Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 02.04.2020: Belligham, Braithwaite, Sancho, Meunier

Jude Bellingham

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jude Bellingham

Mshambuliaji wa England Marcus Rashford amekiri kuwa anatamani sana kucheza na mshambuliaji mwenzake wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 20, Katina klabu ya Manchester United msimu ujao. (Sun)

West Ham wanajiandaa kuweka dau la kushutukiza la £15m, kumnunua mshambuliaji wa Barcelona na Norway Martin Braithwaite, 28, ambaye amecheza mara tatu pekee tangu alipohamia Nou Camp Januari. (Mail)

Borussia Dortmund wanakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Birmingham City Jude Bellingham.(Bild, via Birmingham Mail)

Sancho

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Jadon Sancho

Manchester United wanafuatilia hali ya Thomas Meunier katika klabu ya Paris Saint-Germain huku hatima ya beki huyo wa miaka 28, raia wa Ubelgiji ikiwa haijulikani. (90min.com)

Mkufunzi wa Everton Carlo Ancelotti ana matumaini ya kujumuika tena mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez, 28. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba amedokeza kuwa kipaumbele chake kwa sasa ni kujiunga na Real Madrid dirisha la usajili litakapofunguliwa, kwasababu nyota huyo wa miaka 27 anataka kuungana na Zinedine Zidane. (90min.com)

Braithwaite

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Martin Braithwaite

Mchezaji nyota wa Chelsea Willian, anafikiria Liverpool wanaongoza jedwali la msimamo wa ligi ya Primia kwasababu hawajabadilisha mkufunzi wao kutoka 2015. (ESPN Brazil)

Huku hayo yakijiri, Willian, 31, huenda akaungana tena na mkufunzi wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri katika klabu ya Juventus mkataba wake Stamford Bridge utakapomalizika msimu huu. (Tuttosport)

Leeds United watamsajili kipa mfaransa Illan Meslier, 20, kwa mkataba wa kudumu kutoka Lorient ikiwa watapanda daraja na kujiunga na ligi ya Primia. (Mirror)