Mahakama ya juu nchini Uganda yaidhinisha sheria yenye utata dhidi ya mapenzi ya jinsia moja

Kundi linalojumuisha wanaharakati, viongozi wa kidini na wanasheria wanasema watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu and Asha Juma

  1. ‘Mawe yaliporomoka kama risasi’ – manusura wa tetemeko Taiwan

    fv

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Jengo linaonekana likiwa limeporomoka nusu

    Waokoaji nchini Taiwan wanafanya kazi ya kuwaokoa takribani watu 100 ambao wamekwama, siku moja baada ya kisiwa hicho kukumbwa na tetemeko kubwa zaidi la ardhi katika kipindi cha miaka 25.

    Mtu mmoja aliyenusurika anasimulia jinsi tetemeko hilo lilivyoporomosha mawe “kama risasi” katika eneo la mgodi wa makaa ya mawe anakofanya kazi.

    Tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.4 lilipiga karibu na eneo la mashariki la Hualien, na kuua watu tisa na kujeruhi zaidi ya 1,000.

    Wengine waliokwama chini ya mahandaki na karibu na mbuga ya taifa wameokolewa na helikopta, lakini watu 34 bado hawajulikani walipo.

    Ugawaji wa chakula umefanyika kupitia angani kwa watu kadhaa walionasa katika maeneo yaliyoathirika, ripoti za ndani zinasema.

    "Mlima ulianza kuporomosha mawe kama risasi, hatukuwa na mahali pa kukimbilia, kila mtu alikimbia kando ya mifuko ya mchanga ili kujificha," manusura, aliyetambuliwa kwa jina lake la pili Chu, aliambia Shirika la Habari la Taiwan.

    Watatu kati ya tisa waliofariki walikuwa wasafiri kwenye njia ya kongoro inayoelekea Hifadhi ya Kitaifa ya Taroko, nje kidogo ya Hualien.

    Katika mji wa Hualien, mji mkuu wa eneo hilo - juhudi za kutoa msaada zinaendelea, huku wafanyakazi wakitumia vifaa kubomoa majengo kadhaa yaliyoharibiwa.

    Pia unaweza kusoma:

  2. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu kwa leo. Kwaheri.

  3. WHO yaendelea na kazi Gaza 'chini ya hatari kubwa'

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wapalestina wakikusanyika kupokea msaada katika mji wa Gaza mwezi uliopita

    Msafara uliokuwa na wafanyakazi saba wa shirika la kutoa misaada la World Central Kitchen (WCK) haupaswi kamwe kushambuliwa, anasema Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus.

    Alisema msafara huo ulikuwa na nembo ya WCK, akiongeza kuwa "watu wenye njaa watakosa chakula" kwa sababu wafadhili walisimamisha shughuli zao baada ya tukio hilo.

    Ghebreyesus aliongeza kuwa shirika lake linaendelea kufanya kazi huko Gaza "chini ya hatari kubwa". Alitoa wito wa kuwepo kwa mfumo bora wa utatuzi ili misafara ya misaada iweze kuendeleza shughuli zake kwa usalama, na kwa maeneo zaidi ya kuingia kaskazini mwa Gaza.

  4. Amos Makalla Katibu mpya wa Itikadi na Uenezi wa CCM

    Amos Makalla

    Chanzo cha picha, Amos Makalla, Instagram

    Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi, imekutana hii leo chini ya Mwenyekiti wake na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

    Imefanya mabadiliko madogo ya Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambapo Amos Makalla amechaguliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi na Mafunzo, akichukua nafasi ya Paul Makonda ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

    John Mongella amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Bara, akichukua nafasi ya Anamringi Macha ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

    Wajumbe wengine ni pamoja na Jokate Mwegelo amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, ambaye hapo kabla alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa chama hicho.

    Kadhalika Ally Salum Hapi amekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania.

  5. Rais mpya wa Senegal Bassirou Diomaye ni nani?

    Maelezo ya video, Rais mpya wa Senegal Bassirou Diomaye ni nani?

    Rais mpya wa Senegal Bassirou Diomaye ameahidi kufanya kazi bila kuchoka ili kuimarisha demokrasia ya nchi na kuhakikisha amani na utulivu wake.

    Mwandishi wa BBC Thomas Naadi alitembelea mji aliozaliwa wa Ndiaganiao na kuzungumza na baadhi ya wanafamilia kuhusu malezi ya Faye.

  6. Taiwan: Juhudi za uokoaji zinaendelea baada ya 700 kujeruhiwa katika tetemeko la ardhi

    .

    Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock

    Juhudi za uokoaji zinaendelea nchini Taiwan baada ya tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.4 kupiga pwani ya mashariki ya kisiwa hicho na kuua takriban tisa na kujeruhi zaidi ya 800.

    Watu wapatao 127 wamenaswa katika vinjia vilivyoporomoka na kwenye barabara za milimani kando ya ufuo wa pwani.

    Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa 18km (maili 11) kusini mwa mji wa Hualien, lakini mitetemeko mikali ilisikika katika mji mkuu wa Taipei, umbali wa zaidi ya kilomita 100.

    Hili ndilo tetemeko kubwa zaidi kuwahi kuikumba Taiwan katika kipindi cha miaka 25.

    Soma zaidi:

  7. Zimbabwe yatangaza ukame kuwa janga la kitaifa

    Zimbabwe imetangaza ukame kuwa janga la kitaifa ambao umewaacha takriban watu milioni tatu wakikabiliwa na njaa - na kuifanya kuwa nchi ya tatu kusini mwa Afrika kutoa tahadhari hiyo.

    Mvua kidogo zimesababisha maafa katika sehemu kubwa ya eneo hilo, ambapo kulingana na Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa, watu milioni 20 hawapati chakula chenye lishe bora mara kwa mara.

    Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alisema nchi hiyo inahitaji $2bn (£1.6bn) ili kukabiliana na athari za uhaba wa chakula ndani ya mipaka yake.

    Kama ilivyo katika nchi jirani za Zambia na Malawi, ambazo pia zimetangaza njaa kuwa janga la kitaifa, mvua kidogo imeangamiza takriban nusu ya zao la mahindi la Zimbabwe – chakula kikuu cha taifa hilo.

    Uhaba wa nafaka umeongeza bei ya vyakula.

    Zimbabwe sasa inajiunga na wengine kutafuta mahindi katika soko la kimataifa.

    Mamlaka zinasema kwamba idadi ya watu wanaohitaji msaada wa chakula itakuwa kubwa kuliko makadirio ya awali ya milioni 2.7.

  8. Rais wa zamani wa shirikisho la soka Uhispania akamatwa katika uchunguzi wa ufisadi

    .

    Chanzo cha picha, EPA

    Luis Rubiales, rais wa zamani wa shirikisho la soka la Uhispania (RFEF), amekamatwa kama sehemu ya uchunguzi wa ufisadi.

    Aliwekwa kizuizini alipowasili Madrid kutoka Jamhuri ya Dominika.

    Anashukiwa kupokea kamisheni kinyume cha sheria wakati wa kujadili dili nono la kuandaa mashindano ya Spanish Super Cup nchini Saudi Arabia.

    Bw Rubiales ambaye anakanusha makosa yoyote huenda akafungwa kifungo cha miaka miwili na nusu jela.

    Baada ya kushuka kwenye ndege, aliingizwa kwenye gari jeusi na Walinzi waliokuwa wamevaa Kiraia.

    Polisi sasa wana saa 72 kumhoji Bw Rubiales, ambaye alikuwa katika Jamhuri ya Dominika wakati polisi walipopekua nyumba yake mwezi uliopita.

    Pia walipekua makao makuu ya shirikisho la soka na kukamata watu kadhaa.

    Bw Rubiales pia anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa kosa la unyanyasaji wa kijinsia kwa kumbusu mchezaji Jenni Hermoso mdomoni baada ya fainali ya Kombe la Dunia mwaka jana.

    Bi Hermoso na wachezaji wenzake walisema busu hilo halikutakikana na lilidhalilisha.

    Bw Rubiales alilazimika kujiuzulu, lakini amekanusha makosa yoyote.

    Soma zaidi:

  9. Mahakama ya juu nchini Uganda yaidhinisha sheria yenye utata dhidi ya mapenzi ya jinsia moja

    .

    Chanzo cha picha, AFP

    Mahakama ya Katiba ya Uganda imeidhinisha sheria yenye utata dhidi ya mapenzi ya jinsia moja, ambayo inatoa adhabu ya kifungo cha maisha jela na adhabu ya kifo kwa wale wanaojihusisha na baadhi ya vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

    Lakini mahakama ilidhoofisha sheria hiyo, ikisema kuwa baadhi ya sehemu zilikiuka haki za kikatiba.

    Sehemu zinazoharamisha tabia kama vile kuruhusu ngono kwa wapenzi wa jinsia moja kutokea katika jengo la mtu, kushindwa kuripoti vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na kumpa mtu ugonjwa usiotibika kupitia ngono ya mapenzi ya jinsia moja zitakabiliwa.

    "Tunakataa kubatilisha Sheria ya Kupambana na Mapenzi ya jinsia moja 2023 kwa ujumla wake, wala hatutatoa amri ya kudumu dhidi ya utekelezaji wake," jaji mkuu Richard Buteera alisema wakati wa uamuzi huo Jumatano.

    Waopinga wanasema watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

    Ombi la kubatilisha sheria hiyo liliwasilishwa na wanataaluma wa Uganda, wanaharakati wa haki za binadamu, wanasheria, waandishi wa habari, wabunge na viongozi wa dini.

    Walisema kuwa sheria hiyo inakiuka haki za kimsingi zinazotolewa na katiba, kama vile haki ya faragha na uhuru wa kutobaguliwa.

    Waliongeza kuwa sheria hiyo ilikiuka ahadi za nchi chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu.

    Licha ya wasiwasi kama huo, sheria hiyo imeungwa mkono kwa kiasi kikubwa nchini humo. Wabunge wamewashutumu wapinzani katika nchi za Magharibi kwa kujaribu kuishinikiza Afrika kukubali mapenzi ya jinsi moja.

    Soma zaidi:

  10. Botswana yatishia kupeleka tembo 20,000 nchini Ujerumani

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Botswana ametishia kutuma ndovu 20,000 nchini Ujerumani katika mzozo kuhusu uhifadhi.

    Mapema mwaka huu, wizara ya mazingira ya Ujerumani ilipendekeza kuwe na masharti makali ya uwindaji kwa ajili ya michezo.

    Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi aliviambia vyombo vya habari vya Ujerumani kuwa hii itawafanya watu kuwa maskini nchini mwake.

    Alisema idadi ya tembo iliongezeka kutokana na juhudi za uhifadhi, na masharti ya uwindaji kulisaidia kuwazuia.

    Wajerumani wanapaswa "kuishi pamoja na wanyama, kwa jinsi unavyojaribu kutuambia," Bw Masisi aliambia gazeti la Ujerumani la Bild. "Hii sio mzaha."

    Botswana ni nyumbani kwa takriban theluthi moja ya idadi ya tembo duniani - zaidi ya 130,000 - zaidi ya nafasi iliyonayo ya uhifadhi.

    Walikuwa wakisababisha uharibifu wa mali, kula mazao na kuwakanyaga wakazi, aliambia Bild.

    Botswana hapo awali imetoa tembo 8,000 kwa nchi jirani ya Angola, na imetoa mamia zaidi kwa Msumbiji, kama njia ya kupunguza idadi yake.

    "Tungependa kutoa zawadi kama hiyo kwa Ujerumani," Bw Masisi alisema, akiongeza kwamba hatakubali jibu la hapana.

    Botswana ilipiga marufuku uwindaji kwa ajili ya michezo mwaka 2014, lakini iliondoa vikwazo hivyo mwaka 2019 baada ya kukabiliwa na shinikizo kutoka kwa jamii za wenyeji.

    Soma zaidi:

  11. Ukraine yapunguza umri kwa wanaojiunga na jeshi

    .

    Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametia saini kuwa sheria mswada wa kupunguza umri wa wanaosajiliwa kuingia jeshini kwa miaka miwili kutoka 27 hadi 25.

    Kyiv imekabiliwa na hasara kubwa vitani baada ya miaka miwili ya vita, ambapo Urusi imenufaika kutokana na kuwa na wanajeshi wengi.

    Hatua hiyo itairuhusu Ukraine kusajili watu wengi ili kuwa na wanajeshi wengi wa akiba, baada ya idadi ya waliojitolea kupungua.

    Bw Zelensky alisema mnamo Desemba kwamba wanajeshi 500,000 zaidi walihitajika.

    Ingawa mswada huo ulipigiwa kura na wabunge mnamo Mei 2023, haukuanza kutumika kwa sababu Bw Zelensky hakuutia saini.

    Haijabainika mara moja ni nini kilimsukuma rais kutia saini mswada huo siku ya Jumanne, hata hivyo ameonya hapo awali kuhusu mipango ambayo Urusi inaweza kuwa nayo kuanzisha mashambulizi ya majira ya kuchipua au majira ya kiangazi mwaka huu.

    Kutia saini kwa Bw Zelensky katika mswada huo kunaweza kuashiria juhudi za Ukraine za kujenga ngome imara za ulinzi ili kujiandaa na mashambulizi ya Urusi.

    Vikosi vya Ukraine vilikuwa na matumaini ya kurudisha maeneo mengi yaliyochukuliwa na Urusi pamoja na kukata njia za usambazaji wa Urusi hadi Crimea.

    Lakini kwa kukosa ubora wa anga na kukabiliwa na ulinzi wa kutisha wa Urusi, uwanja wa kukabiliana na mashambulizi wa Kyiv ulisimama mwanzoni mwa majira ya baridi na kuna hofu kwamba majeshi ya Urusi yanaweza kuishinda Ukraine.

    Soma zaidi:

  12. Uhusiano wa Israeli na washirika wake waonyesha dalili za kuyumba

    .

    Chanzo cha picha, EPA

    Mazungumzo kati ya Uingereza na Israel katika siku iliyopita yamekuwa yasio ya kawaida.

    Balozi wa Israel aliitwa kwa Ofisi ya Mambo ya Nje kwa mara ya kwanza baada ya miaka 12.

    Na mazungumzo ya Rishi Sunak na mwenzake wa Israel jana usiku yalikuwa ya wazi.

    Sunak alimwambia Benjamin Netanyahu kuwa "amechukizwa" na mauaji hayo, kwamba wafanyikazi wengi wa mashirika ya kutoa misaada na raia wamefariki na hali "inazidi kutovumilika".

    Mazungumzo ya aina hiyo sio unayoweza kutarajia kutoka kwa taarifa rasmi kati ya washirika wawili.

    Na tumeona mfadhaiko sawa na huo kutoka kwa nchi zingine ambazo kwa kawaida zinaunga mkono Israeli. Shinikizo kwa Netanyahu linaongezeka.

    Uingereza pia imeweka wazi kuwa inataka ulinzi zaidi kwa raia, masharti kidogo ya utoaji wa misaada na hatua zaidi kuchukuliwa kukarabati miundombinu muhimu kama hospitali.

    Serikali ya London huenda ikasubiri kuona iwapo Israel itatekeleza matakwa ya uchunguzi huru, wa uwazi na wa kina.

    Lakini uhusiano huo unaonyesha dalili za kuyumba - kama vile uhusiano wa Israeli na washirika wengine.

    Soma zaidi:

  13. Video: Tazama wakati tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.4 lilipopiga Taiwan

    Maelezo ya video, Tazama wakati tetemeko la ardhi la ukubwa wa 7.4 lilipoikumba Taiwan
  14. Bei ya mafuta yapanda Tanzania

    .

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Bei ya mafuta yapanda Tanzania

    Bei za mafuta nchini Tanzania zimepanda mwezi huu Aprili ikilinganishwa na mwezi Machi 2024.

    Katika Jiji la Dar es Salaam mafuta ya petroli yamependa kutoka Tsh. 3,163 mwezi Machi hadi 3,257 kwa lita huku dizeli ikiongezeka kutoka Tsh. 3126 hadi 3,210 mwezi Aprili.

    Mamlaka ya udhibiti wa huduma ya Nishati na maji Ewura imesema kwamba ongezeko hilo la bei limechangiwa na kuongezeka kwa bei ya mafuta yaliosafishwa katika soko la dunia, mbali na ongezeko la kiwango cha kubadilisha fedha za kigeni kwa asilimia 3.19 kutokana na ongezeko la matumizi ya Euro kulipia mafuta yalioagizwa.

    Bidhaa hiyo pia imeongezeka bei katika miji ya Tanga , na Mtwara ambako itauzwa kutoka Tsh. 3,209 hadi Tsh. 3,303.

  15. Sudan yavifunga kwa muda vituo vya televisheni vya pan-Arab kutokana na uhusiano mbaya

    Sudan imevifungia vituo vitatu vya Televisheni vya Pan-Arab, ikivishutumu kwa "ripoti zisizo za kitaalamu na uchapishaji unaodhuru".

    Sky News Arabia inayomilikiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Al Arabiya na Al Hadath inayomilikiwa na Saudi Arabia, ambazo zimeathiriwa na agizo hilo, zimeripoti kwa mapana kuhusu vita vya wenyewe kwa wenyewe na machafuko ya kisiasa nchini Sudan.

    Kusimamishwa huko kulichochewa na watangazaji hao "kutojitolea kwa taaluma na uwazi unaohitajika" na kushindwa kwao kuhuisha leseni zao, Waziri wa Habari Graham Abdel Gader alinukuliwa akisema.

    Kusimamishwa kwa Sky News Arabia inayofadhiliwa na UAE pia kulitokana na "uchapishaji mbaya", kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

    Al Hadath na Al Arabiya walisema hawakufahamishwa rasmi kuhusu kusimamishwa kazi na mara nyingi wamehuisha leseni zao.

    Kusimamishwa huko kumekuja siku chache baada ya wizara ya mambo ya nje ya Sudan kuishutumu Sky News Arabia kwa kupeperusha bandia za wanamgambo.

    Kituo hicho kilitumia video ya shambulio la kundi la wanamgambo wa al-Shabab nchini Somalia mwaka 2016 kuhusu makundi ya wanamgambo wanaodaiwa kupigana pamoja na Wanajeshi wa Sudan.

    Uhusiano kati ya Sudan na UAE umedorora baada ya jeshi la Sudan na vyombo vya habari vya Magharibi kushutumu UAE kwa kusambaza silaha kwa Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF) katika mzozo wa karibu mwaka mzima.

    Muungano wa Wanahabari wa Sudan (SJS) ulitaja uamuzi huo "ukiukaji wa wazi wa uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari".

  16. Ousmane Sonko ateuliwa kuwa waziri mkuu wa Senegal

    .

    Chanzo cha picha, Senegal Presidency/X

    Rais mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amemtaja kiongozi wa chama kikuu cha upinzani kuwa waziri mkuu wake.

    Ousmane Sonko ni mshauri wa kisiasa wa Rais Faye na wawili hao walikuwa wamefungwa muda mfupi kabla ya uchaguzi wa Machi.

    Walipewa msamaha, pamoja na wafungwa wengine wengi wa kisiasa, na Rais anayemaliza muda wake Macky Sall."

    Saa chache baada ya kuchukua madaraka kama rais wa Senegal, mheshimiwa Faye amemteua Sonko kuwa waziri mkuu," ofisi ya rais ilichapisha kwenye X.

    Awali Bw Sonko alikuwa ametajwa kuwa mgombea urais wa upinzani hadi alipokamatwa na kuamuliwa kuwa hana sifa ya kugombea nafasi hiyo - hatua iliyozua maandamano makubwa.

    Wakati wa kampeni wagombea wote walielezea mageuzi makubwa ya kisiasa na kiuchumi, ikiwa ni pamoja na maridhiano ya kitaifa baada ya miezi kadhaa ya misukosuko iliyosababishwa na kufungwa kwao jela.

    Katika hotuba yake ya kuapishwa siku ya Jumanne, Rais Faye alisema Senegal itakuwa nchi ya matumaini yenye demokrasia iliyoimarishwa.

  17. Tetemeko la ardhi: China yatoa msaada kwa Taiwan

    Mamlaka ya Uchina imetoa taarifa mara baada ya tetemeko hilo kutokea, ikisema wako tayari kutoa msaada wa maafa.

    Pwani ya mashariki ya Uchina iko kilomita 180 tu (maili 111) kutoka Taiwan.

    "China ina wasiwasi mkubwa kuhusu hali hiyo na inatoa pole za dhati kwa watu wa Taiwan walioathiriwa na maafa," alisema Zhu Fenglian, msemaji wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Baraza la Serikali.

    Vyombo vya habari vya serikali ya China pia vimekuwa vikiripoti kwa wingi maafa hayo.China na Taiwan zina uhusiano wa wasiwasi.

    Taiwan inajiona kuwa nchi huru, lakini Beijing inaona kuwa ni jimbo lililojitenga na ambalo hatimaye litakuwa sehemu ya nchi, na haijakataza matumizi ya nguvu kufanikisha hili.

    Mvutano huo ni wa mara kwa mara - saa moja kabla ya tetemeko la ardhi wizara ya ulinzi ya Taiwan ilikuwa imetoa taarifa ya kila siku ikibainisha kuwa ndege 20 za kijeshi za China zilivuka katika eneo lake la ulinzi wa anga katika muda wa saa 24 zilizopita.

  18. Mgonjwa miongoni mwa raia waliouawa katika shambulio la waasi DR Congo

    Watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa ADF walichoma nyumba wakati wa shambulio hilo (picha ya maktaba)

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa ADF walichoma nyumba wakati wa shambulio hilo (picha ya maktaba)

    Raia 10 waliuawa katika shambulio mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa Allied Democratic Forces (ADF), ripoti zinasema.

    Waasi hao walichoma moto kituo cha afya, kupora maduka na kuchoma nyumba katika kijiji jirani cha Mangodomu siku ya Jumanne, kulingana na Emmanuel Kathembo Salamu, meya wa jiji la Mangina katika jimbo la Kivu Kaskazini.

    "Jeshi linawasiliana na adui. Saikolojia inatawala hapa," meya alinukuliwa akisema.

    Mgonjwa katika kituo hicho cha afya aliripotiwa kuwa miongoni mwa raia waliouawa wakati wa shambulio hilo.

    Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bado halijatoa tamko lolote kuhusu uvamizi huo.

    Awali ADF ilikuwa ni kundi la kijihadi la Uganda lakini iliahidi utiifu kwa Islamic State mwaka 2019.

    Miaka miwili baadaye, majeshi ya Uganda na DR Congo yalianzisha operesheni ya pamoja ya kijeshi dhidi ya ADF, lakini walishindwa kudhibiti mashambulizi yao.

  19. Habari za hivi punde, Tetemeko Taiwan: Zaidi ya 700 wajeruhiwa - idara ya moto

    .

    Chanzo cha picha, Iris Li

    Shirika la Kitaifa la Zimamoto la Taiwan limesema watu 711 wamejeruhiwa katika tetemeko la ardhi; huku watu 77 wakibaki "wamenaswa".

    Maafisa wanasema kufikia sasa watu wanne wanajulikana kufariki.

  20. Video:Tazama: Tetemeko la ardhi lasababisha maporomoko ya ardhi mashariki mwa Taiwan

    Maelezo ya video, Tazama: Tetemeko la ardhi lasababisha maporomoko ya ardhi mashariki mwa Taiwan