Je, rafiki zako ni wabaya kwa afya yako?

marafiki

Chanzo cha picha, Nappy

Kila mwanzo wa mwaka watu wengi huamua kufanya madiliko mazuri na ya muhimu katika maisha yao.

Wengi hujiwekea malengo mbalimbali kama vile kuacha kula vyakula visivyo na afya au kuamua kuanza kufanya mazoezi ya mwili.

Lakini sio mabadiliko yote ya afya tunakusudia kuyafanya, kwa kuwa mara nyingi tunaiga tabia za marafiki zetu, wafanyakazi wenzetu na familia ambayo wapo kama sisi au tunatamani kuwa kama wao.

Kwa bahati mbaya, muda mwingine tunaiga hadi tabia ambazo sio nzuri kwa afya zetu, kama vile kuvuta sigara au kula sana.

Kitendo hiki kinaweza maanisha magonjwa kama ya moyo, kiharusi na saratani.

Tabia hii huwa kama inasambaa kutoka mtu mmoja kwenda mwingine, kutoka kwa rafiki mmoja kwenda kwa mwingine.

Je rafiki zako wanaweza kuathiri maisha yako?

Marafiki

Chanzo cha picha, Getty Images

Watu tunaowathamini na wale tunaoanana nao kila siku hutengeneza mazingira yetu ya kujamiana na watu.

Utafiti uliofanywa na shirika la Framing Heart umechunguza nguvu ya kujamiana tangu miaka ya 1940, kwa kufatilia vizazi vitatu vya raia fulani katika mji wa Framingham, ndani ya jimbo la Massachutes nchini Marekani.

Kuongezeka unene

Utafiti ulionesha kuwa mtu mmoja alikuwa hatarini kuwa na unene uliopitiliza kama mtu mmoja kati ya wale watu wake wa karibu ana tatizo kama hilo.

Ilipendekeza kuwa asilimia 57 walikuwa hatatarini zaidi kama mtu huyo wa karibu ni rafiki, asilimia 40 kama ni ndugu na asilimia 37 kama ni mwenzi wake.

Commuters cycling to work

Chanzo cha picha, Getty Images

Athari hii ilikuwa mbaya zaidi kama watu wawili ni wa jinsia moja na iliunganishwa na jinsi gani mtu mmoja anavyojisikia kuhusu mtu mwingine.

Katika utafiti wa Framingham ulionyesha uzito wa mtu haukuathiriwa na ule wa jirani ambaye wanaonana kila siku iwapo kama hawakuwa na urafiki wa karibu.

Presentational grey line

Kiwango cha talaka, uvutaji sigara na unywaji wa pombe pia umeoneka kusambaa kati ya marafiki na familia.

Urafiki

Chanzo cha picha, NAPPY

Utafiti huu ni muhimu sana.

Ingawaje tunaweza kuathirika kutokana na umri wetu na inaweza kuwa ni kwa sababu ya matatizo fulani.

Lakini hatari kubwa kwetu ya kupata magonjwa ya kawaida na yasiyo ambukizwa huongezeka kwa haraka kutokana na tabia fulani ambazo rafiki zetu wanazo kama:

  • Unavuta sigara
  • Mlo wako
  • Kiwango cha mazoezi ya mawili unayofanya
  • Kiwango cha pombe unacho kunywa

Magonjwa haya yasio ambukizwa kama kiharusi, magonjwa ya moyo, saratani, na kisukari na ugonjwa wa mapafu, husababisha vifo saba kati ya kumi duniani kote.

mlo

Chanzo cha picha, Nappy

  • Kuathirika kwa hisia zetu
  • Kujamiana pia kunaweza kuathiri tabia na hali zetu.

Kwa mfano vijana wanovuta sigara inaweza huwa wameshawishika na watu maarufu wenye umri kama wao ambao wanavuta sigara, kwa ujumla idadi ya wanaovuta sigara inaongezeka huku idadi ya watu wanaoacha ikishuka.

ashtray with cigarette butts

Chanzo cha picha, Getty Images

Pembeni na hayo, vijana ambao rafiki zao walikuwa wanasumbumbuliwa na matatizo ya hali walikutwa wakiwa hatarini kusumbuliwa na tatizo kama hilo na kinyume chake.

Lakini kuwa na hali ya chini inajulikana kuathiri ubora wa maisha ya vijana wengi na muda mwingine inaweza sababisha kupata ugonjwa wa upweke huko mbeleni.

Watu tunaowathamini na wale tunaoanana nao kila siku hutengeneza mazingira yetu ya kujamiana na watu.

Presentational grey line
line