Khadija, mwanamke muhimu katika kuanza kwa Uislamu

Illustration of a veiled woman in a Mosque

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Khadija bint Khuwaylid ni nani?

"Alivunja rekodi. Hata mwanamke wa kisasa angependa kufikia alichofikia miaka 1,400 iliyopita."

Hivi ndio vile Asad Zaman, imam kutoka mji wa Manchester (Uingereza), alivyomuelezea Khadija, mwanamke aliyezaliwa karne ya 6 mji ambao sasa hivi unajulikana kama Saudi Arabia.

Alikuwa akiheshimiwa, mwanamke tajiri na mwenye nguvu aliyekataa posa za wengi tu waliokuwa matajiri.

Na hatimaye, aliolewa mara mbili.

Mume wake wa kwanza alifariki dunia na inasemekana kwamba aliamua kutalakiana na mume wake wa pili.

Baada ya hapo, aliahidi kwamba hatawahi kuolewa tena... hadi alipokutana na mwanaume ambaye angekuwa mume wake wa tatu na wa mwisho.

Khadija aliona "baadhi ya sifa za kipekee [kwake] ambazo zilimfanya abadilishe fikra zake kuhusu ndoa," Zaman amezungumza na BBC.

Kawaida enzi hizo, Khadija ndiye aliyemchagua na kumposa.

Wakati huo alikuwa na umri wa miaka 40 huku mume wake akiwa na umri wa miaka 25 kutoka familia yenye unyenyekevu.

Lakini hii ni zaidi ya simulizi ya mapenzi; ndio chimbuko la dini ambayo ni ya pili kwa yenye idadi kubwa ya watu duniani.

Mume mpya wa Bi. Khadija, Muhammad, ambaye karibuni angekuwa mtume wa Kiislamu.

Mfanyabiashara

Camel caravan

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ngamia wa Khadija wakielekea Mashariki ya Kati

Robert Hoyland, Profesa wa historia ya kale Mashariki ya Kati katika chuo kikuu cha New York, ameonya kwamba ni vigumu kupata taswira kamili ya Khadija alikuwa nani, kwasababu kinachojulikana kumhusu kiliandikwa miaka mingi baada ya kifo chake.

Hata hivyo, vyanzo vingi vinaonesha kwamba alikuwa mwanamke mwenye "malengo makubwa, na uthubutu wa kipekee," Hoyland amezungumza na BBC.

Kwa mfano, alikataa kuolewa na binamu yake - kama familia yake ilivyokuwa inataka kulingana na tamaduni - kwasababu alitaka kujichagulia mume wake mwenyewe.

Khadija alikuwa binti wa mfanyabiashara aliyebadilisha biashara ya familia na kuifanya kuwa himaya ya kibiashara.

Baada ya baba yake kufariki dunia akiwa vitani, Khadija alichukua usukani.

"Bila shaka alikuwa na uzoefu," amesema mwanahistoria na mwandishi wa vitabu Bettany Hughes katika makala ya BBC.

"Ukweli ni kwamba utaalamu wake kibiashara ndio uliomfanya kuwa katika nyanja ambayo baadaye ingebadilisha historia ya dunia."

Msaidizi

Close up of Bettany Hughes

Chanzo cha picha, David Levenson/Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanahistoria Bettany Hughes: Khadija alikuwa anaishi maisha ya kipeke yake duniani

Khadija aliendesha biashara zake mji wa Mecca nchini (Saudi Arabia), na biashara yake ilihusisha misafara katika usafirishaji wa bidhaa kwenda na kutoka miji mikubwa Mashariki ya Kati.

"Khadija alikuwa na uzoefu wa kibiashara," amesema Bettany Hughes.

Misafara yake ilikuwa inakwenda umbali mrefu kutoka kusini mwa Yemen hadi kaskazini mwa Syria.

Ingawa sehemu ya utajiri wake ulikuwa unatoka kwa familia yake, Khadija pia naye alijitengenezea utajiri wake mwenyewe, amesema Fozia Bora, Profesa mshiriki wa historia ya Kiislamu katika chuo kikuu cha Leeds nchini Uingereza.

"Alikuwa mfanyabiashara aliyejiitegemea na mwenye kujiamini kwa hilo."

Khadija alikuwa mzoefu katika kuajiri wafanyakazi wake, kuchagua watu waliokuwa na ujuzi utakaonufaisha biashara yake.

Aliposikia kuhusu mwanamume aliyekuwa na sifa ya kuwa mwaminifu na mchapa kazi, na baada ya kufanya mazungumzo naye, alimwajiri kuongoza moja ya msafara wake.

Khadija alifurahia sana ujasiri wake na kadiri muda ulivyokwenda, alifurahishwa mno naye kiasi kwamba akaamua kuolewa tena.

Mtume Muhammad (S.A.W) - ambaye alikuwa yatima, alilelewa na mjomba wake - maisha yake yakaanza kubadilika ghafla" akawa thabiti na kustawi kiuchumi," amesema Fozia Bora.

Inaaminika kuwa wanandoa hao waliishi pamoja na kujaaliwa watoto wanne ingawa ni binti zake tu ndio waliojaaliwa kuishi baada ya utoto wao.

Pia kulikuwa na kitu kingine ambacho kilikuwa cha kipekee katika uhusiano wao:"Hii ilikuwa ni ndoa ya mke mmoja," Profesa Rania Hafaz, kutoka Taasisi ya Kiislamu ya London, amezungumza na BBC.

Hili lilikuwa la kipekee "kutoka mtazamo wa kijamii, wakati ambapo wanaume wengi walikuwa na wake wengi.

Ilikuwa ni jamii ya wanaume kuoa wake zaidi ya mmoja."

Panoramic view of Mecca

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Khadijah na familia yake ilikuwa inaishi Mecca, Saudi Arabia

Muhammad alizaliwa na kukulia katika kabila la Quraysh (kama Khadijah), wakati ambapo makundi kadhaa katika eneo hilo walikuwa wanaabudu miungu.

Miaka michache katika ndoa yake, Muhammad alianza mabadiliko na kufanya ibada tu, kuwa karibu na mola wake - na akaanza kwenda maeneo ya milimani kuzunguka mji mtakatifu wa Mecca na kufanya sala kimoyo moyo.

Kulingana na imani ya dini ya Kiislamu, Muhammad alipokea sura za kwanza kutoka kwa Mungu kupitia malaika Jibrili (A.S) malaika yule yule ambaye wakati mmoja alitangaza kwamba Bi. Mariam atakuwa mama yake Issa.

Na hivi ndio vile Koran, Kitabu kitakatifu kwa Waislamu kilivyoteremshwa kwa mtume Muhammad (S.A.W).

Inasemekana kwamba alipokuwa anapokea sura ya kwanza, aliogopa hasa kwasababu hakuelewa kitu gani kilikuwa kinaendelea.

"Hakuelewa alichokuwa anapitia wakati huo. Hakuwa na mtu ambaye angeweza kufananisha anachopitia wakati huo kwasababu hakukuzwa katika mazingira ya muamini Mungu mmoja," amesema Fozia Bora.

"Alikuwa amechanganyikiwa na kushtushwa na tuki hilo. Vyanzo vinasema wahyi aliyoshukishiwa haukuwa rahisi, na ingawa alichopitia kilikuwa cha kiungwana alishutuka sana."

Mtume Muhammad akaamua kuzungumza wazi "kwa mtu aliyejua kwamba yeye pekee ndiye ambaye angemuani," amesema Profesa Hoyland.

A copy of the Koran on a wooden book stand, in front of an open window

Chanzo cha picha, Getty Images

Khadija alimsikiliza na kumtuliza. Moyoni mwake, Bi. Khadija alijua kuwa hili ni jambo zuri na alimfariji.

Pia alitafuta ushauri kutoka kwa jamaa ambao walikuwa na ufahamu wa dini ya Kikiristo.

Inaaminika kuwa Waraqah ibn Nawfal alihusishwa na wahyi wa Muhammad hadi ule uliopokelewa na Musa.

"Alijua sura za awali," Bora anaelezea, kwahiyo "ilikuwa kama uthibitisho wa uhakika wa wahyi alipokea."

"Tunajua kwamba alipoanza kupokea sura za Korani, mtume Muhammad (S.A.W) mwenyewe alianza kujishuku.

Lakini Bi. Khadija alimhakikishia kuwa yeye, ni mtume," amesema Leila Ahmed, msomi wa Kiislamu, anayefundisha chuo kukuu cha Harvard.

Muislamu wa kwanza alikuwa mwanamke

Fozia Bora at her desk

Chanzo cha picha, Fozia Bora

Maelezo ya picha, Fozia Bora:Anavutiwa na historia ya Khadija

Wasomi wengi wanakubaliana na hilo, kwasababu Khadija alikuwa wa kwanza kusikia sura alizoshukishiwa mtume Muhammad (S.A.W), lazima atambuliwe kama Muislamu wa kwanza katika historia, wa kwanza kuslimu kwa dini hii mpya.

"Aliamini na kukubali ujumbe huo," amesema Foiza Bora.

"Nafikiri hilo lilimpa mtume Muhammad imani kubwa na kuanza kusambaza dini hiyo kulimfanya ahisi kana kwamba anasauti."

Mwana historia Bettany Hughes anasema hadi kufikia hatua hiyo, Muhammad alikwenda kinyume na viongozi wa kabila lake na kuamua kuanza kutangaza dini yake hadharani: "Kuna Mungu mmoja pekee, Allah. Na kuabudu wengine ni ukafiri."

Kulingana Foiza Bora, mtume Muhammad alipoanza kufunza Uislamu, alitengwa na wengi wa jamii ya Mecca ambao walipinga imani ya kuwa [Mungu ni mmoja.

"Lakini Khadija," ameongeza Foia Bora, "alimuunga mkono na alimpa ulinzi alivyohitaji kweli wakati huo."

"kwa kipindi cha miaka 10, Khadija alitumia mtandao wa familia yake na utajiri wake wote kumuunga mkono mume wake na pamoja na kufadhili dini mpya," amesema Hughes, "dini ambayo msingi wake wa kuabudu Mungu mmoja kilileta utata, katika jamii ambayo ilikuwa inaamini miungu".

'Mwaka wa huzuni'

Woman praying in a Mosque

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Katika historia ya kiislamu kuna wanawake kadhaa maarufu katika dini

Khadija alifanya kila alichoweza kumuunga mkono mume wake - lakini mwaka 619, alikuwa mgonjwa na akafariki dunia.

Baada ya kuishi pamoja kwa miaka 25, mtume Muhammed aliathirika sana na kifo chake.

"Hakuwahi kurejea katika hali yake ya kawaida kutokana na kifo cha Bi. Khadija," amesema Profesa Hoyland.

"Cha kipekee zaidi kuhusu vyanzo vya wakati huo ni namna wanavyozungumza juu ya Khadijah kama rafiki wa dhati wa mtume Muhammad, karibu zaidi hata kuliko ilivyokuwa na washirika wake kama Abu Bakar au Omar," profesa ameongeza.

Mwanahistoria Bettany Hughes amesema kuwa Waislamu bado wanakumbuka mwaka wa kifo chake kama 'Mwaka wa huzuni'.

Hatimaye, mtume Muhammad (S.A.W) akaoa tena, na wakati huo alikuwa kwenye ndoa ya wake wengi.

Mmoja wa wasimuliaji wa hadithi alikuwa Aisha, mmoja ya wake zake mtume Muhammad (S.A.W), ambaye pia alikuwa mwanamke mwingine maarufu katika historia ya Kiislamu.

"Bila shaka mtume alimuelezea simulizi za Bi. Khadijah, na anakumbuka kilichotokea alipokuwa anapokea sura ya kwanza ya Korani alipokuwa mtume," amesema Fatima Barkatulla.

Mfano wa kuigwa

Young Muslim women looking into an iPad

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wasichana wa Kiislamu wanavutiwa na simulizi ya Bi. Khadija

Kwa Foiza Bora, kujifahamisha historia ya Khadija ni muhimu katika kuondoa imani kuwa katika jamii za Kiislamu zamani za kale, wanawake walikuwa wanafungiwa nyumbani tu.

Muhammad hakumtaka Khadijah kuacha kufanya alichotaka.

Kwanza anasema kuwa, Uislamu ulitoa haki zaidi na umaarufu kwa wanawake wakati huo.

"Kwangu mimi, kama mwanahistoria na Muislamu, Khadija ni mwanamke anayewapa wengine moyo, na inasemekana Fatima [mmoja kati ya binti zake na mtume Muhammad] pamoja na Aisha, ni miongoni mwa wanawake wengine maarufu," amesema Foiza Bora.

"Walikuwa wenye akili, waliopenda siasa na walikuwa na jukumu muhimu katika kusambaza dini ya Kiislamu na kuanzisha jamii ya Kiislamu."

"Inafurahisha kwangu mimi," kama msomi, "kufundisha wanafunzi wangu, ama wawe ni Waislamu au la, kuhusu wanawake hawa."