Patrice Motsepe: Kutoka kuwa bilionea Afrika hadi rais wa Caf

Patrice Motsepe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Patrice Motsepe

Ijumaa, Patrice Motsepe atakuwa rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) wakati ambapo raia huyo wa Afrika Kusini atakuwa bila mpinzani kwenye uchaguzi utakaofanyika Morocco.

Anavyofahamika kama mmoja kati ya matajiri barani Afrika, Bwana Motsepe pia ni mwasisi wa klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini waliokuwa mabingwa wa Afrika mwaka 2016 - lakini je yeye ni nani? Mwandishi wa BBC Pumza Fihlani amekuwa akimfuatilia kwa karibu:

Watu wengi wanafahamu msemo wa "Kuendana na akina Jones", lakini je! Unajua nahau "Kuendelea na Motsepes"?

Lazima uwe una ufahamu - kwasababu Patrice Motsepe ni mtu wa tisa tajiri Afrika, kulingana na jarida la Forbes, na miongoni mwa mabilionea weusi nchini mwake.

Mwasisi na mwenyekiti wa kampuni ya madini ya African Rainbow Minerals, alikuwa bilionea mwaka 2008 - huku jarida la Forbes likimtaja kuwa mwafrika wa kwanza kuingia katika kundi hilo.

Kuongezeka kwa umaarufu na utajiri wake haujapotea katika nchi ambayo sheria za kibaguzi zilifanya wengi kutumbukia katika lindi la umaskini na ukosefu wa fursa za kibiashara kwa miongo mingi.

Leo hii mara nyingi utasikia "Mimi sio Motsepe" wa mzazi ambaye hata huwezi kumuomba pesa au usikie utani wa "Mimi ni kijana wa Motsepe" wakiwa na pesa kidogo tu zinazowasumbua.

Kwa kifupi, amekuwa mwakilishi wa utajiri na utani na hili linaonesha kuwa uwepo wa Patrice Motsepe una umuhimu mkubwa kwa wengi .

Ni ukumbusho wa kile kinachowezekana, sasa basi je Motsepe alifanikiwa vipi kuwa bilionea?

Kununua vya rahisi lakini malengo ni ya juu

Motsepe alianzisha kampuni yake ya kwanza ya uchimbaji madini mwaka 1994, na kuanza kununua migodi inayozalisha dhahabu kidogo miaka michache baadaye wakati ambapo soko la dhahabu lilikuwa linakabiliwa na changamoto ya kuporomoka na bei yake ikiwa nzuri.

Mwaka 2016 klabu yake ya Mamelodi Sundowns ilikua klabu ya pili ya Afrika kusini kushinda kombe la klabu bingwa Afrika
Maelezo ya picha, Mwaka 2016 klabu yake ya Mamelodi Sundowns ilikua klabu ya pili ya Afrika kusini kushinda kombe la klabu bingwa Afrika

Mwaka 2016, klabu ya Mamelodi Sundowns ikawa ya pili kutoka Afrika Kusini kushinda Ligi ya Mabingwa Afrika.

Na muda si muda, migodi nayo ikaanza kubadilishwa na kuwa yenye faida.

Afueni kubwa kwake inahusishwa na sera za kuwezesha watu weusi kiuchumi nchini Afrika Kusini ili kukabiliana na tatizo na ukosefu wa usawa ambalo lilikuwepo kwa miongo kadhaa kwasababu ya utawala wa wazungu walio wachache uliofikia ukomo wake mwaka 1994.

Kampuni za uchimbaji migodi zilihitajika kuwa na angalau asilimia 26 ya umiliki kabla ya kupatiwa leseni.

Na tangu wakati huo, utawala wa migodi wa Motsepe umekuwa ukikua na sasa hivi ana nia ya kuanza kujishughulisha na upatikanaji wa madini ya kobalti, nikeli, madini ya chuma, shaba na makaa ya mawe.

Ni mtu aliyejitafutia mali

Alizaliwa Januari 28 mwaka 1962.

Motsepe alitajwa Patrice Lumumba, waziri mkuu wa kwanza kuteuliwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Akiwa kijana, alijifunza ujasiriamali kutoka kwa baba yake Augustine Motsepe, aliyekuwa na familia ya kifalme ya Tswana.

Pia alikuwa mmiliki wa duka ambalo ni mmarufu sana Afrika Kusini eneo la Hammanskraal, nje ya mji wa Pretoria.

Patrice Motsepe na mkewe Precious wana ushirikiano wa karibu na chama cha ANC
Maelezo ya picha, Patrice Motsepe na mkewe Precious wana ushirikiano wa karibu na chama cha ANC

Wakati shule zimefungwa, alikuwa akifanya kazi na baba yake na kuanza kujifunza namna ya kufanya biashara.

Akasomea uwakili na kuwa mtu wa kwanza mweusi kuongoza kampuni maarufu, Bowman Gilfillan.

Baba huyo wa watoto watatu pia ana shahada katika uchimbaji wa madini na anaendesha kampuni ya mawakili kutoka chuo kikuu cha Johannesburg

Utajiri wake ukisemekana kuwa dola bilioni 3.

Tajiri huyo pia anasaidia miradi kadhaa ya elimu na afya kupitia wakfu wake.

Mnamo mwaka 2013, Motsepe alikuwa Mwafrika wa kwanza kutia saini ahadi ya Bill Gate na Warren Buffett ya kujitolea kutoa angalau nusu ya utajiri wake.

Motsepe yupo karibu na mamlaka aki kati ya rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa na rais wa zamani wa Marekani Barrack Obama

Motsepe pia yuko karibu sana na watu wenye mamlaka - anavyoonekana hapo mwaka 2018 kati ya Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama.

Mwaka jana, wakfu wa Motsepe uliahidi kutoa randi dola bilioni 1 kusaidia kukabiliana na janga la virusi vya corona Afrika Kusini.

Wakati ambapo kila kitu anachoshika Motsepe kinaonekana kubadilika na kuwa dhahabu, amekuwa akilengwa na baadhi ya vyama vya kisiasa ambavyo vinasema kwamba nguvu kubwa iliyo na familia yake inawafanya kupata upendeleo fulani.

Lakini amekuwa akikanusha madai hayo na kusema kwamba utajiri wake umepatikana kwa njia halali.