Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 30.04.2021: White, Abraham, Messi, Alaba, Ten Hag, Luk
Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, aliyeondoka Barcelona kujiunga na Atletico Madrid msimu uliopita amemtaka mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33, kusalia Nou Camp. (TV3, via Sport)
Aston Villa ipo kwenye tahadhari baada ya kujitokeza kuwa Chelsea iko tayari kukubali ofa ya takriban pauni milioni 40 kwa ajili ya mshambuliaji Tammy Abraham, 23. (Mirror)
Borussia Dortmund imeingia kwenye kinyanganyiro cha kumsajili mlinzi wa Uingereza Ben White, 23, huku Paris St-Germain, Manchester United na Arsenal zikimnyatia mchezaji huyo. (Sun)
Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, aliyeondoka Barcelona kujiunga na Atletico Madrid msimu uliopita amemtaka mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33, kusalia Nou Camp. (TV3, via Sport)
Real Madrid iko tayari kutangaza kumsajili mlinzi wa Austria David Alaba, 28, kwa uhamisho wa bure kutoka Bayern Munich mkataba wake utakapomalizika msimu huu. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Tottenham inataka kuzungumza na Erik ten Hag kuhusu kuwa kocha wao mpya baada ya Jose Mourinho kupigwa kalamu. Erik ten Hag, 51, yuko tayari kuchukua jukumu hilo jipya baada ya kuwa kocha wa Ajax kwa miaka minne. (Guardian)
Hata hivyo, Spurs bado inamfuatili kocha wa Leicester Brendan Rodgers, licha ya yeye mwenye kujiondoa kwenye kinyanganyiro hicho Jumatano. (Mail)
Inter Milan have imeieleza Manchester City kuwa haiku tayari kusikiliza ofa yoyote kwa ajili ya mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 27. (Calciomercato - in Italian)
Leicester itatoa dau lake kumsaka mlinzi wa Atalanta na Ujerumani Robin Gosens, 26, ikiwa itafanikiwa kuingia kwenye Ligi ya Mabingwa. (Tuttomercatoweb, via Team Talk)
Inter Milan inafikiria kutoa ofa yake ya mkataba mpya kwa mlinzi wa England Ashley Young ikiwa itashinda kombe la Serie A wikendi hii. Watford inataka kumsajili aliyekuwa mwanafunzi wake, 35. (Mirror)
Everton ni miongoni mwa vilabu kadhaa za Ligi ya Primia zinazo msaka mshambuliaji wa RB Leipzig raia wa Kore Kusini Hwang Hee-chan, 25. (Goal)
Kiungo wa kati wa Arsenal Bukayo Saka, 19, amesema hakusita kutia saini makubaliano mapya na Gunners, licha ya Borussia Dortmund na Liverpool kuonesha kuwa nazo zinamtaka. (ESPN)
West Ham na Newcastle zimeonesha nia ya kumsajili Mario Lemina wa Southampton. Kiungo huyo wa kati raia wa Gabon, 27, sasa hivi yuko Fulham kwa mkopo na anapatika kwa kima cha pauni milioni 7. (Guardian)
Mlinzi wa Chelsea Andreas Christensen amesema anataka kutia saini makubaliano mapya na klabu ya Ligi ya Primia. Mchezaji huyo, 25, anaichezea Stamford Bridge kwa mwaka wake wa 10. (Metro)
Leeds imekataa ofa kutoka kwa Legia Warsaw ya kumchukua mchezaji wa Poland Mateusz Bogusz, 19, msimu ujao kwa mkopo. (Football Insider)
Southampton ina mfuatilia mlinda lango wa West Brom Josh Griffiths kabla ya uwezekano wa kumsajili kipindi cha uhamisho mchezaji huyo, 19, ambaye ameonesha umahiri wake Cheltenham akiwa huko kwa mkopo msimu huu. (Football Insider)