Waziri wa Ukraine ahimiza Afrika kuwa na msimamo katika vita vya Urusi

Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba amezitaka nchi za Afrika kukomesha msimamo wao wa kutoegemea upande wowote kuhusu uvamizi wa Urusi wakati akianza ziara ya pili barani humo.

Moja kwa moja

  1. Marais Samia na Museveni wazindua mradi wa kimkakati wa umeme

    .

    Chanzo cha picha, STATE HOUSE UGANDA

    Maelezo ya picha, Picha kutoka maktaba

    Marais wa nchi mbili za Tanzania na Uganda wamezindua mradi kimakakati wa umeme Afrika Mashariki ujulikanao kama Kikagati Murongo Hydropower Plant, wenye uwezo wa kuzalisha megawati 14 ambazo zitanufaisha nchi hizo mbili.

    Kulingana na gazeti la mwananchi, mradi huo unaotokana na maji ya Mto Kagera, umegharimu dola za Kimarekani milioni 56, na umezinduliwa wilayani Isingiro nchini Uganda na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishirikiana na Rais wa Uganda, Yoweli Kaguta Museveni.

    Mmoja wa viongozi waandamizi katika wizara zinazosimamia nishati kwenye nchi hizo, amesema mradi huo ulianza kutekelezwa 2017 na kukamilika 2022 na wannachi wa pande zote mbili wananufaika kwa kupata megawati 7 kila mmoja.

  2. Vumbi la 'shetani' lanaswa kwenye kamera Marekani

    Maelezo ya video, Dust devil caught on camera in US city

    Mtumiaji mmoja wa Twitter amenasa vumbi lisilo la kawaida aliloliita ‘la shetani’ likizunguka tena kwa kasi mno katika eneo la Frederick, Maryland.

    Katika mtandao wa kijamii wa Twitter,, mtu huyo alidai, 'ameona kimbunga'.

  3. Wapinzani wa Sudan wanashutumiana kwa ukiukaji wa usitishaji mapigano

    .

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Moshi ulionekana ukipanda kutoka kwa majengo mjini Khartoum siku ya Jumatano

    Pande zinazozozana nchini Sudan zimeshutumiana kwa kukiuka makubaliano ya hivi punde ya kusitisha mapigano, ambayo sasa ni siku ya tatu.

    Makubaliano hayo ya wiki moja yalikiukwa dakika chache baada ya kuanza kutekelezwa Jumatatu usiku, huku wakaazi wa mji mkuu, Khartoum wakishuhudia mashambulizi ya anga na mizinga.

    Mapigano ya hapa na pale kati ya jeshi na kikosi cha Rapid Support Forces (RSF), yameendelea hadi Alhamisi.

    .

    Chanzo cha picha, AFP

    Hatua hiyo ilikuwa imesaidia baadhi ya wakaazi kutoka nje ya nyumba zao kutafuta chakula, maji na matibabu.

    Mapigano hayo yamezidisha mzozo uliopo wa kibinadamu, na kuwalazimu zaidi ya watu milioni 1.3 kutoroka na kutishia kuyumbisha eneo hilo.

    Soma zaidi:

  4. Sudan Kusini inaweza ikaathirika ikiwa vita vya Sudan vitaendelea – UN

    .

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Mapigano kati ya vikosi hasimu nchini Sudan sasa yamefikia wiki ya sita

    Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (Unmiss) umeonya kuwa nchi hiyo inaweza ikaathirika iwapo vita katika taifa jirani la Sudan vitaendelea.

    Nicholas Haysom, mkuu wa Unmiss, aliwaambia waandishi wa habari katika mji mkuu, Juba, kwamba Sudan Kusini "itaathirika kutokana na kile kinachotokea Sudan" akibainisha kuwa athari mbaya za vita zitashuhudiwa nje ya nchi hiyo.

    Alisema kukatizwa kwa bomba la mafuta la Sudan Kusini hadi Sudan - ambapo nchi hiyo isiyo na bandari inasafirisha mafuta yake yote ghafi - kutakuwa na athari za moja kwa moja.

    Alisema Sudan Kusini na raia wake katika "kujikimu" wataathirika "kwa sababu 90% ya huduma na mishahara yote yanatokana na pesa za mafuta".

    "Kwa hiyo katika suala hilo, bila shaka tungetaka kusema- tena kwa sauti, kwa nguvu, mara kwa mara - kwamba vita lazima vifike mwisho," Bw Haysom aliongeza.

    Mapigano kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha Rapid Support Forces paramilitary (RFS), sasa yameingia katika wiki yake ya sita, na yamesababisha karibu watu milioni moja kutoroka makwao, kulingana na Umoja wa Mataifa.

    Idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini ambao wametoroka vita na kurejea nyumbani imezidi 70,000, kulingana na Unmiss

  5. Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda 'aliyesakwa sana' akamatwa Afrika Kusini

    .

    Chanzo cha picha, International Residual Mechanism for Criminal Tribunals

    Maelezo ya picha, Fulgence Kayishema amekuwa akitoroka tangu 2001 alipofunguliwa mashtaka na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda

    Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda 'anayesakwa sana' akamatwa SA

    Fulgence Kayishema, mmoja wa washukiwa wanaosakwa sana wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya halaiki ya Rwanda mwaka 1994, amekamatwa katika mji wa Paarl nchini Afrika Kusini baada ya kutoroka kwa zaidi ya miaka 20.

    .

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Fulgence Kayishema (chini kushoto) alikuwa mmoja wa watoro wanaosakwa sana duniani.

    Alizuiliwa Jumatano mchana katika operesheni ya pamoja kati ya mamlaka ya Afrika Kusini na timu ya Umoja wa Mataifa ambayo inawasaka watoro waliosalia.

    Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia kesi bora za uhalifu wa kivita kwa Rwanda na Yugoslavia, inayojulikana kama International Residual Mechanism for Criminal Tribunals' (IRMCT), Kayishema alikuwa mmoja wa watu waliotoroka mauaji ya kimbari waliokuwa wakitafutwa zaidi duniani.

    Alishtakiwa mwaka 2001 na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) na kushtakiwa kwa mauaji ya halaiki, kushiriki katika mauaji ya halaiki, kula njama ya kutekeleza mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu kwa mauaji na uhalifu mwingine.

    Anadaiwa kupanga mauaji ya takriban Watutsi 2,000 - wanawake, wanaume, watoto na wazee - katika kanisa moja katika wilaya ya Kivumu, ambapo alikuwa inspekta wa polisi.

    Alituhumiwa kushiriki moja kwa moja katika kupanga na kutekeleza mauaji hayo, ikiwa ni pamoja na kununua na kusambaza petroli ili kuchoma kanisa hilo pamoja na waliokuwa wanatafuta hifadhi humo.

    "Hili liliposhindikana, Kayishema na wengine walitumia tingatinga kuangusha kanisa, kuwazika na kuwaua wakimbizi waliokuwemo ndani yake.

    Kayishema na wengine kisha wakasimamia uhamishaji wa maiti kutoka katika viwanja vya kanisa hadi kwenye makaburi ya pamoja kwa takriban siku mbili zilizofuata," taarifa ya IRMCT imesema.

    Zawadi ya hadi $5m ilikuwa imetolewa na Marekani kwa kukamatwa kwake.

    Mshukiwa ambaye amekuwa akitoroka tangu kufunguliwa mashtaka, anatazamiwa kufikishwa katika mahakama ya Cape Town siku ya Ijumaa, ripoti zinasema.

    Takriban Watutsi 800,000 wa kabila na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa na Wahutu wenye msimamo mkali katika muda wa siku 100 mwaka 1994.

    Soma zaidi:

  6. Waziri wa Ukraine ahimiza Afrika kuwa na msimamo katika vita vya Urusi

    Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alifanya mazungumzo nchini Ethiopia

    Chanzo cha picha, Dmytro Kuleba/Twitter

    Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro Kuleba amezitaka nchi za Afrika kukomesha msimamo wao wa kutoegemea upande wowote kuhusu uvamizi wa Urusi wakati akianza ziara ya pili barani humo.

    "Kwa kutoegemea upande wowote dhidi ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, unaonyesha kutoegemea upande wowote kwa ukiukaji wa mipaka na uhalifu mkubwa ambao unaweza kutokea karibu na wewe, ikiwa hautatokea kusaidia," alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa.

    Siku ya Jumatano. Bw Kuleba hata hivyo alibainisha kwamba "uhusiano wa Ukraine na nchi za Afrika haukuzingatiwa ipasavyo katika sera yetu ya mambo ya nje kwa miaka mingi na tulipoteza mengi".

    Alifanya mazungumzo na Waziri Mkuu Abiy Ahmed, mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki na Rais wa Comoro Azali Assoumani, ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa AU.

    Nchi sita za Afrika - zikiongozwa na Afrika Kusini - zinaongoza mpango wa amani kati ya Moscow na Kyiv kwani vita vinaathiri vibaya usambazaji wa nafaka na mbolea katika eneo hilo.

    Wakati nchi nyingi zimekuwa zikilaani mara kwa mara uvamizi wa Urusi wakati wa mijadala katika Umoja wa Mataifa, kujiepusha na nchi mbalimbali za Afrika kumezua ukosoaji wa Magharibi.

    Ziara ya Bw Kuleba barani Afrika pia inajumuisha ziara za Morocco na Rwanda.

    Alifanya safari yake ya kwanza barani humo Oktoba mwaka jana alipotembelea Senegal, Ivory Coast, Ghana na Kenya.

    Pia unaweza kusoma

  7. Zimbabwe yashutumiwa kwa kuwaachilia 'wabakaji hatari' kwa msamaha

    Magereza Zimbabwe

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Muungano wa upinzani nchini Zimbabwe Citizens Coalition for Change (CCC) has umedai kuwa zaidi ya wafungwa 4,000 walioachiwa huru kwa msamaha wa rais wiki iliyopita wanajumuisha wabakaji watoto.

    Rais Emmerson Mnangagwa aliwasamehe wafungwa waliotoka katika magereza 47 ya nchi hiyo katika jaribio la kupunguza msongamano.

    Mamlaka za magereza hata hivyo zilisema, ubakaji ni miongoni mwa makosa ambayo hayakujumuishwa katika msamaha huo.

    Video zilizosambazwa mtandaoni zilionyesha kile ambacho vyombo vya habari vya nchini humo vilisema ni wabakaji wakisherehekea uhuru wao huku baadhi yao wakisemekana kuwa wametumikia hukumu yao kwa chini ya mwaka mmoja.

    CCC katika taarifa yake siku ya Jumatano ilisema "haikuwa sawa kuwaachilia wahalifu hatari na ambao hawajarekebishwa kujumuika tena na jamii" kabla ya kuwaarifu au kuwatayarisha kisaikolojia waathiriwa wa ubakaji.

    "Kumwachilia mbakaji ambaye hajarekebisha maadili yake katika jamii bila ulinzi wowote wa kuwalinda waathiriwa kunahatarisha wanawake na wasichana na kamwe hakuwezi kuwa na sababu za msingi katika jamii ya kidemokrasia," msemaji wa CCC Fadzayi Mahere alisema.

    Baadhi ya Wazimbabwe kwenye mitandao ya kijamii pia wametaka uamuzi huo kubatilishwa kwani unawaweka wanawake katika hatari.

    Mwanahabari mashuhuri wa uchunguzi Hopewell Chin’ono alisema msamaha "kamwe hautolewi kwa wabakaji au watu ambao wamefanya uhalifu wa kikatili".

    Bw Chin’ono, mkosoaji wa serikali, alisema wanawake wa Zimbabwe hawatakuwa salama kufuatia msamaha huo.

    Mamlaka za Zimbabwe bado hazijatoa maoni yoyote kuhusu madai hayo.

  8. IMF imeidhinisha mkopo wa dola bilioni 3.5 kwa Ivory Coast

    Shirika la fedha duniani IMF, limeidhinisha mkopo wa $3.5bn kwa Ivory Coast kukabiliana na changamoto za kifedha na kusaidia mabadiliko ya kiuchumi.

    Nchi hiyo ya Afrika Magharibi itapokea karibu $500m mara moja.

    Fedha zaidi zitategemea Ivory Coast kufanya mabadiliko ya kimuundo kwa uchumi wake.

    IMF inasema mkopo huo utasaidia nchi hiyo kukabiliana na majanga ya Covid, uimarishaji wa fedha duniani na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

  9. China yakanusha kuwa ilidukua mashirika ya serikali ya Kenya

    th

    Chanzo cha picha, Kenya presidency/Twitter

    Maelezo ya picha, Shirika la habari la Reuters lilikuwa limeripoti kuwa mashambulizi ya mtandaoni ya miaka mingi yalianza mwaka wa 2019 wakati Wachina walipoanza kufungia Kenya mikopo.

    Ubalozi wa China nchini Kenya umekanusha ripoti ya shirika la habari la Reuters kwamba wadukuzi kutoka taifa hilo la Asia walishambulia mashirika muhimu ya serikali jijini Nairobi, ikiwa ni pamoja na ofisi ya rais, ili kutathmini iwapo nchi hiyo italipa mabilioni ya dola inayodaiwa na Beijing.

    Shirika la habari la Reuters lilikuwa limeripoti kuwa mashambulizi ya mtandaoni ya miaka mingi yalianza mwaka wa 2019 wakati Wachina walipoanza kufunga njia za mkopo kwa Kenya huku matatizo ya deni yakianza kuonekana.

    Lakini katika taarifa siku ya Jumatano, ubalozi wa China ulisema ripoti hiyo "ni potofu na upuuzi mtupu".

    "Udukuzi ni tishio la kawaida kwa nchi zote na China pia ni mwathirika wa mashambulizi ya mtandao," iliongeza.

    Ubalozi unasema ni suala nyeti sana la kisiasa kulaumu serikali fulani kwa shambulio la mtandao bila ushahidi thabiti.

    Inasema uhusiano kati ya Kenya na China unatokana na kuheshimiana.

    Kenya imeripotiwa kupunguza kukopa kutoka China na kufikia Machi ilidaiwa na nchi hiyo ya kusini-mashariki mwa Asia $6.31bn (£5.8bn).

    Pia uanweza kusoma:

  10. Lishe inayotokana na mimea ni nzuri kwa moyo

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Vyakula vinavyotokana na mimea kwenye lishe yako ni vizuri kwa afya ya moyo, utafiti wa miongo minne ya data umeonyesha.

    Watafiti nchini Denmark walionyesha vyakula vya mboga mboga hupunguza viwango vya cholesterol na mafuta katika damu ambayo huongeza mashambulizi ya moyo.

    Athari - sawa na karibu theluthi moja ya kuchukua dawa za kila siku - ilikuwa "kubwa sana", walisema.

    Lakini wataalam walisema nyama na maziwa vina faida zao za kiafya - na sio lishe zote zisizo na nyama zilikuwa na afya.

    Utafiti huo ulikusanya majaribio 30 tangu 1982 ambapo wanasayansi waliwapa watu wa kujitolea lishe iliyowekwa na kufuatilia athari zake kwa afya ya moyo.Kwa jumla, karibu watu 2,400 kutoka kote ulimwenguni walihusika.

    Viwango vya juu vya cholesterol mbaya husababisha mkusanyiko wa mafuta kwenye mishipa ya damu, ambayo inaweza kusababisha mshtuko wa moyo au kiharusi.

    Matokeo,yaliyochapishwa katika Jarida la Moyo la Ulaya, yalionyesha mlo wa mboga :

    • kupunguza cholesterol mbaya kwa 10%
    • Hupunguza cholesterol jumla kwa 7%
    • Hupunguza apolipoprotein B (protini kuu katika cholesterol mbaya) kwa 14%

    "Hiyo inalingana na theluthi moja ya athari za statin ya kupunguza kolesteroli [kidonge] - hivyo hiyo ni muhimu sana," Prof Ruth Frikke-Schmidt, ambaye aliendesha kazi hiyo, huko Rigshospitalet, nchini Denmark, aliambia BBC News.

    Lakini Prof Frikke-Schmidt alitumia data kutoka kwa majaribio ya statins kukadiria kudumisha lishe kama hiyo kwa miaka 15 kunaweza kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na mishipa kwa 20%.

    Shirika la Afya Ulimwenguni linakadiria ugonjwa wa moyo na mishipa huua karibu watu milioni 18 kila mwaka.

    Unaweza pia kusoma

  11. Tazama: Nyimbo nane kati ya nyimbo maarufu za Tina Turner

    Maelezo ya video, Tazama: Nyimbo nane kati ya nyimbo maarufu za Tina Turner

    Tunaangazia baadhi ya vibao vya Tina Turner - na maonyesho ya kitambo - baada ya kufariki akiwa na umri wa miaka 83.

  12. Belgorod: Kikundi cha wanamgambo wa Urusi chaapa kufanya uvamizi zaidi ndani ya nchi hiyo

    th

    Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/SHUTTERSTOCK

    Mkuu wa kundi la wanamgambo wa Urusi ambalo lilisema lilihusika na uvamizi wa mpakani nchini Urusi kutoka Ukraine ameapa kuongoza uvamizi zaidi kama huo.

    "Nadhani utatuona tena upande huo," alisema Denis Kapustin, anayeongoza Kikosi cha Kujitolea cha Urusi (RDK).

    Urusi ilisema imezuia uvamizi huo, na kuua zaidi ya wahujumu 70.Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu aliahidi "jibu kali" kwa uvamizi wowote wa siku zijazo.

    Ukraine inakanusha kuhusika na uvamizi huo.

    RDK pamoja na Jeshi la Uhuru wa Russia (LSR) walidai kutekeleza uvamizi wa Jumatatu katika eneo la Belgorod.

    Akizungumza siku ya Jumatano na waandishi wa habari katika mpaka wa Ukraine, Bw Kapustin, ambaye jina lake ni White Rex, alisema: "Tumeridhika na matokeo [ya uvamizi]."

    Alisema kundi lake lilifanikiwa kukamata "baadhi ya silaha", ikiwa ni pamoja na shehena ya magari ya kivita yenye silaha, na kuwashika mateka watu kadhaa wakati wa operesheni - kabla ya kuondoka katika eneo la Urusi baada ya saa 24.

    Alisema wapiganaji wawili wa RBK walijeruhiwa, akikanusha madai ya jeshi la Urusi kuhusu hasara kubwa iliyofanywa dhidi ya wavamizi hao.

    LSR ilisema wapiganaji wake wawili wameuawa na 10 kujeruhiwa.

    Pia unaweza kusoma:

    • Uvamizi wa Belgorod: Je ni wapiganaji gani wanaoingia Urusi kutoka Ukraine?
    • Urusi yadai kuudhibiti mji wa Bakhmut, Ukraine inasema ni "mtego wa panya". Nani yuko sahihi?
  13. Salamu za rambirambi zamiminika baada ya kifo cha Malkia wa Rock 'n' Roll Tina Turner

    Tina Turner

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Nyota huyu aliyeshinda tuzo nyingi za Grammy alifariki akiwa na umri wa miaka 83.

    Salamu za rambi rambi zimekuwa zikimiminika kufuatia kifo cha mwimbaji Tina Turner nchini Uswizi. Nyota aliyeshinda tuzo nyingi za Grammy alifariki akiwa na umri wa miaka 83.

    Kuanzia kwa Obama hadi Oprah, Beyoncé hadi Brian Wilson, majina mengi makubwa yamekuwa yakisherehekea maisha ya marehemu nyota huyo. Wengi walinukuu mojawapo ya nyimbo zake bora zaidi, wakisema kwamba alikuwa "mzuri sana".

    Pamoja na kuangazia mafanikio yake ya muziki, wengine walimpongeza kwa kujiondoa katika uhusiano mbaya. Kama Mariah Carey alivyosema, alikuwa "mwokozi na msukumo kwa wanawake kila mahali".

    Rais wa Marekani Joe Biden alisema Turner "amebadilisha muziki wa Marekani daima", baada ya kukua kama binti wa mkulima huko Tennessee.

    Mwanzilishi wa Hip-hop Grandmaster Flash alisifu "nguvu thabiti" za Turner katika kushinda matatizo ya kibinafsi na kuwa "nyota bora"

    Maelezo zaidi:

  14. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Alhamisi 25.05.2023.