"Ndugu wa kambo wa Trump" azua kicheko mitandaoni

Chanzo cha picha, Rickey Smiley
Labda mwenyewe umetambua hivyo. Huyu si ndugu wa kambo wa Donald Trump kutoka Kenya!
Lakini hili halijazuia vicheko kwenye mitandao kutokana na picha hii.
Wakati picha hii ilitumaa kwa ukurasa wa Facebook wa mchekeshaji na mtangazaji wa redio nchini Marekani Ricky Smiley, mamia ya watu walitoa maoni na maelfu ya wengine kusambaza picha hiyo.
Ukweli ni kwamba mtu aliye kwenye picha hii na rais wa Ghana Nana Akufo-Addo.

Chanzo cha picha, Nana Akufo-Addo
Hii ndiyo picha iliyofanyiwa ukarabati ambapo anaonekana akimsalimia mcheza filamu raia wa Ghana Kofi Adu.

Chanzo cha picha, Nana Akufo-Addo








