Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Afghanistan: Juu vita chini madini yenye thamani ya dola $1 trillion
Afghanistan unaweza kusema ni uwanja wa vita, kutokana na nchi hiyo kukumbwa na vita vya miongo karibu miwili. Miaka 20 iliyopita Marekani na washirika wake walianzisha operesheni maalumu ya kukabiliana na vikundi vya wapiganaji vilivyomo nchini humo, vikiongozwa na kundi kubwa la Taliban. Taliban kwa sasa linashikilia mamlaka nchini humo, baada ya kufanikiwa kuiangusha serikali ya rais Ashraf Ghani aliyekimbilia uhamishoni.
Maelfu ya watu hasa raia wa nchi hiyo na wa kigeni wamekuwa wakikusanyika kwenye uwanja wa ndege wa Kabul kwa ajili ya kukimbia kwenye mataifa yaliyo na usalama. Wana hofu na usalama wao. Watu hawa wanaacha mali zao kwa sababu mazingira hayaruhusu kubeba mali hizo zikiwemo nyumba, mifugo, samani, mashamba, ofisi na nyinginezo. Lakini kwa utajiri uliopo Afghanistan mali hizo si kitu, nchini hiyo ina madini ya kutosha yaliyogunduiwa mwaka 2010 na maafisa wa jeshi la Marekani,.
Maafisa hao pamoja na wataalam wa miamba na madini wamegundua nchi hiyo ina madini yenye thamani ya zaidi ya dola $1 trillion.
Aina za madini zilizopo
Nchi hiyo inatajwa kuwa na madini aina nyingi kama chuma, shaba na dhahabu pamoja na akiba ya madini adimu kabisa ya Lithiumu yanayotajwa kuwa ya kutosha na pengine akiba kubwa duniani. Kwa sasa nchi tatu za China, DRC na Australia — kwa sasa ndio wazalishaji wakubwa wa karibu asilimia 75% ya madini adimu yakiwemo ya lithium na cobalt.
Serikali ya Marekani inakadiria kuwa kiwango cha madini ya lithium yanayopatikana Afghanistan kinaweza kulingana na kiwango cha madini hayo nchini Bolivia, nchi inayoongoza kwa akiba kubwa ya madini hayo duniani.
Gari ya kawaida ya umeme inahitaji karibu mara sita ya gari ya kawaida kwa mujibu wa Mamlaka ya kimataifa ya kushughulikia masuala ya nishati (IEA). Madini ya Lithium, nickel na cobalt ni muhimu kwa utengenezaji wa mabetri. Mfumo wa umeme pia unahitaji kiwango kikubwa cha shaba na aluminum, huku madini mengine adimu hutumika kwenye sukamu zinazosaidia mitambo ya upepo.
Lakini kwanini Masikini?
Kwa mujibu wa ripoti ya benki ya duia ya mwaka 2020, Afghanistan ina uchumi unaodorora kila siku huku asilimia 90% ya watu wake wakiishi kwenye umasikini wa kutupwa wa chini ya dola $2 kwa siku. Nchi nyingi zenye serikali dhaifu ama zenye kukumbwa na mizozo na mapigano ya mara kwa mara zinatajwa kuwa katika nafasi finyu za kushughulikia rasilimali zake zinazoweza kusaidia maisha ya watu wake. Lakini nchi hizo zimekuwa kama na laaana ya kubarikiwa rasilimali, ambazo juhudi za kuzitumia kwa faida ya umma zimekuwa zikigonga mwamba.
Awali kabisa kwenye utafiti uliofanywa na Muungano wa Soviet, ulileta matumaini kwa Afghanistan kwamba madini yaliyogunduliwa yataleta mabadiliko makubwa kwenye uchumi wa nchi hiyo na watu wake. Lakini mambo yamekuwa tofauti. Licha ya mahitaji makubwa ya madini kama lithium, Afghanistan imekuwa na mtihani wa kunufaika nayo kutokana na hali ya usalama na vita vinavyokinza shughuli nyingi za uchumi.
Kwa sasa nchi hiyo inaingiza dola $1 billion pekee kwa mwaka kutoka sekta ya madini, kiwango ambacho ni kidogo kulingana na madini yaliyopo na hakilingani na uwekezaji unaolengwa Afghanistan. Vita vilivyodumu kwa miaka na miaka, vinazuia shughuli za uchimbaji na uwekezaji mkubwa katika sekta hiyo. Kwa ujumla wananchi hawanufaiki sana na madini yaliyopo nchini humo.
Kikwazo kingine kinachoiangusha Afghanistan ni teknolojia duni ya uchimbaji iliyonayo. Mbali na vita na hali tete ya usalama, teknolojia inayotumika kwenye shughuli za uchimbaji ni duni inayopelekea kuchimba kwa kiwango kidogo cha madini. Ingawa kuna fursa kwa kundi la Taliban, kuongeza uwekezaji kwenye sekta hiyo.
Wataalam wanasema uchimbaji mkubwa wa madini kama dhahabu, shaba, chuma na lithium unahitaji ujuzi mkubwa na teknolojia kubwa pamoja na muda wa kutafiti ili kutekeleza miradi kwa kiwango bora. IEA wanakadiria kuwa inachukua miaka kutoka ugunduzi mpaka uchimbaji wa madini.
Wananchi wanakimbia nchi yao sasa kutafuta usalama, Je ni fursa kwa mataifa rafiki na kundi la Taliban kama China na Urusi kutumia fursa hiyo? litabaki swali la muda mrefu.