Chama cha Democratic chaweka wazi mashtaka dhidi ya rais Donald Trump

Chanzo cha picha, AFP
Chama cha Democratic nchini Marekani kinatarajia kuweka wazi mashtaka dhidi ya rais Donald Trump, ambayo ni muhimu katika hatua za kumwondoa madarakani.
Wasaidizi wa chama hicho wamesema nakala za kumwondoa madarakani zitajikita kwenye matumizi mabaya ya madaraka na kuliingilia bunge.
Bwana Trump anashutumiwa kwa kuzuia misaada kwenda kwa Ukraine kwa ajili ya manufaa yake ya kisiasa ndani ya Marekani.
Hata hivyo, Trump amepuuzia hatua hiyo na kuiona kama kampeni chafu dhidi yake.
Taarifa hiyo iliowasilishwa na bunge la wawakilishi itasababisha kufanyika kwa kura ya kumtoa madarakani.
Kama nakala hiyo ikikubaliwa na bunge, ambalo linaendeshwa na chama cha Democratic, kesi hiyo itasikilizwa ikiwezekana mapema mwezi Januari.
Inaaminika kuwa bunge limetayarisha nakala za kumuondoa madarakani, ambako kutaaanza na kusikilizwa kwa hoja kwa muda wa miezi miwili.
Hatua hii ya kumuondoa madarakani ilianzishwa baada ya mtu ambaye hakutaka kujulikana kulalamika kwa bunge la Congress mwezi Septemba kuhusu simu iliyopigwa na rais Trump kwa rais wa Ukraine.

Chanzo cha picha, AFP
Trump anakabiliwa na shutuma gani?
Katika simu hiyo bwana Trump amesikika akihusisha msaada wa jeshi la Marekani kwa Ukraine ili kuanzisha uchunguzi ambao unaweza kumsaidia kisiasa.
Kama matokeo ya uchunguzi yatapatikana, chama cha Democratic kinasema Bw Trump alitoa misaada miwili ya kijeshi yenye thamani ya dola milioni 400 za kimarekani ambazo tayari zilikuwa zimeshapangwa na bunge, na mkutano na rais Volodymyr Zelensky.
Chama cha Democratic kinasema shinikizo hili kwa mshirika wa Marekani linaonesha matumizi mabaya ya madaraka.
Uchunguzi wa kwanza ambao Bw Trump aliutaka kutoka kwa Ukraine ulikuwa unahusu makamu wa rais mstaafu Joe Biden, ambaye ni mshindani wake mkubwa kutoka chama cha Democratic na mtoto wake Hunter. Hunter Biden alijiunga na baraza la kampuni ya nishati la Ukraine, pale baba yake alipokuwa makamu wa rais mstaafu Barack Obama.
Kitu cha pili ambacho Trump alitaka ni Ukraine kujaribu kurekebisha njama zinaonyesha kuwa Ukraine na sio Urusi ndio walioingilia uchaguzi mkuu uliopita wa Marekani. Nadharia hii ilikuwa dhaifu, na vyombo vya uchunguzi nchini Marekani vimeficha kusema kuwa Moscow ndio waliofanya udukuzi wa barua pepe mwaka wa 2016.
Je kuna namna yoyote ambayo rais atapatwa na hatia?
Ni viongozi wachache wa Marekani ndio walifikia katika hatua ya namna hii. Kwa kuwa chama cha upinzani cha Democratic kina wingi wa wawabunge, kuna uwezekano kuwa Trump ataondolewa.
Democratic wanataka kura hiyo ipigwe kabla ya mwisho wa mwaka. Je kuna namna yoyote ambayo rais atapatwa na hatia?













