Malkia wa Uingereza akutwa na corona

Chanzo cha picha, Getty Images
Malkia Elizabeth wa Uingereza amepima virusi vya Covid na kukutwa na corona, kasri la Buckingham limesema.
Malkia anakabiliwa na "dalili kali kama baridi" lakini anatarajia kuendelea na "kazi nyepesi" huko Windsor katika wiki ijayo, kasri yake ilisema.
"Ataendelea kupata matibabu na atafuata miongozo yote inayofaa," iliongeza taarifa hiyo.
Malkia mwenye umri wa miaka 95, alikuwa akiwasiliana na mtoto wake mkubwa ambaye ndiye mrithi wake, Prince of Wales, ambaye alikutwa na virusi vya corona wiki iliyopita.
Inaeleweka kuwa watu kadhaa wamepima virusi katika Windsor Castle, ambako Malkia anakaa.
Tangazo hilo linakuja wiki kadhaa baada ya Malkia kuwa kiongozi aliyetawala kwa muda mrefu zaidi nchini Uingereza, na kusheherekea miaka 70 (Queen's Platinum Jubilee) mnamo Februari 6.
Alifanya shughuli yake kuu ya kwanza ya umma kwa zaidi ya miezi mitatu katika mkesha wa Jubilee yake, akikutana na wafanyikazi wa hisani katika Sandringham House.
Mwandishi wa BBC wa masuala ya kifalme Nicholas Witchell alisema kwamba Malkia amechanjwa kikamilifu.
Alisema amekuwa akichukua maisha "badala yake kwa urahisi zaidi" tangu kulazwa hospitalini kwa uchunguzi wa matibabu mnamo Oktoba mwaka jana.
Malkia alipokea chanjo yake ya kwanza ya Covid mnamo 9 Januari 2021.
Mke wa Prince Charles, Duchess wa Cornwall, alipimwa virusi vya ugonjwa huo wiki zilizopita, siku chache baada ya mumewe.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa duchess kupata Covid, na mara ya pili kwa Prince Charles.












