Vita vya Ukraine: Lengo la Wagner PMC nchini Belarus ni kuivuruga NATO mashariki - Poland

Chanzo cha picha, VOENTV/BELARUSIAN DEFENCE MINISTRY VIA REUTERS
Mamluki wa PMC ya Urusi "Wagner" walihamishiwa Belarus ili kuyumbisha upande harakati za NATO upande wa mashariki, amesema Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki.
Aliongeza kuwa kulingana na makadirio ya Poland na Lithuania ambayo ni jirani, kuna mamluki wapatao 4,000 kutoka kundi la Wagner PMC nchini Belarus, ambao wanaweza kutumiwa kwa mashambulizi.
"Lazima tujitayarishe kwa ukweli kwamba idadi za chokochoko zitaongezeka," Morawiecki alisema baada ya kukutana na Rais wa Lithuania Gitanas Nausėda.
Siku ya Jumamosi, Morawiecki alisema kuwa zaidi ya mamluki 100 wa Wagner walioko Belarus walihamishiwa katika eneo la ukanda wa Suwalki (ukanda wa ardhi kati ya Belarusi na mkoa wa Kaliningrad, karibu kilomita 100, kwenye mpaka kati ya Poland na Lithuania.
"Kundi la Wagner ni hatari sana, na vitengo vya kundi hili vinapelekwa kwenye eneo la mashariki linalodhibitiwa na NATO ili kuliyumbisha usalama," Morawiecki alisema.
Belarus inakanusha kuwepo kwa mipango hiyo. Kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko alisema siku chache zilizopita kwamba Belarusi "haihitaji" ukanda wa Suwalki kwa miaka elfu: "Hatuendi kwenye ukanda huu."
Baada ya kuonekana kwa kambi za mamluki za Wagner kwenye eneo la Belarus, viongozi wa Kipolishi waliamua kuimarisha vikosi vya wanajeshi wao kwenye mpaka wa mashariki, wakipeleka askari zaidi ya 1,000 kwenye mpaka wao wa mashariki.
Vita vya Ukraine: Mengi zaidi:
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine

























