Msanii wa muda
mrefu kutoka nchini Marekani Snoop Dogg, ambaye amejitengenezea umaarufu kutokana
na uvutaji wake wa bangi amesema kwamba ameacha kuvuta bangi
Msanii huyo wa muziki
wa Pop, ambaye jina lake halisi ni Calvin Broadus, alitoa tangazo hilo la
kushtukiza kwenye mitandao ya kijamii.
"Baada ya
kufikiria na kufanya majadiliano mengi na familia yangu, nimeamua kuacha kuvuta
sigara. Tafadhali heshimu faragha yangu kwa wakati huu," alichapisha
kwenye mtandao wake wa Instagram,
external na X.,
Hakutaja ni aina
gani ya uvutaji anayoacha, au hata ikiwa alikuwa mkweli.
Baadhi ya
mashabiki walikisia kuwa chapisho hilo lilikuwa miongoni mwa harakati zake
kukuza kampuni yake ya bangi Leafs by Snoop
Wengine walijibu
kwa kutoamini.
"Leo sio
siku ya Aprili Fools Snoop," alisema mmoja.
"Snoop bila
moshi ni kama ardhi bila maji," aliongeza mwingine.
Ro Marley, mtoto
wa gwiji wa reggae Bob Marley, alitoa maoni: "Hakuna BBQ tena kwa
uncle's... grill imezimwa kwa msimu huu."
Matumizi ya bangi ya Snoop yamethibitishwa vyema katika
muziki wake na mahojiano.
Rapa huyo mwenye
umri wa miaka 52, alitamba kwa mara ya kwanza kwenye albamu ya Dr Dre ya mwaka
1992, The Chronic, ambayo jina lake ni jina la mzaha la bangi ya hali ya juu.
Kwa miaka mingi,
maneno yake yamekuwa na marejeleo mengi ya tabia hiyo.
"Tutavuta
moshi kidogo," alirap kwenye wimbo wake wa pekee wa Gin And Juice.
Ushirikiano wa Dr Dre The Next Episode - ambao ulifungua onyesho wakati wa
mapumziko ya mechi ya Super Bowl mnamo
2022 - ulibeba maoni: "Vuta bangi kila siku."
Mnamo 2013,
akizungumza na jarida la GQ, msanii huyo alisema alikuwa akivuta bangi 80 kwa
siku.
Alianzisha Leafs
By Snoop miaka miwili baadaye. Kampuni hiyo ina utaalam wa kutengeneza aina zake za bangi.