Kwa nini mpango wa kuipa Ethiopia njia ya Bahari ya Sham ni muhimu

 Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anaelezea hitaji la nchi yake la kufikia bandari zaidi kama suala "lililopo".

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anaelezea hitaji la nchi yake la kufikia bandari zaidi kama suala "muhimu".
    • Author, Kalkidan Yibeltal, Esther Kahumbi na Aaron Akinyemi
    • Nafasi, Addis Ababa & London

Somalia imepinga vikali mpango uliopendekezwa ambao utaipa Ethiopia ufikiaji wa bandari muhimu katika eneo la Somaliland linalotaka kujitenga.

Katika hatua ya kukabiliana na mkataba wa maelewano (MOU) kati ya Ethiopia na Somaliland, nchi hiyo imemwita nyumbani balozi wake kutoka Ethiopia.

Msemaji wa serikali alisema anapinga vikali pendekezo linalokiuka mamlaka yake na uadilifu wa eneo - Somalia inaichukulia Somaliland kama sehemu ya himaya yake.

Waziri Mkuu wa Somalia Hamza Abdi Barre alisema: "Ninataka kuwasihi watu wa Somalia watulie, nataka kuwahakikishia kwamba tumejitolea kuilinda nchi yetu. Hakuna sehemu ya ardhi yetu, bahari yetu na hewa yetu inayoweza kukiukwa, na tutaitetea kwa kila njia ya kisheria. Na nina hakika kwa msaada wa watu wetu iwe kaskazini au kusini tunaweza kuilinda nchi yetu”

Somaliland ilijitenga kutoka Somalia mwaka 1991 lakini haitambuliwi kimataifa kama taifa huru, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika. Kwa hiyo hatua yoyote kuelekea kutambuliwa rasmi- hasa kutoka kwa taifa lenye ushawishi mkubwa wa AU kama Ethiopia - inaweza kuwa muhimu kwa mustakabali wake.

Ikumbukwe kuwa hadi sasa, hakuna mpango wowote ambao umerasimishwa kisheria. Hakuna mkataba. Ingawa maafisa wa serikali ya Ethiopia walipendekeza kwa waandishi wa habari kuwa inaweza kukamilika mwezi ujao.

Malori yaliyokuwa yamepakia mgao wa chakula kutoka kwa meli ya Thorco Liva yanaondoka kwenye bandari ya Berbera huko Somaliland.

Hakuna shaka mpango wowote ungeipa Ethiopia ufikiaji wa kona ya kimkakati na yenye faida kubwa duniani. Hatua hii inaweza kumaanisha nini kwa majirani zake?

 Malori yaliyokuwa yamepakia mgao wa chakula kutoka kwa meli ya Thorco Liva yanaondoka kwenye bandari ya Berbera huko Somaliland

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Malori yaliyokuwa yamepakia mgao wa chakula kutoka kwa meli ya Thorco Liva yanaondoka kwenye bandari ya Berbera huko Somaliland

Ethiopia

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ufikiaji wa kilomita 20 tu za ukanda wa pwani huenda usionekane kama jambo kubwa lakini kwa Ethiopia isiyo na bandari, ufikiaji wa bandari ni muhimu kwa mustakabali wake wa kifedha. Ni nchi yenye watu wengi zaidi duniani ambayo haina ukanda wa pwani - na hii inatoa changamoto za wazi kwa ukuaji.

Zaidi ya 95% ya biashara ya kimataifa ya Ethiopia inategemea nchi jirani ya Djibouti, ambayo ina 31km ya ukanda wa pwani.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed anaelezea hitaji la nchi yake la kupata ufikiaji zaidi wa bandari kama suala "muhimu", na alisema katika hotuba ya runinga mnamo Oktoba mwaka jana kwamba bandari ya Bahari Nyekundu ni muhimu kwa raia wake milioni 120 kujikwamua kutoka "gerezani ya kijiografia"

Biashara inaweza isiwe sababu pekee. Nchi hiyo ilikuwa na ushawishi baharini wakati ilipokuwa na bandari mbili - Massawa na Assab. Lakini Ethiopia ilipoteza maeneo hayo pamoja na maeneo mengine ya pwani wakati Eritrea ilipojitenga na kuunda nchi mpya mwaka 1993.

Kulingana na Balozi wa zamani wa Marekani nchini Ethiopia David Shinn, sababu ya msingi ya bandari ya Bahari Nyekundu ya Ethiopia MOU na Somaliland ni kuanzisha kituo cha wanamaji mahali fulani katika Bahari Nyekundu au Ghuba ya Aden.

Aliambia kipindi cha Newsday cha BBC: "Somaliland imesema itakodisha kilomita 20 za ufuo wa pwani kando ya Ghuba ya Aden ili Ethiopia iweze kuanzisha kituo kama hicho. Pia huenda ingetumika, au angalau kuruhusu Ethiopia kutumia bandari ya Berbera, ambayo ni bandari muhimu ya Somaliland, kwa matumizi ya kuagiza na kuuza bidhaa zake nje ya nchi. Ingawa sioni hiyo kama sababu kuu ya hatua hii. Nadhani inahusiana zaidi na hamu ya kuwa na kituo cha jeshi majini.

Michael Shurkin, mwenzake wa Kituo cha Afrika cha Baraza la Atlantiki: "Ni hatari iliyohesabiwa kwa Ethiopia, na ambayo ina mambo ya kweli. Ethiopia inatamani sana kupata ufikiaji mkubwa wa bahari, na kwa njia hii inaweza kuwa na mwelekeo mdogo wa kuanzisha vita na Eritrea. Zaidi ya hayo inaipa Somaliland kutambuliwa inavyostahili. Bila shaka, pia inaikasirisha Somalia, lakini hiyo ni hatari kidogo kuliko makabiliano na Eritrea."

Ali Abdi Elmi akinywa maziwa ya ngamia, nje kidogo ya mji wa Hargeisa, Somaliland.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ali Abdi Elmi akinywa maziwa ya ngamia, nje kidogo ya mji wa Hargeisa, Somaliland.

Somalia

Wadau wakuu wa kisiasa wa Somalia wanaamini kuwa hatua hiyo inaweza kutishia uthabiti wa eneo hilo la Pembe ya Afrika. Inakuja siku chache baada ya Somalia na Somaliland kufikia mwafaka wa kuanza tena mazungumzo yenye lengo la kutatua mvutano wa kisiasa. Mjumbe maalum wa Somalia katika Somaliland Abdikarim Hussein Guled alisema mpango uliopendekezwa unaonyesha "kutozingatia waziwazi kwa Ethiopia kanuni za kimataifa" na kufichua maendeleo kati ya Mogadishu na mji mkuu wa Somaliland Hargeisa.

Rais wa zamani wa Somalia Mohamed Farmaajo alisema katika taarifa yake kwenye mtandao wa kijamii wa X, MOU ni "kitisho kikubwa kwa Somalia na Afrika nzima". Aliongeza: "Heshima kwa mamlaka na uadilifu wa eneo ndio nguzo ya utulivu wa kikanda na ushirikiano wa nchi mbili. Serikali ya Somalia lazima ijibu ipasavyo.”

Mohamed Mubarak mwenyekiti wa zamani wa Taasisi ya Hiraal, mdau wa masuala ya usalama katika Pembe ya Afrika alisema kuna maelfu ya wanajeshi wa Ethiopia kusini mwa Somalia. Ikiwa uhusiano utazidi kuwa mbaya, Ethiopia inaweza kujiondoa, na hivyo kuvuruga hali ya usalama sehemu hiyo.

"Abiy amekuwa akisema kwa miezi mingi kwamba angeiwezesha Ethiopia kupata bahari," Bw Mubarak alisema. "Hicho ndicho amefanya [uwezekano] na mpango huu. Yuko tayari kufanya chochote kinachohitajika bila kujali athari zake kwa amani na utulivu wa eneo hilo.

Ramani

Kenya

Miongoni mwa nchi ambazo Ethiopia imekuwa ikifanya mazungumzo nazo ili kufikia upatikanaji wa bandari yake ni Kenya.

Mnamo Agosti 2023, maafisa wa Ethiopia walitembelea bandari ya Lamu. Bandari ni sehemu ya mradi wa usafiri wa kikanda kati ya Ethiopia, Kenya, na Sudan Kusini uitwao LAPSSET.

Kupitia Lamu, Kenya ilitarajiwa kupunguza sehemu ya Djibouti ya mahitaji ya ndani ya Ethiopia kwa 15% kulingana na Ripoti ya Benki ya Dunia.

Kwa hivyo mkataba wowote mpya wa bandari na Somaliland au kuchelewa kupanua Lamu kunaweza kuathiri Kenya kwa kiwango fulani.

Mnamo 2020, Somalia ilikata uhusiano na Kenya kwa muda mfupi baada ya kuwa mwenyeji wa kiongozi wa Somaliland Muse Bihi. Kenya inasema kwamba inatambua Somaliland kama serikali ya kikanda ndani ya Somalia, lakini sawa na Ethiopia, Kenya ina ubalozi wake mdogo mjini Hargeisa.

Misri

Misri ambayo ni mhusika mkuu katika pwani ya Bahari ya Sham ina idadi kubwa ya bandari zikiwemo bandari 8 za kibiashara na bandari tano za mafuta, madini na watalii.

Kumekuwa na wasiwa wa kikanda kuhusu muda ambao Waziri Mkuu Bw. Abiy Ahmed yuko tayari kwenda kupata ufikiaji wa Bahari ya Sham. Amenukuliwa akielezea ufikiaji kama "suala linalowezekana".

Wachambuzi wanasema maoni yake kuhusu hili hayana tofauti sana na yale alipoamua kuendelea na ujenzi wa Bwawa la Kuu la Ethiopia(Gerd).

Mkataba wa 1929 uliwapa Misri na Sudan haki kwa karibu maji yote ya Mto Nile lakini Ethiopia na Misri bado hazijakubaliana juu ya sheria za uendeshaji wa bwawa hilo.

Njia ya kupitia Berbera inaweza kuifanya Ethiopia kujiunga na mataifa mengi (pamoja na Misri,) ambayo yamekuza uchumi wao kwa kiasi kikubwa kutokana na kufikia Bahari ya Sham

 Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh akizungumza katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa mjini Dubai

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh akizungumza katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa mjini Dubai

Djibouti

Taifa hilo dogo la Kiafrika ni lango la kuelekea kwenye Mfereji wa Suez, mojawapo ya njia zenye shughuli nyingi zaidi za meli duniani.

Bandari yake ya thamani ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wake, ikitoa chanzo kikubwa cha mapato na ajira katika nchi nyingine isiyo na bandari.

Kama lango kuu la biashara kwa jirani yake mkubwa mpango wowote wa biashara zaidi kupitia Berbera unaweza kuhatarisha hali yake.

China

China inaweza pia kuwa na nia ya dhati katika mpango wowote - Somaliland imepokea msaada kutoka kwa Taiwan na kwa upande wake China inaunga mkono Somalia.

Somaliland na Taiwan zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 2020 katika hatua iliyowakasirisha majirani zao wakubwa.

Meneo hayo mawili yanayotaka kujitenga hayatambuliki kimataifa - Somalia na China - zinasisitiza kuwa ni sehemu ya maeneo yao.

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi