Wakuu wa jeshi la Ethiopia-Somaliland wakutana huku kukiwa na mvutano wa kikanda
Pande hizo mbili zilitia saini mkataba Januari 1 ili kuipa Ethiopia fursa ya kibiashara na kijeshi baharini
Moja kwa moja
Yusuf Jumah and Ambia Hirsi
Niger: Utawala wa kijeshi wamwachia huru mwana wa kiume Mohamed Bazoum,

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum na mke wake bado wanazuiliwa na utawala wa kijeshi. Mtoto wa kiume wa Rais wa Niger aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum ameachiliwa huru na mahakama ya kijeshi baada ya kukaa kizuizini kwa zaidi ya miezi mitano.
Salem Bazoum aliondoka kuelekea Togo baada ya juhudi za upatanishi za viongozi wa eneo hilo kukusaidia kuachiwa kwake.
Alizuiliwa pamoja na wazazi wake katika ikulu ya rais baada ya jeshi kufanya mapinduzi Julai mwaka jana.
Wazazi wake bado wako kizuizini, huku jutawala wa kijeshi ikikataa kuitikia shinikizo la kidiplomasia kuwaachilia.
Katika taarifa, mahakama ya kijeshi ilisema kuwa kuachiliwa kwa Bw Bazoum Jnr ni kwa muda tu, na "tutawasilaian naye mara tu atakapohitajika kufanya hivyo".
Alikuwa ameshtakiwa kwa njama ya kuhujumu mamlaka ya serikali kufuatia mapinduzi hayo.
Mnamo Oktoba, junta ilidai kuwa rais aliyepinduliwa na familia yake, wapishi wake wawili na maafisa wawili wa usalama walifanya jaribio lisilofaulu la kutoroka.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Togo Robert Dussey alikuja Niger kumsindikiza Bw Bazoum Jnr nje ya nchi, taarifa ya mahakama hiyo ilisema. Serikali ya Togo ilithibitisha kuachiliwa kwake, lakini haikutoa maelezo kuhusu aliko.
Sierra Leone pia ilihusika katika juhudi za upatanishi ili kupata kuachiliwa kwa mtoto wa kiume wa rais aliyepinduliwa, iliongeza katika taarifa yake.
Mwezi uliopita, mahakama ya muungano wa kanda ya Afrika Magharibi Ecowas iliamua kwamba kuzuiliwa kwa familia ya Bazoum ilikuwa hatua ya kiholela.
Iliamuru kuachiwa kwao, na kurejeshwa kwa Bw Bazoum kama rais.
Utawala wa kijeshi umepuuza uamuzi huo, na umesema kuwa kutakuwa na mpito wa hadi miaka mitatu kwa utawala wa kiraia.
Bw Bazoum aliondolewa madarakani na mkuu wa walinzi wa rais, Jenerali Abdourahamane Tiani, katika mapinduzi ambayo yalilaaniwa na Ecowas na mataifa ya Magharibi, ikiwa ni pamoja na ukoloni wa zamani Ufaransa.
Pia unaweza kusoma:
Wakuu wa jeshi la Ethiopia-Somaliland wakutana huku kukiwa na mvutano wa kikanda

Chanzo cha picha, ETHIOPIA DEFENCE FORCE
Wakuu wa jeshi la Ethiopia isiyo na ile ya Somaliland wamekuwa wakijadiliana kuhusu ushirikiano wa kijeshi huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu makubaliano ambayo yanaweza kuipa Ethiopia kambi ya jeshi la wanamaji kwenye Ghuba ya Aden.
Pande hizo mbili zilitia saini mkataba Januari 1 ili kuipa Ethiopia fursa ya kibiashara na kijeshi baharini.
Somalia ilikiita kitendo cha uchokozi. Inachukulia Somaliland kama sehemu ya eneo lake na imeapa kutetea uhuru wake.
Somaliland iliyokuwa chini ya ulinzi wa Uingereza, ilijitenga kutoka Somalia mwaka 1991 lakini haitambuliwi kimataifa kama taifa huru.
Mkuuwa jeshi la Ethiopia Birhanu Jula alizungumza na Meja Jenerali wa Somaliland Nuh Ismael Tani kuhusu "njia zinazowezekana za kufanya kazi pamoja" katika mkutano wa Jumatatu mjini Addis Ababa, jeshi la Ethiopia lilisema katika taarifa.
Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.
Soma:
Habari za hivi punde, Macron amteua Attal, 34, kuwa Waziri Mkuu wa Ufaransa

Chanzo cha picha, LUDOVIC MARIN/AFP/POOL
Maelezo ya picha, Gabriel Attal (Kulia) ana jukumu la kuongoza serikali katika uchaguzi wa Bunge la Ulaya mwezi Juni Gabriel Attal ameteuliwa kuwa waziri mkuu ajaye wa Ufaransa, huku Emmanuel Macron akilenga kufufua urais wake na serikali mpya.
Akiwa na umri wa miaka 34, ndiye Waziri Mkuu mdogo zaidi katika historia ya kisasa ya Ufaransa, akimzidi cheo hata Msoshalisti Laurent Fabius aliyekuwa na umri wa miaka 37 alipoteuliwa na François Mitterrand mwaka wa 1984
Bw Attal anachukua nafasi ya Élisabeth Borne, ambaye alijiuzulu baada ya kuhudumu kwa miezi 20.
Kwa muda wote huo alihangaika na ukosefu wa wingi wa wabunge bungeni.
Gabriel Attal, ambaye kwa sasa ni waziri wa elimu, hakika anafanya miadi ya kuvutia macho.
Sasa atakuwa na jukumu la kuiongoza serikali ya Ufaransa katika uchaguzi muhimu wa Bunge la Ulaya mwezi Juni.
Kupanda kwake kumekuwa kwa kasi.
Miaka kumi iliyopita alikuwa mshauri asiyejulikana katika wizara ya afya, na mwanachama wa mrengo wa Wanasoshalisti.
Sierra Leone yawafungulia mashtaka wanajeshi 27 kwa jaribio la mapinduzi

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Jeshi la Sierra Leone lilisema lilifanikiwa kutibua jaribio la mapinduzi Novemba mwaka jana baada ya watu wenye silaha kuvunja ghala la kijeshi na magereza kadhaa mjini Freetown. Mahakama nchini Sierra Leone imewashtaki wanajeshi 27 kwa madai ya jaribio la mapinduzi.
"Mashtaka hayo ni pamoja na uasi, kushindwa kukandamiza uasi, mauaji, kusaidia adui, kuwasiliana na adui na makosa mengine yanayohusika," wizara ya ulinzi ilisema katika taarifa yake.
Novemba mwaka jana, watu wenye silaha walivamia ghala la kijeshi na magereza kadhaa mjini Freetown, na kuwaachilia karibu wafungwa 2,000.
Mamlaka ilielezea hatua hiyo kama jaribio la "kupindua" serikali.
Wiki iliyopita, Rais wa zamani Ernest Bai Koroma alishtakiwa kwa uhaini kuhusiana na tukio hilo hilo.
Alikanusha kuhusika kwa vyovyote katika matukio ambayo watu 20 waliuawa.
Mamlaka pia inamfungulia mashtaka mmoja wa walinzi wa rais wa zamani wa Bw Koroma pamoja na polisi 11 wa zamani na maafisa wa magereza.
Wameshutumiwa kwa uhaini, kuficha uhaini na "kuhifadhi, kumuelekeza na kumsaidia adui".
Ghasia za mwezi Novemba zilikuja miezi mitano baada ya uchaguzi ambao ulishuhudia Rais wa sasa Julius Maada Bio kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili.
Matokeo hayo yalikataliwa na upinzani na kukosolewa na waangalizi wa kimataifa kwa ukosefu wa uwazi.
Maelezo zaidi:
Boeing 737 Max 9: United Airlines yapata vifaa vilivyolegea wakati wa ukaguzi,
Vifaa vinavyohitaji "kuimarishwa zaidi" zimepatikana wakati wa ukaguzi wa ndege za aina ya Boeing 737 Max 9, shirika la ndege la United Airlines limesema.
United Airlines ilisema "matatizo" yanayohusiana na plagi za milango "yatarekebishwa" kabla ya aina hiyo ya ndege kuanza kutumika.
Ukaguzi ulianza baada ya sehemu ya ya ndege ya 737 Max 9 inayomilikiwa na shirika la ndege la Alaska kuanguka kutoka angani siku ya Ijumaa.
Alaska Airlines inasema tangu wakati huo imepata "vifaa vilivyolegea" kwenye ndege za Max 9.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga (FAA), ambayo inadhibiti usafiri wa anga nchini Marekani, imezuia ndege 171 za aina aina hiyo kupaa.
United ilisema: "Tangu tulipoanza ukaguzi wa awali siku ya Jumamosi, tumepata matukio ambayo yanaonekana kuhusiana na masuala ya kufunga kwenye plagi ya mlango - kwa mfano, boliti ambazo zilihitaji kukazwa zaidi."
Plagi ya mlango ni kipande, kilicho na dirisha, ambacho kinajaza nafasi sehemu ya kutoka kwa dharura endapo ajali itatokea.
Ni sehemu hiyo ya ndege ya Alaska Airlines ambayo ilianguka kwa kasi katikati ya safari kwenye jimbo la Oregon la Marekani, hatimaye ikatua kwenye bustani ya nyuma ya mwalimu.
Ndege hiyo ilitua kwa dharura lakini hakuna abiria au mfanyakazi hata mmoja aliyejeruhiwa vibaya.
Wanajeshi wa DRC wazingira nyumba ya Moise Katumbi

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Moïse Katumbi Vikosi vya usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo vilizingira kwa muda nyumba ya mwanasiasa mkuu wa upinzani Moïse Katumbi, ambaye alishika nafasi ya pili katika uchaguzi wa mwezi uliopita wenye utata.
Alizuiwa kuondoka nyumbani kwake kusini mwa jimbo la Katanga siku ya Jumatatu, msemaji wake Hervé Diakesse alisema.
Lakini vikosi vya usalama vilijiondoa baadaye kwa amri ya gavana wa eneo hilo.
Bw Katumbi amekataa ushindi wa kishindo wa Rais Félix Tshisekedi katika uchaguzi wa mwezi uliopita kama uzushi.
Viongozi wengine watano wa upinzani, akiwemo Martin Fayulu, aliyeshika nafasi ya tatu, wameitisha maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi.
Jumatatu jioni, wakaazi wa kijiji cha Kashobwe walionekana kwenye video za mitandao ya kijamii wakikusanyika nyumbani kwa Bw Katumbi baada ya habari kuenea kwamba vikosi vya usalama vinamzuia kuondoka.
Jamaa mmoja wa Bw Katumbi aliambia tovuti ya habari ya RFI ya Ufaransa kwamba nyumba hiyo ilikuwa imezingirwa na "askari waliokuwa na silaha nzito".
"Tunajitahidi kufahamu ni kwa nini," Bw Diakesse, aliliambia shirika la habari la Reuters.
Katika juhudi za kujaribu kutuliza mzozo huo uliokuwa ukiongezeka, gavana wa jimbo hilo Jacques Kyabula Katwe aliamuru vikosi vya usalama kuondoka, akitaja tukio hilo kuwa la "faux pas".
Alisema nia ya awali ya vikosi vya usalama ilikuwa kulinda mali ya Bw Katumbi dhidi ya vitendo vya uharibifu vinavyoweza kutokea.
Uchaguzi wa Disemba 20 ulikumbwa na matatizo mengi ya vifaa, huku baadhi ya waangalizi huru wakiibua wasiwasi kuhusu kura hiyo.
Ni mgombea mmoja pekee ambaye ameenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais.
Wakuu wanasema hawana imani na mahakama na badala yake wametaka idadi ya watu "kupinga udanganyifu wa uchaguzi" bila kutoa maelezo yoyote.
Bw Tshisekedi alipata takriban 73% ya kura, huku Bw Katumbi akipata 18% na Bw Fayulu 5%, tume ya uchaguzi ilisema
Serikali za Magharibi zimetoa wito wa utulivu huku kukiwa na hofu ya kuzuka kwa ghasia za baada ya uchaguzi, huku afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu, Volker Turk, akionya kuhusu kuongezeka kwa mvutano wa kikabila.
Takriban watu 20 waliuawa katika ghasia zinazohusiana na uchaguzi wakati wa maandalizi ya upigaji kura.
Makumi ya watu waliuawa na kujeruhiwa katika saa 24 zilizopita - wizara ya Hamas

Chanzo cha picha, Reuters
Wizara ya afya ya Gaza inayodhibitiwa na Hamas inasema vifo 57 vilirekodiwa katika hospitali ya al-Aqsa katika muda wa saa 24 zilizopita.
Taarifa iliyotumwa kwenye Telegram ilidai kuwa watu 65 waliojeruhiwa pia waliletwa katika hospitali hiyo - ambayo iko katikati mwa Gaza - katika muda huo huo.
Siku ya Jumatatu, mashirika ya kimataifa ya misaada yalisema yanaondoka hospitalini, kwa sababu ya mashambulio ya Israeli kwenye eneo hilo.
Makumi ya watu waliuawa kaskazini mwa Gaza - ripoti
Tuliripoti mapema kwamba vifo 57 vilirekodiwa katika hospitali ya al-Aqsa katikati mwa Gaza katika saa 24 zilizopita.
Sasa Wafa, shirika rasmi la habari la Palestina, linasema Israel ilifanya mashambulizi ya anga katika maeneo ya kati na kusini, ikiwa ni pamoja na kuzunguka kambi za Maghazi na al-Bureij.
Shirika hilo linasema makumi ya watu waliuawa huko Jabalia na Beit Hanoun, ambazo zote ziko kaskazini mwa ukanda wa Gaza.
Israel inasema inalenga magaidi na miundombinu yao, na inajaribu kupunguza vifo vya raia.
Israel inasema 'imewaangamiza magaidi 40' huko Khan Younis
Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) Avichay Adraee ametoa taarifa kuhusu mashambulizi katika Ukanda wa Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita.
- Katika kusini mwa Ukanda huo, anasema askari wa IDF walihamia "ndani" ya Khan Younisna na "kuwaangamiza magaidi 40", akiongeza "njia mbalimbali za mapigano na fursa muhimu za handaki zilipatikana"
- Katika eneo la Maghazi katikati mwa Gaza, anasema IDF iliona "wahujumu" na kuelekeza ndege ambayo "iliwashambulia na kuwaangamiza"
- Na kutoka baharini,Adraee anasema vikosi vya wanamaji vya Israel vilishambulia maeneo ya kijeshi, maghala na magari ya wanamaji yanayotumiwa na Hamas huko Gaza.
Urushaji wa satelaiti ya China juu ya Taiwan wasababisha tahadhari katika kisiwa hicho

Chanzo cha picha, VCG
Mamlaka ya Taiwan ilisema Jumanne mchana kwamba satelaiti ya Uchina iliruka juu ya anga ya kusini mwa Taiwan.
Watumiaji wa simu za rununu kote nchini Taiwani walipokea "tahadhari ya uvamizi wa anga" ikiwaonya "kuwa makini kwa usalama wako".
Satelaiti hiyo ilirushwa kutoka kwenye Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Xichang katika mkoa wa Sichuan nchini China saa 15:03 kwa saa za huko, wizara ya ulinzi ya Taiwan ilisema.
Kituo cha utangazaji cha China CCTV kilithibitisha kuwa setilaiti kwa jina Einstein Probe ilikuwa imerushwa kutoka kituo hicho.
Iliongeza kuwa misheni ya uzinduzi ilikuwa "mafanikio kamili".
Taiwan ilisema wizara yake inaangalia mkondo wa satelaiti hiyo "kutoa tahadhari ipasavyo na kujibu" hali hiyo.
Vyombo vya habari vya Taiwan vinasema hii ni mara ya kwanza kwa serikali yake kutoa tahadhari ya aina hii kisiwani kote.
Tukio hilo linakuja siku chache kabla ya uchaguzi muhimu wa rais na wabunge nchini Taiwan, ambao wachambuzi wamesema utachagiza mwelekeo wa uhusiano kati ya Beijing na Washington.
Korea Kusini yapitisha sheria ya kupiga marufuku biashara ya nyama ya mbwa

Chanzo cha picha, Reuters
Korea Kusini imepitisha sheria mpya, ambayo inalenga kukomesha uchinjaji na uuzaji wa mbwa kwa ajili ya nyama yao ifikapo 2027.
Sheria hiyo inalenga kukomesha tabia ya karne nyingi ya kula nyama ya mbwa.
Nyama ya mbwa imekosa kupendwa na watu wengikatika miongo michache iliyopita. Vijana hasa huiepuka.
Chini ya sheria, kufuga au kuchinja mbwa kwa ajili ya kuliwa kutapigwa marufuku, vile vile kusambaza au kuuza nyama ya mbwa. Wale watakaopatikana na hatia ya kufanya hivyo wanaweza kupelekwa jela.
Wale wanaochinja mbwa wanawezakufungwa jela miaka mitatu, huku wale wanaofuga mbwa kwa ajili ya nyama au kuuza nyama ya mbwa wanaweza kutumikia kifungo cha miaka miwili. Hata hivyo, ulaji wa nyama ya mbwa yenyewe hautakuwa kinyume cha sheria.
Sheria hiyo mpya itaanza kutumika katika muda wa miaka mitatu, na kuwapa wakulima na wamiliki wa migahawa muda wa kutafuta vyanzo mbadala vya ajira na mapato. Watalazimika kuwasilisha mpango wa kumaliza biashara zao kwa mamlaka zao za mitaa.
Serikali imeahidi kusaidia kikamilifu wakulima wa nyama ya mbwa, wachinjaji na wamiliki wa mikahawa, ambao biashara zao zitalazimika kufungwa, ingawa maelezo ya iwapo fidia itatolewa bado hayajafanyiwa kazi.
Kulingana na takwimu za serikali, Korea Kusini ilikuwa na karibu mikahawa 1,600 ya nyama ya mbwa na mashamba 1,150 ya mbwa mnamo 2023.
Kitoweo cha nyama ya mbwa, kinachoitwa "boshintang", kinachukuliwa kuwa kitamu miongoni mwa baadhi ya Wakorea Kusini wenye umri wa juu, lakini nyama hiyo si maarufu tena kwa vijana.
Korea Kusini yapitisha sheria ya kupiga marufuku biashara ya nyama ya mbwa

Chanzo cha picha, Reuters
Korea Kusini imepitisha sheria mpya, ambayo inalenga kukomesha uchinjaji na uuzaji wa mbwa kwa ajili ya nyama yao ifikapo 2027.
Sheria hiyo inalenga kukomesha tabia ya karne nyingi ya kula nyama ya mbwa.
Nyama ya mbwa imekosa kupendwa na watu wengikatika miongo michache iliyopita. Vijana hasa huiepuka.
Chini ya sheria, kufuga au kuchinja mbwa kwa ajili ya kuliwa kutapigwa marufuku, vile vile kusambaza au kuuza nyama ya mbwa. Wale watakaopatikana na hatia ya kufanya hivyo wanaweza kupelekwa jela.
Wale wanaochinja mbwa wanawezakufungwa jela miaka mitatu, huku wale wanaofuga mbwa kwa ajili ya nyama au kuuza nyama ya mbwa wanaweza kutumikia kifungo cha miaka miwili. Hata hivyo, ulaji wa nyama ya mbwa yenyewe hautakuwa kinyume cha sheria.
Sheria hiyo mpya itaanza kutumika katika muda wa miaka mitatu, na kuwapa wakulima na wamiliki wa migahawa muda wa kutafuta vyanzo mbadala vya ajira na mapato. Watalazimika kuwasilisha mpango wa kumaliza biashara zao kwa mamlaka zao za mitaa.
Serikali imeahidi kusaidia kikamilifu wakulima wa nyama ya mbwa, wachinjaji na wamiliki wa mikahawa, ambao biashara zao zitalazimika kufungwa, ingawa maelezo ya iwapo fidia itatolewa bado hayajafanyiwa kazi.
Kulingana na takwimu za serikali, Korea Kusini ilikuwa na karibu mikahawa 1,600 ya nyama ya mbwa na mashamba 1,150 ya mbwa mnamo 2023.
Kitoweo cha nyama ya mbwa, kinachoitwa "boshintang", kinachukuliwa kuwa kitamu miongoni mwa baadhi ya Wakorea Kusini wenye umri mkubwa, lakini nyama hiyo si maarufu tena kwa vijana.
Idadi ya juu zaidi ya raia waliojeruhiwa na vilipuzi ilirekodiwa mwaka wa 2023

Chanzo cha picha, AFP
Mwaka jana ulishuhudia idadi kubwa zaidi ya majeruhi wa raia waliouawa au kujeruhiwa na vilipuzi katika zaidi ya muongo mmoja, kulingana na utafiti mpya.
Shirika la kutoa misaada kuhusu Vurugu za Kivita (AOAV) lenye makao yake makuu nchini Uingereza (AOAV) lilirekodi ongezeko la asilimia 122 la vifo vya raia vilivyosababishwa na vilipuzi mwaka wa 2023.
Kupanda huko kumechangiwa zaidi na vita vinavyopiganwa kati ya Israel na Hamas huko Gaza.
Migogoro ya Ukraine, Sudan, Myanmar na Somalia pia ilichangia.
Utafiti wa shirika la hisani lenye makao yake London unatumiwa na majukwaa ya kimataifa kama vile UN.Pia imewasilisha ushahidi wake kwa Bunge la Uingereza.
Mnamo 2023, AOAV iligundua takriban matukio 7,307 ya milipuko kote ulimwenguni, kutoka 4,322 yaliyorekodiwa mwaka uliopita.
Mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya takriban raia 15,305, na hivyo kuchangia kuongezeka kwa 122% kutoka 2022. Makumi ya maelfu ya wengine walijeruhiwa.
AOAV inaelezea vita vya Israeli huko Gaza kama "sababu kubwa ya ongezeko kubwa kama hilo" la vifo vya raia, ikichukua karibu theluthi moja ya jumla ya ulimwengu.
Ilirekodi matukio 920 ya matumizi ya silaha za milipuko huko Gaza, na kusababisha watu 9,334 kuuawa.Hiyo ni chini kuliko makadirio mengine.
Thierry Henry asema alikuwa na msongo wa mawazo katika maisha yake yote ya uchezaji

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambulizi wa zamani wa Arsenal Thierry Henry anasema "lazima awe alikuwa na huzuni" wakati wa uchezaji wake.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 46 alifunga rekodi ya klabu mabao 228 katika michezo 377 akiwa na The Gunners na kushinda Kombe la Dunia mwaka 1998 na Euro 2000 akiwa na Ufaransa.
"Katika kazi yangu yote, na tangu nilipozaliwa, lazima ningekuwa katika msongo wa mawazo," Henry aliambia Diary of a CEO podcast
"Je! nilijua? Hapana. Je! nilifanya kitu juu yake? Hapana. Lakini nilijizoea kwa njia fulani."
Henry sasa ni mkufunzi wa Vijana wa U-21 wa Ufaransa, pia alifanya kazi kwenye ben chi Ła ukocha wa Ubelgiji na aliisimamia Monaco kabla ya kuchukua mikoba ya Montreal Impact mwishoni mwa 2019.
Anasema kulikuwa na kipindi mapema katika janga la corona ambapo "alikuwa akilia karibu kila siku".
"Lazima uweke mguu mmoja [mbele] na mwingine na utembee," alisema.“Hivyo ndivyo nilivyoambiwa tangu nikiwa mdogo.
"Sikuacha kutembea - [kama ningefanya] basi labda ningetambua [kuhusu matatizo ya kiafya]. Wakati wa Covid - Niliacha kutembea. Sikuweza. Kisha unaanza kutambua."
Mshambulizi huyo wa zamani wa Juventus, Monaco na Barcelona aliongeza: "Nilikuwa peke yangu huko Montreal, na kutoweza kuwaona watoto wangu kwa mwaka mmoja ilikuwa ngumu.
"Machozi yalikuwa yanatirirka . Mbona sijui, lakini labda walikuwa huko kwa muda mrefu sana."
Henry alisema uhusiano wake na babake, ambaye anasema alikuwa mkosoaji wa uchezaji wake, unaweza kuwa na athari kwake.
Alisema baba yake "alikuwa na mani yen makali sana nyakati fulani kuhusu jinsi nilivyokuwa mchezaji".
"Kama mvulana mdogo ilikuwa daima 'hukufanya vizuri'," alisema.
"Kwa hivyo ni wazi unaposikia kwamba mara nyingi zaidi kuliko sivyo, hiyo ndiyo itasalia."
Franz Beckenbauer: Gwiji wa soka wa Ujerumani afariki akiwa na umri wa miaka 78

Chanzo cha picha, Getty Images
Gwiji wa Ujerumani Franz Beckenbauer, anayetambulika kama mmoja wa wachezaji nguli wa kandanda, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 78.
Alishinda Kombe la Dunia kama nahodha wa Ujerumani Magharibi mnamo 1974 na alinyanyua tena kombe kama meneja mnamo 1990.
Beckenbauer, ambaye kimsingi alikuwa mlinzi, aliichezea Bayern Munich mara 582 na kushinda ligi kuu ya Ujerumani akiwa mchezaji na meneja.
Aliitwa 'Der Kaiser', kama mchezaji pia alishinda Ubingwa wa Uropa mnamo 1972, na pia Ballon d'Or mara mbili.
Taarifa kutoka kwa familia yake kwa shirika la habari la Ujerumani DPA ilisema: "Ni kwa huzuni kubwa kwamba tunatangaza kwamba mume wangu na baba yetu, Franz Beckenbauer, alifariki dunia kwa amani usingizini jana, Jumapili, akiwa amezungukwa na familia yake.
"Tunaomba mturuhusu kuomboleza kwa farègha na tujizuie kuuliza maswali yoyote."
Afisa wa jeshi la wanamaji la Marekani afungwa jela kwa kuwa jasusi wa China

Chanzo cha picha, Getty Images
Afisa wa jeshi la wanamaji wa Marekani aliyekiri kutoa taarifa nyeti za kijeshi kwa China amefungwa jela kwa zaidi ya miaka miwili.
Wenheng Zhao, mwenye umri wa miaka 26, alikiri hatia mwezi Oktoba kwa kupeana taarifa kwa majasusi wa China kwa rushwa.
Bw Zhao alikuwa afisa mdogo anayefanya kazi katika kituo cha wanamaji cha California.
Alipitisha habari kuhusu mazoezi ya kijeshi, maagizo ya operesheni na miundombinu muhimu Kuanzia 2021 hadi 2023, maafisa wa Amerika walisema.
Hasa, alitoa taarifa kuhusu mazoezi makubwa ya jeshila Wanamaji la Marekani katika eneo la Indo-Pacific, pamoja na michoro ya umeme na michoro ya mfumo wa rada ulioko kwenye kambi ya Marekani kwenye kisiwa cha Japan cha Okinawa.
Kambi ya Jeshi la Wanamaji la Marekani huko Okinawa ni muhimu kwa shughuli zake barani Asia. Marekani imefanya kile inachokiita eneo la "Indo-Pasifiki" kuwa kipaumbele kikuu cha usalama, na katika miaka ya hivi karibuni imefanya kazi katika kuimarisha ushirikiano huko ili kukabiliana na uwepo wa kijeshi wa China.
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo Jumanne tarehe tisa Januari 2024
