Tetesi za soka Ulaya Jumatano 05.05.2021:Johnstone, Sterling, Bale, Sancho, Buendia, Kante, Depay

Manchester United imejiunga na mahasim wa ligi ya primia Tottenham na West Ham katika kinyang'anyiro cha msajili mlinda mlango wa West Brom Sam Johnstone, 28, ikijiandaa kuondoka kwa Mhispania David de Gea, 30, msimu huu wa joto. (ESPN)
United badala yake itamfuatilia mlinda mlango wa Aston Villa Muingereza Tom Heaton,35, kama Johnstone atapendelea kwenda West Ham.(Star)
West Brom watataka kiasi cha pauni milioni 20 kwa ajili Johnstone. (Telegraph)
Mlinzi wa zamani wa England Sol Campbell ni miongoni mwa wale walioomba nafasi ya kuwa mbadala wa Aidy Boothroyd katika nafasi ya meneja wa kikosi cha England kwa wachezaji wa chini ya miaka 21.
Campbell,46, ambaye alianza kazi ya umeneja katika klabu ya Macclesfield mwaka 2018 hakuwa kazini tangu alipoondoka Southend United mwezi Juni mwaka 2020. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid wanamfuatilia mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling,26, ambaye anaweza kuondoka Etihad kwa kitita cha pauni milioni 75. (Football Insider)
Kocha wa Everton Carlo Ancelotti anataka kumchukua mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 31, anayecheza kwa mkopo Tottenham msimu huu. (El Chiringuito, via Sport Witness)
Chelsea wanaweza kujiunga na Manchester United na Liverpool kuwannia saini ya winga Jadon Sancho baada ya Borussia Dortmund kushusha dau la kumnasa mchezaji huyo mwenye miaka 21. (Bild, via Football London)

Chanzo cha picha, Getty Images
Klabu hiyo ya Bundesliga itahitaji karibu pauni milioni 85 kwa ajili ya Sancho msimu huu wa joto,kiasi ambacho bado ni zaidi ya kile Manchester United iko tayari kulipa. (Eurosport)
Leeds United wanapenda kumsajili winga wa Club Bruge winga Mholanzi Noa Lang, 21. (Telegraph)
Wakati beki mwenye umri wa miaka 34 David Luiz anaingia miezi miwili ya mwisho ya kandarasi yake na Arsenal, wawakilishi wake wameanza kutafuta kilabu kipya kwa ajili ya Mbrazili huyo. (CBS Sports)
Tottenham itamsaka mshambuliaji mwingine wakiwa hawategemei kufanya uhamisho wa mkopo wa Vinicius, 26, kutoka Benfica kuwa wa kundumu (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Norwich City Emi Buendia, 24 anatolewa macho kwa kiasi kikubwa, huku Leeds United ikifikiria kumnyakua Muajentina huyo ambaye amehusishwa na taarifa za kutakiwa pia Arsenal, Aston Villa, Crystal Palace, Atletico Madrid, Sevilla na Villareal. (Footmercato-in French)
Rais wa zamani wa Inter Milan Massimo Moratti amemhimiza Narazzurri kujaribu kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea, Mfaransa N'Golo Kante,30, kabla ya jaribio lao la kutetea taji la Italia msimu ujao . (Sky Sport Italia)
Borussia Dortumund inapenda kumsajili kiungo wa kati wa England Alex Oxlade-Chamberlain kutoka Liverpool msimu wa joto. (Fichajes-in Spanish)
Barcelona imefanya mawasiliano ya awali na wawakilishi wa kiungo wa kati Gerson anayekipiga katika klabu ya Flamengo, wakati wakiangalia uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo Mbrazili mwenye miaka 23. (ESPN-in Portuguese)

Mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay, 27, ana hamu kubwa ya kusainiwa Barcelona na tayari ameanza kutafuta nyumba katika jiji la Catalin. (Mundo Deportivo in Spanish)
Massimiliano Allegri ameeleza nia yake ya kurejea kwenye uongozi wa mpira wa miguu na anahusishwa na taarifa za kurejea Juventus, wakati Real Madrid ikiwa kama chaguo jingine kwa Muitaliano huyo mwenye miaka 53. (Tuttosport-in Italian)
Roma na Inter Milan iko kwenye mapambano ya kupata saini ya kiungo wa kati wa Cagliari Nahitan Nandez, 25, (Calciomercato-in Italian)
Bayern Munich wanaongoza mbio za kumsajili kiungo wa kati Carney Chukwuemeka ,17,anayecheza klabu ya Aston Villa. (Football Insider)














