opiah, akisema moto huo umeteketeza watu kwa namna ambayo haijafahamika bado.
Kiwango kikubwa cha umaskini na ukosefu wa ajira umefanya kiwanda hicho ambacho hakijasajiliwa kisheria kiliwavutia wakazi wengi kufanya kazi hapo.
Mamlaka imekuwa ikikabiliana na viwanda vya namna hiyo.
Tukio hilo linakuja huku serikali ya Nigeria ikisema inashinda vita dhidi ya baadhi ya vijana wa Niger Delta wanaovunja mabomba na kuiba mafuta, wakiyasafisha katika baadhi ya viwanda kinyume cha sheria.












