Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mabaharia wa Kiasia sasa huru kurudi nyumbani
Baadhi ya kundi la mabaharia wa Kiasia walioachiwa na maharamia wa Kisomali baada ya kuwa matekani kwa karibu miaka mitano wamezungumzia kuhusu mateso yao nchini kenya.
Mmoja wa mateka hao Arnel Balbero kutoka Ufilipino aliiambia BBC kuwa walikua wakipata mateso zaidi ya wanyama na ilibidi kuwinda panya kwa ajili ya chakula.
Maharimia hao waliwakabidhi mabaharia hao 26 kwa mamlaka huko kaskazini mwa somalia katika mji Galkayo siku ya jumamosi asubuhi. waliwasili mji mkuu wa Kenya, Nairobi siku ya Jumapili.
Sasa wanarudi katika nchi zao huko China, Taiwan, Vietnam, Kambodia, Ufilipino na Indonesia. Mabaharia hao walitekwa mwaka 2012 wakati maharamia walipoteka mashua yao ya uvuvi karibu na ushelisheli.