Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 14.04.2020: Mbappe, Haaland, Sancho, Torres, Ighalo, Onana

Erling Braut Haaland

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Real Madrid kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 19, kutoka Borussia Dortmund mwaka huu

Real Madrid wana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 19, kutoka Borussia Dortmund mwaka huu na mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21, kutoka Paris St-Germain 2021. (Marca)

Real Madrid pia inakabiliana na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa England wa miaka 20 Jadon Sancho, ambaye anachezea klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund. (Daily Star)

Jadon Sancho

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Manchester United kumenyana na Real Madrid kumsajili winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho

Borussia Dortmund imetoa dau la Euro milioni 40 sawa na (£34.9m) kumnunua winga wa miaka 20 wa Uhispania na Valencia Ferran Torres, ambaye mkataba wake unamalizika 2021. (Bild, via Sport)

Mshambuliaji waNigeria Odion Ighalo, 30, atalazimika kupokea paundi £200,000-kwa wiki ikiwa anataka kubadilisha-uhamisho wake wa mkopo Manchester United kutoka klabu ya Shanghai Shenhua inayoshiriki Super League ya China, ambako alikuwa nalipwa where he was on £300,000- kwa wiki. (Daily Star)

Odion Ighalo

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mshambuliaji waNigeria Odion Ighalo kupunguziwa akiamua kujiunga rasmi na Manchester United

Chelsea italazimika kulipa £5m ikiwa inataka kumsajili kiungo wa kati wa Derby County wa miaka 19- Muingereza Max Bird, ambaye mchezo wake umemvutia mkufunzi Blues Frank Lampard alipokuwa meneja wa klabu hiyo. (Football Insider)

Paris St-Germain imeungana na Barcelona katika kinyang'anyiro cha kumsaka kipa wa Cameroon na Ajax Andre Onana, 24. (L'Equipe, in French, subscription required)

Ivan Rakitic

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiungo wa kati wa Croatia Ivan Rakitic, amekosoa jinsi Barcelona ilivyomfanyia alipokataa kujiunga na Paris St-Germain

Kiungo wa kati wa Croatia Ivan Rakitic, 32, amekosoa jinsi Barcelona ilivyomfanyia aliposema kuwa alikataa Paris St-Germain mwaka jana kama sehemu ya mkataba ambao ungelimrudisha mshambuliaji wa Brazil Neymar, 28, Nou Camp. (Mundo Deportivo, in Spanish)

Real Madrid ina mpango wa kusalia na mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic, 22, ambaye ananyatiwa na Arsenal. (AS, in Spanish)

Ousmane Dembele

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 22, kusalia Barcelona

Mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 22, kusalia Barcelona kwasababu hakuna klabu iko tayari kumlipa euro milioni 60 sawa na(£52.3m). (Marca)

Tottenham wanpania kumsajili kiungo wa kati wa wa Uholanzi Lamare Bogarde, 16, kutoka Feyenoord. (Football Insider)