Mwandishi wa habari mashuhuri wa Pakistani auawa kwa kupigwa risasi nchini Kenya

Vyombo vya habari vya ndani viliripoti kwamba kuuawa kwa Bw Sharif na polisi ni kisa cha utambulisho usio sahihi.

Moja kwa moja

  1. Mpaka hapo tumefika tamati ya taarifa zetu kwa leo, mpaka kesho panapo majaaliwa

  2. Waziri Mkuu mpya wa Uingereza aahidi kuhudumu kwa 'uadilifu na unyenyekevu'

    Rishi Sunak

    Rishi Sunak amepanda jukwaani kwa hotuba yake ya kwanza kwa umma kama kiongozi wa Tory.

    Anaanza kwa kutoa pongezi kwa Liz Truss kwa uongozi wake "wenye heshima" "chini ya hali ngumu nje ya nchi na nyumbani".

    Sunak ameahidi kutumikia kwa uadilifu na unyenyekevu. Anasema "atafanya kazi siku baada ya siku kwa ajili ya watu wa Uingereza."

    "Ninaahidi kuwa nitahudumu kwa uadilifu na unyenyekevu," Sunak alisema.

    Rishi Sunak amesema Uingereza ni nchi kubwa lakini inakabiliwa na changamoto "kubwa" za kiuchumi.

    Ametoa wito wa utulivu na umoja.

    Sunak amesema "ananyenyekea na kuheshimu" kuungwa mkono na wabunge wenzake na kuchaguliwa kuwa kiongozi.

    "Ni bahati kubwa maishani mwangu kuweza kutumikia chama ninachokipenda na kurudisha nchi ninayodaiwa sana."

  3. Majeshi ya Rwanda yagundua hifadhi ya pili ya silaha nchini Msumbiji,

    Jeshi

    Chanzo cha picha, Reuters

    Vikosi vya usalama vya Rwanda vinavyohusika katika operesheni za kukabiliana na ugaidi katika jimbo la kaskazini mwa Msumbiji lenye utajiri wa gesi la Cabo Delgado vimegundua hifadhi ya silaha iliyoachwa na wanajihadi.

    Ilikuwa ugunduzi wa pili kama huo ndani ya siku saba zilizopita.

    Silaha hizo zilipatikana katika msitu wa Limala, kusini-mashariki mwa wilaya ya Mocimboa da Praia - ambayo zamani ilikuwa ngome ya wanajihadi kabla ya kufurushwa na vikosi vya Msumbiji na Rwanda mnamo Agosti mwaka 2021.

    Taarifa kutoka kwa Wizara ya Ulinzi ya Rwanda inasema waasi hao wa Kiislamu wanaohusishwa na kundi la Islamic State wamejaribu "mara kadhaa kurejea kuchukua silaha bila mafanikio".

    Silaha na risasi zilizofichwa na wanajihadi ziligunduliwa tarehe 15 Oktoba, katika eneo la msitu mnene la Mbau.

    Vikosi vya Rwanda vimekuwa katika operesheni ya kuwazuia wanajihadi hao kurejea na kujizatiti katika eneo hilo kwa ajili ya vitendo zaidi vya uasi.

    Wanajihadi walifukuzwa kutoka Palma na Mocímboa da Praia, wilaya hizo mbili zilizo chini ya jukumu la vikosi vya usalama vya Rwanda, lakini wamesalia katika wilaya jirani.

  4. Habari za hivi punde, Rishi Sunak sasa kuchukua nafasi ya Waziri Mkuu wa Uingereza

    Rishi Sunak

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rishi Sunak sasa atachukua nafasi ya Waziri Mkuu katika wakati mgumu sana kwa uchumi.

    Haijasikika mipango yoyote ya kina kutoka kwake tangu kampeni ya uongozi katika msimu wa joto.

    Sasa kutakuwa na wito wa kumtaka atoe ufafanuzi kuhusu jinsi anavyokusudia kusawazisha vitabu.

    Pia kutakuwa na shinikizo la kisiasa kwa uchaguzi mkuu.

    Wiki saba baada ya kushindwa katika uchaguzi wa viongozi wa Conservative, Rishi Sunak sasa atakabidhiwa ufunguo wa Downing Street.

    Wiki saba baada ya kushindwa na Liz Truss katika kinyang'anyiro hicho mwaka huu

    Anatarajiwa kuwa waziri mkuu wa kwanza wa Uingereza mwenye asili ya Asia , na atachukua madaraka huku Uingereza ikikabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi.

  5. Mwanasiasa wa Brazil awarushia guruneti polisi katika jimbo la Rio de Janeiro

    Gari la polisi likiwa na kioo cha mbele kilichovunjwa baada ya tukio la Jumapili

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mwanasiasa wa Brazil amekamatwa baada ya kuwarushia maguruneti maafisa wa polisi waliofika nyumbani kwake katika jimbo la Rio de Janeiro kumkamata.

    Roberto Jefferson, mshirika wa Rais wa mrengo mkali wa kulia Jair Bolsonaro, aliwajeruhi maafisa wawili kabla ya kujisalimisha siku ya Jumapili.

    Awali hakimu wa Mahakama ya Juu aliamuru akamatwe kwa kumtusi Jaji Mkuu Cármen Lucía.

    Tayari alikuwa chini ya kizuizi cha nyumbani kwa kumtishia. Bw Bolsonaro alijibu kwa kusema wale waliowafyatulia risasi polisi wanapaswa kukamatwa.

    Maafisa hao wawili walijeruhiwa na vilipuzi wakati wa shambulizi huko Comendador Levy Gasparian, kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo la Rio de Janeiro.

    Walipelekwa hospitali na baadaye kuruhusiwa. Bw Jefferson, kiongozi wa zamani wa chama cha kisiasa cha PTB, mwenye umri wa miaka 69, pia alifyatua risasi kadhaa na kuvunja kioo cha mbele cha gari la polisi.

    Jaji wa Mahakama ya Juu Alexandre de Moraes alikuwa ameamuru mwanasiasa huyo azuiliwe kwa msingi kwamba alikiuka masharti ya kifungo cha nyumbani.

    Mvutano wa kisiasa umetanda nchini Brazil kabla ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais Jumapili kati ya Bw Bolsonaro na Luiz Inacio Lula da Silva.

  6. Wanafunzi wabuni kofia za mtihani za 'kuzuia udanganyifu'

    Mwanafunzi

    Chanzo cha picha, MARY JOY MANDANE-ORTIZ

    Picha za wanafunzi waliovalia ziitwazo "kofia za kuzuia udanganyifu" wakati wa mitihani ya chuo kikuu zimeenea kwenye mitandao ya kijamii nchini Ufilipino, na hivyo kuwa jambo la burudani.

    Wanafunzi katika chuo kimoja katika Jiji la Legazpi waliombwa wavae vazi ambalo lingewazuia kuchungulia karatasi za wengine.

    Wengi walifanya ubunifu wa nyumbani wakitumia kadi ngumu, trei ya mayai na vifaa vingine.

    Mkufunzi wao aliiambia BBC kwamba amekuwa akitafuta "njia ya kufurahisha" kuhakikisha "uadilifu na uaminifu" katika madarasa yake.

    Mary Joy Mandane-Ortiz, profesa wa uhandisi wa mitambo katika Chuo Kikuu cha Uhandisi cha Bicol, alisema wazo hilo lilikuwa "lenye ufanisi sana". Ilitekelezwa kwenye mitihani ya hivi karibuni ya katikati mwa muhula, ambayo ilifanywa na mamia ya wanafunzi katika chuo hicho katika wiki ya tatu ya Oktoba.

    Prof Mandane-Ortiz alisema ombi lake la awali lilikuwa kwa wanafunzi kutengeneza muundo "rahisi" kutokana na karatasi.

    Alitiwa moyo na mbinu iliyoripotiwa kutumika nchini Thailand miaka kadhaa hapo awali.

    Wanafunzi wakiwa darasani

    Chanzo cha picha, MARY JOY MANDANE-ORTIZ

    Mnamo mwaka 2013, picha ilisambaa ikionesha chumba cha wanafunzi wa chuo kikuu huko Bangkok wakichukua karatasi za mtihani huku wakiwa wamevaa "vizibo vya masikio" - karatasi zilizowekwa kila upande wa vichwa vyao ili kuzuia uwezo wao wa kuona.

    Msururu wa machapisho ya profesa huyo kwenye Facebook - yanayowaonesha vijana hao wakiwa wamevalia ubunifu wao wa hali ya juu - ilipata maelfu ya 'likes' katika muda wa siku chache, na kuvutia habari kutoka kwa vyombo vya habari vya Ufilipino.

    Pia inasemekana walihamasisha shule na vyuo vikuu katika maeneo mengine ya nchi kuwahimiza wanafunzi wao wenyewe kuweka pamoja vazi la kupinga udanganyifu.

    Prof Mandane-Ortiz alisema wanafunzi wake walifanya vyema zaidi mwaka huu, baada ya kuchochewa na masharti magumu ya mitihani ya kusoma kwa bidii zaidi.

    Wengi wao walimaliza majaribio yao mapema, aliongeza - na hakuna mtu aliyekamatwa akidanganya mwaka huu.

  7. Mashambulio ya Urusi dhidi ya Ukraine: maelezo ya Mkuu wa majeshi ya Ukraine kwa ufupi

    Pavlo Kirilenko/telegram

    Chanzo cha picha, Pavlo Kirilenko/telegram

    • Kwa muda wa saa 24, Urusi iliwafyatua makombora kwenye miundo mbinu ya raia na makazi katika majimbo ya Bakhmut, Zaporozhye, Nikolaev na Novotavricheskoye na Zaporozhye
    • Kwa ujumla, katika muda wa saa 24, kulikuwa na mashambulizi ya makombora mawili na mashambulizi ya anga 28 kutoka kwa Urusi, pamoja na mashambulizi 65 kutoka kwenye mifumo mingi ya roketi, amesema mkuu wa Majeshi ya ulinzi ya Ukraine katika ripoti yake leo asubuhi.
    • Kutokana na mashambulio ya makombora katika jimbo laDonetsk, raia sita wameuawa, wengine 5 wakajeruhiwa, alisema mkuu wa polisi katika jimbo la Donetsk ,Pavel Kirilenko.
    • Katika jimbo la Bakhmut, jeshi la Urusi lilishambulia hospitali, katika nyumba za kibinafsi za eneo la Nikolaev, shule, mifumo ya umeme iliharibiwa. Hapakuwa na majeruhi.
    • Katika jimbo la Kharkiv, mashambulio ya wilaya za Kupyansky, Chuguevsky, Izyumsky na Bogodukhovsky.
  8. Burundi yawazuia raia wake kwenda nchini Serbia

    NTARE HOUSE

    Chanzo cha picha, NTARE HOUSE

    Maelezo ya picha, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye

    Maafisa nchini Burundi wamewazuia raia wa nchi hiyo kwenda Serbia hata kama wana paspoti na visa.

    Mamia ya Warundi waliokuwa wakisafiri hivi karibuni kuelekea Serbia wamekwama katika viwanja vya ndege vya Uturuki na Qatar huku wakiombwa vibali vyao vya kusafiria -visa , baadhi wameiambia BBC.

    Karibu Warundi 200 walirejeshwa nyumbani mwishoni mwa juma, wizara ya mambo ya ndani ilitangaza kwenye ukurasa wa Twitter Jumapili.

    “Warundi wenye paspoti ya kawaida na visa walizuiwa kuelekea Serbia katika uwanja wa ndege wa Bujumbura, na pia kupitia nchi jirani”, ilisema wizara.

    Makubalino ya visa ya bila malipo yaliyoidhinishwa mwezi Juni yaliwafanya maelfu ya Warundi kununua tiketi za kwenda Serbiana mara baada ya kuwasili kwa nchihiyo ambayo sio mwanachama wa Muungano wa Ulaya wengi wao walisafiri kuelekea katika nchi za Magharibi, hususan Ubelgiji.

    Kutokana na ukosefu wa visa, mwanamke mmoja aliyekwama nchini Uturuki na watoto wake wawili mmoja mwenye umri wa miaka mitatu na mwingine mwenye umri wa mwaka mmoja, alisema: “Ni zaidi ya wiki moja sasa niko hapa. Nilitumia franga milioni 30 (karibu US$15,000).

    “Wengi wanauza mali zao zote kwa matumaini ya kupata maisha bora Ulaya. Tunawezaje kurudi?” aliiambia BBC Jumapili.

  9. Mamlaka ya kusimamia shughuli za Polisi yachunguza mauaji ya mwandishi wa habari wa Pakistan

    Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi nchini Kenya (Ipoa) inasema imeanzisha uchunguzi kuhusu mauaji ya mwanahabari mashuhuri wa Pakistani Arshad Sharif.

    Vyombo vya habari vya ndani viliripoti kwamba kuuawa kwa Bw Sharif na polisi ni kisa cha utambulisho usio sahihi.

    Ipoa, chombo cha kiraia, kiliundwa kufuatilia kazi ya polisi.

    Mkuu wake, Ann Makori, amewaambia waandishi wa habari katika mji mkuu, Nairobi, kwamba timu maalum ya kutafuta majibu ya haraka imetumwa kuchunguza mauaji ya mwandishi huyo.

    Kituo cha runinga cha Citizen kimechapisha kwenye ukurasa wa twitter video ya matamshi ya Bi Makori:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  10. Diwali 2022: India yaadhimisha tamasha kwa kuonyesho taa za kung’aa

    Diwali pia inaitwa tamasha la taa

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Diwali pia inaitwa tamasha la taa

    Mitaa ya India na nyumba zinang’aa kwa rangi za kupendeza na taa zinazotoa mwangazahuku mamilioni ya watu wakiadhimisha tamasha Wahindu la Diwali .

    Lakini sherehe hizo pia zinaibua hofu kuhusu uchafuzi wa hewa , ikiwa ni pamoja na katika mji mkuu , Delhi.

    Ni muda wa siku kuu, maombi na kufyatua baruti, Diwali ni mojawapo ya matamasha muhimu nchini India. Inafahamika kama tamasha la taa huku watu wakiwasha mataa ya mafuta au mishumaa kama ishara yaushindi wa nuru dhidi ya giza na wema juu ya ubaya.

    Watu huwasha mwangaza majumbani mwao kwa kutumia taa za mafuta na kuchorarangolis -mitindo ya kitamaduni iliyochorwa kwa kutumia poda za rangi mbali mbali – nje ya milango kukaribisha bahari nzuri na fikra chanya katika maisha yao.

    G

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Watu huchora michoro ya kitamaduni ya rangolis kwa ajili ya bahati nzuri
    Mamilioni ya Wahindi huadhimisha Diwali

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Mamilioni ya Wahindi huadhimisha Diwali
    watu hung'iniza taa nje ya nyumba zao

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, watu hung'iniza taa nje ya nyumba zao
  11. Kenya kuanza kesi dhidi ya maafisa wa 'kikosi cha polisi wauaji'

    th

    Chanzo cha picha, AFP

    Polisi wanne wa Kenya wanaodaiwa kuhusika na msururu wa mauaji, utekaji nyara na mateso kote nchini wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu katika mji mkuu, Nairobi.

    Walikuwa sehemu ya kikosi maalum ambacho kilivunjwa na Rais William Ruto kwa madai ya kutekeleza mauaji ya kiholela na kutoweka kwa washukiwa kwa miaka kadhaa.

    Miongoni mwa wanaodaiwa kuwa wahasiriwa wa hivi punde ni raia wawili wa India waliotoweka mwezi Julai na ambao mabaki yao yaligunduliwa wiki iliyopita katika msitu mmoja katikati mwa Kenya.

    Wanachama wa Kitengo cha Huduma Maalum kilichovunjwa sasa wanakabiliwa na mashtaka mengi yakiwemo mauaji, matumizi mabaya ya ofisi na kula njama ya kutenda uhalifu.

    Kitengo hicho kilivunjwa baada ya rais kupokea ripoti ya polisi kuhusu kutoweka kwa raia hao wawili wa India.

    Zulfiqar Ahmad Khan na Mohamed Zaid Sami Kidwai walikuwa nchini Kenya kusaidia kampeni za uchaguzi za Bw Ruto, lakini walitoweka pamoja na dereva wao wa eneo hilo Nicodemus Mwania mara baada ya kuchukuliwa na polisi jijini Nairobi.

    Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema uchunguzi wao huru umehusisha kikosi hicho na vitengo vingine vya polisi na vifo vya zaidi ya watu 600 katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

    Baadhi ya miili hiyo ilipatikana baadaye katika mito magharibi na kaskazini mwa Kenya.

    Muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa na ya ndani sasa unaitaka serikali kuwafungulia mashitaka maafisa hao, na kuwalipa fidia waathiriwa wa unyanyasaji wa polisi.

  12. Mwandishi wa habari mashuhuri wa Pakistani auawa kwa kupigwa risasi nchini Kenya

    Polisi nchini Kenya wamethibitisha kupigwa risasi kwa mwanahabari maarufu wa Pakistani Arshad Sharif Jumapili usiku katika kaunti ya Kajiado, ambayo ni jirani na mji mkuu Nairobi.

    Msemaji wa polisi Bruno Shioso anasema wanachunguza hali iliyosababisha kifo cha Bw Sharif.

    Vyombo vya habari vya ndani vinasema alipigwa risasi kwenye kizuizi cha barabarani kwenye barabara kuu ya Nairobi-Magadi katika kisa cha utambulisho kimakosa.

    Mkewe Bw Sharif, Javeria Siddique alisema kupitia Twitter siku ya Jumatatu kwamba "amempoteza [rafiki], mume na mwanahabari ninayempenda".

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Rais wa Pakistan Arif Alvi alisema "Kifo cha Arshad Sharif ni pigo kubwa kwa uandishi wa habari na Pakistan. Roho yake ipumzike kwa amani na familia yake, ambayo ni pamoja na wafuasi wake, wawe na nguvu kustahimili pigo hili".

  13. Ujasusi wa Uingereza: Ukraine inapigana na droni za Iran na kwa mafanikio zaidi

    IRANIAN ARMY/GETTY IMAGES

    Chanzo cha picha, IRANIAN ARMY/GETTY IMAGES

    Ujumbe wa Twitter kutoka Wizara ya ulinzi, umeelezea taarifa mpya kuhusu uchunguzi wa kijasusi wajeshi la Uingereza. Haya ndio mambo yaliyoelezwa katika taarifa hiyo:

    • Juhudi za Ukraine za kupambana na ndege zisizokuwa na rubani za Iran Shahed-136 zinazojiongoza zimekuwa na mafanikio makubwa
    • Vyanzo rasmi, akiwemo rais waUkraine Volodymyr Zelensky, anasema hadi 85% ya ndege hizi ambazo zimekuwa zikizurura zimekuwa zikilazimishwa kurudi nyuma.
    • Ndege hizi zinakwenda mwendo wa kasi ya chini, zina kelele, na zinasafiri katika kima cha chini, na hivyo kuzifanya kuwa rahisi kuzishughulikia zinapopaa peke yake.
    • Kuepuka athari zinazoongezeka kutoka kikosi cha ulinzi wa anga cha Ukraine, Urusi imelazimika kutumia idadi kubwa ya droni za Iran.
    • Urusi inazitumia kama silaha mbadala kwa ajili ya silaha za masafa marefu za Urusi zinazopiga maeneo yaliyo yaliyolengwa kwa ufanisi. Silaha hizi zimeendelea kuwa haba.
    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Unaweza pia kusoma:

    • Vita vya Ukraine: Kukua kwa uhusiano kati ya Urusi na Iran kunaleta hatari mpya
    • Vita vya Ukraine: Kyiv yalaani madai ya Urusi ya 'bomu chafu'
    • Urusi na Ukraine: Ni zipi hatari za shambulio la kinyuklia?
  14. Watu tisa zaidi wapatikana na maambukizi ya Ebola Uganda

    G

    Watu wengine tisa wamepatikana na virusi vya Ebola, katika hospitali ya rufaa ya taifa nchini Uganda ya Mulago iliyopo katika mji mkuu Kampala.

    Idadi hii inapelekea idadi ya visa vya wagonjwa wenye Ebola nchini humo waliotengwa kwenye vituo maalumukuwa 14.

    Waziri wa afya nchini UgandaDkt. Jane Ruth Aceng amesema kwamba waliopatikana na virusi ni wale waliowasiliana na watu waliotoka Kassanda, moja ya wilaya zilizoathiriwa zaidi, ambao hivi karibuni walifariki katika hospitali ya Mulago.

    Visa saba kati ya visa vipya ni watu wa kutoka familia moja. Wengine ni mhudumu wa afya na mke wake. Mhudumu wa afya anatoka katika kliniki ya neo lililopo nje kidogo ya jiji la Kampala, ambako alimtibu mmoja wa watu ambao wamepatikana virusi kwa sasa.

    Hofu imeendelea kuongezeka kwamba mlipuko huo huenda usiweze kudhibitika , huku visa vya maambukizi vikiendelea kuripotiwa katika mji mkuu.

    Kuna karantini inayoendelea Tkatika wilaya mbili zilizoathiriwa zaidi zaMubende na Kassanda, lakini visa vya maambukizi vimeendelea kuongezeka,

    Wiki iliyopita, maafisa walifanya ukaguzi katika hospitali na kliniki mjini Kampala, kuangalia utayari wao wa kushughulikia visa vya Ebola.

    Ni zaidi ya mwezi mmoja tangu uliporipotiwa mlipuko wa Ebolaaina ya Sudan kwa mara ya kwanza katika eneo la kati la Uganda, katika eneo la vijijini la wilaya la Mubende.

    Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa kuna watu 75 ambao wamepatikana na Ebola nchini Uganda, na 28 yao walifariki.

    Hivi ni visa vilivyothibitishwa pekee, na idadi hii haijumuishi idadi ya visa ambavyo vya maambukizi na vifo ambavyo huenda havikurekodiwa.

  15. Umoja wa Mataifa : watu wengi wanakimbia mapigano baina ya jeshi la serikali na M23 katika Rutshuru

    Umoja wa Mataifa unasema kuwa watu wengi wamezikimbia nyumba zao kutokana na mapigano yanayoendelea katika eneo la Rutshuru, miongoni mwao wakikimbilia nchini Uganda.

    Katika ujumbe wake wa Twitter, shirika la Umoja wa Mataifa la usimamizi wa mishaa OCHA, linasema kuwa bado linachunguza kufahamu idadi ya wakimbizi na msaada gani unaohitajika kwa ajili ya kuwasaidia.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Jeshi la DRC - FARDC na wapiganaji wa M23 hawajasema lolote kuhusiana na vita hivyo vinavyoendelea.

  16. Rishi Sunak huenda akawa Waziri mkuu Uingereza baada ya Johnson kujiondoa

    th

    Chanzo cha picha, Reuters

    Huku waziri mkuu wa zamani Boris Johnson akijiondoa kutoka kinyang’anyiro cha kuiongoza Uingereza na chama cha conservative anayetarajiwa na wengi kuwa waziri mkuu mpya ni Rishi Sunak - na, iwapo Penny Mordaunt hatakusanya jeshi la wafuasi mara nyingi zaidi ya wale waliosajiliwa sasa, na kati ya sasa na wakati wa chakula cha mchana, ushindi wa Sunak unaweza kuthibitishwa leo mchana.

    Chochote kitakachotokea kutakuwa na waziri mkuu mpya mwishoni mwa juma.

    Ndio, waziri mkuu wa tatu katika wiki saba.

    Kiwango kisicho na kifani cha msukosuko; mfululizo wa matukio mabaya ambayo wanachama wengi wa Torries wanakiri faraghani yamefikia sarakasi ya upuuzi na kuharibu sana sifa ya chama chao.

    Mshindi atarithi kikapu kile kile cha kuugua cha matatizo ambayo yameonekana kuwa mazito sana kwa Liz Truss kubeba: chama kilichogawanyika sana; kupanda kwa bei, ufinyu wa fedha za umma na kundi la vyama vya upinzani vikisema havina uhalali wa uchaguzi.

  17. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo Jumatatu tarehe 24 Oktoba 2022