Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 20.10.2019: Sterling, Eriksen, Solskjaer, Koulibaly, Ceballos, McGinn, Matic

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City inajiandaa kumlipa Raheem Sterling kitita cha £450,000-kwa wiki ili kukatiza azma ya Real Madrid ya kumnunua mshambuliaji huyo wa Uingereza wa miaka 24. (Star)
Paris St-Germain itamenyana na Real Madrid kujaribu kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. (Mail on Sunday)
Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anatafakari hatma yake ya baadae katika klabu hiyo ikihisi kuwa uwepo wake utaathiri hali ya mambo katika uwanja wa Old Trafford. (Metro)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson alionekana akizungumza na Solskjaer katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wakatibwa mazoezi kuelekea mechi yao dhidi yao na Liverpool leo Jumapili. (Manchester Evening News)
Mwenyekiti wa Napoli Aurelio De Laurentiis amekiri kuwa "wakati utawadia" ambapo klabu hiyo italazimika kumuuza mchezaji wa safu ya kati na nyuma wa klabu hiyo Kalidou Koulibaly,28, ambaye amehusishwa na tetesi za kuhamia Manchester United. (Sky Sports Italia, via Sunday Express)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham inamlenga beki wa West Brom Nathan Ferguson, huku Crystal Palace pia ikimnyatia mchezaji huyo wa miaka 19. (Sun on Sunday)
Kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, 23, amefanya mazungumzo na rais wa Real Madrid Florentino Perez kuhusu uwezekano wa kubadilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Arsenal kuwa uhamisho wa kudumu. (El Desmarque, via Mail on Sunday)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Aston Villa Dean Smith amesema klabu hiyo haina mpango wa kumuuza kiungo wa kimataifa John McGinn, 25. (Sunday Express)
Vilabu vya Manchester City na Barcelona vinapania kumnunua mchezaji wa safu ya kati waklabu ya Anderlecht Albert Sambi Lokonga, 19, ambaye amehusishwa na uhamisho kwenda Sevilla. (Marca)
Manchester United wanatafakari uwezekano wa kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja kiungo wa kati wa Serbia Nemanja Matic kwa kuhofia kumpoteza mchezaji huyo wa miaka 31, ambaye analengwa na Inter Milan, kwa uhamisho wa bure msimu ujao. (Corriere dello Sport, via Sunday Express)
Tetesi Bora Jumamosi
Mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 32, anasema kwamba baadhi ya watu katika klabu hiyo hawamtaki mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, kurudi. (Metro 95.1 via Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wanafikiria kumsajili aliyekuwa kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 na raia wa Ujerumani alijiunga na Juventus 2018. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil anaamini amefanywa kisingizio katika klabu hiyo. Raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 31 anasema kwamba atasalia katika klabu hiyo hadi mwisho wa kandarasi yake 2021. (Times via The Athletic - subscription required)

Chanzo cha picha, Getty Images
United pia wana hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Leicester na England James Maddison, 22, mbali na mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele. (ESPN)














