Uingereza yatayarisha mabilioni ya Pauni kusaidia silaha na kuijenga upya Ukraine

Kiasi kikubwa - £2.3bn - kitakwenda kufadhili mauzo ya nje ya ulinzi wa Uingereza kwa Ukraine, na mikopo ya £ 700m iliyobaki itaenda kwa makampuni ya Uingereza ambayo Ukraine itaalika kuijenga upya nchi baada ya uvamizi wa Urusi.

Moja kwa moja

  1. Na hapo ndio mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa hii leo

  2. Urusi na Ukraine: Uingereza yatayarisha mabilioni ya Pauni kusaidia silaha na kuijenga upya Ukraine

    Mamlaka ya Uingereza imechukua hatua muhimu kusaidia usambazaji wa silaha kwa Ukraine

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Mamlaka ya Uingereza imechukua hatua muhimu kusaidia usambazaji wa silaha kwa Ukraine

    Mamlaka ya Uingereza imechukua hatua muhimu katika kutenga pauni nyingine bilioni 3 kwa kusaidia usambazaji wa silaha kwa Ukraine na ujenzi mpya wa nchi hiyo baada ya vita.

    Televisheni ya Uingereza Sky News iliripoti kwamba Mkuu wa hazina wa Uingereza, Nadeem Zahavi, aliunga mkono utoaji wa ufadhili wa kabla ya mauzo ya nje kupitia wakala wa serikali UKEF.

    "Ninaona kuwa ni muhimu sana kuendelea kusaidia mamlaka ya Ukraine kwa njia zote zinazopatikana. Ni lazima tuoneshe imani katika mustakabali wa Ukraine,” Zahavi, ambaye anasimamia sera ya bajeti ya nchi hiyo, alisema katika maoni yake kuhusu pendekezo la UKEF la kutenga fedha.

    Kiasi kikubwa - £2.3bn - kitakwenda kufadhili mauzo ya nje ya ulinzi wa Uingereza kwa Ukraine, na mikopo ya £ 700m iliyobaki itaenda kwa makampuni ya Uingereza ambayo Ukraine itaalika kuijenga upya nchi baada ya uvamizi wa Urusi.

    Soma zaidi:

  3. Wakenya waguswa na tukio la naibu rais kulia

    Wakenya waguswa na tukio la naibu rais kwa bubujikwa na machozi kanisani

    Wananchi wajawa na hisia na kisa cha Naibu Rais wa Kenya William Ruto kuangua kilio wakati wa mkutano wa maombi nyumbani kwake.

    Hii ni mara ya pili kwa Bw Ruto kumwaga machozi hadharani, mara ya kwanza ikiwa 2013 wakati yeye na Rais Uhuru Kenyatta waliposhinda muhula wao wa kwanza afisini.

    Naibu rais wametofautiana na rais tangu wakati huo na sasa rais anamuunga mkono mshindani wa naibu rais, aliyekuwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga katika uchaguzi huu.

    Kipindi cha Bw Ruto ‘’kububujikwa na machozi’’ siku ya Jumanne kiliripotiwa na vyombo vingi vya habari nchini.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Katika video hiyo iliyosambazwa mtandaoni, Bw Ruto aliuzika uso wake mikononi mwake na baadaye akaonekana akifuta machozi.

    Mhubiri anaweza kusikika nyuma akiomba katikati ya nyimbo za ibada.

    Mkutano huo ulikuwa umeandaliwa ili kuombea nchi kabla ya uchaguzi wa Jumanne.

    Wakenya kwenye Twitter walikuwa na maoni tofauti kuhusu kisa hicho: “Je, Ruto anayelia na Ruto anayerusha matusi mitaani ni mtu yule yule?”

    Lydia Ngaira aliweka kiuliza.

    “Dkt William Ruto analia, anasali na kuombea Kenya. Mungu atamlipa,” Sammy Masio aliweka ujumbe kwenye mtandao wa Twitter.

    Kinyanganyiro cha urais nchini Kenya kimekaribia kati ya Bw Ruto na Bw Odinga, kwa mujibu wa kura za hivi punde - hakuna hata mmoja anayekidhi matakwa ya kikatiba ya kupata zaidi ya 50% ya kura zinazohitajika ili kushinda.

    Soma zaidi:

  4. DR Congo inataka msemaji wa Umoja wa Mataifa kuondoka

    Serikali imeweka wazi kuwa inatarajia kuharakisha Umoja wa Mataifa kujiondoa nchini humo

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Serikali imeweka wazi kuwa inatarajia kuharakisha Umoja wa Mataifa kujiondoa nchini humo

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imemtaka msemaji wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo kuondoka haraka iwezekanavyo.

    Wizara ya mambo ya nje ilimshutumu Mathias Gillmann kwa kutoa ‘’taarifa zisizoeleweka na zisizofaa’’.

    Wiki iliyopita, kikosi cha Umoja wa Mataifa, kinachojulikana kama Monusco, kilikuwa kitovu cha maandamano ya ghasia mashariki mwa DR Congo.

    Takriban watu 30, wakiwemo wanajeshi wanne wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na maafisa wa polisi, walikufa wakati wa machafuko hayo.

    Waandamanaji hao walilalamika kwamba ujumbe wa Umoja wa Mataifa umeshindwa kukomesha kuzuka upya kwa ghasia za waasi, zaidi ya miongo miwili baada ya kutumwa kwa mara ya kwanza.

    Soma zaidi:

  5. Je, Marekani na China zimekuwa zikisema nini kuhusu ziara ya Nancy Pelosi Taiwan?

    Nancy Pelosi akiwa katika ziara rasmi Taiwan

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Nancy Pelosi akiwa katika ziara rasmi Taiwan

    Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alitoa kauli kadhaa zenye maneno makali wakati wa ziara ya Pelosi nchini Taiwan, akiwashutumu wanasiasa wa Marekani kwa ‘’kucheza na moto’’.

    Akiita ziara hiyo kuwa ni ya ‘’kizushi’’, Wang Yi alisema kuwa Marekani ‘’inakiuka mamlaka ya China kwa kisingizio cha kile kinachoitwa ‘’demokrasia’’.

    Pia alimshutumu rais wa Taiwan Tsai Ing-wen kwa ‘’kung'ang'ania Marekani’’ na ‘’kupuuza haki yake ya kitaifa&quot’’.

    Wakati huo huo, msemaji wa usalama wa kitaifa wa White House John Kirby alisema kuwa Marekani’’haitatishwa’’ na vitisho vya Uchina au matamshi ya kejeli na kwamba hakuna sababu ya ziara ya Pelosi kuzua mzozo kati ya nchi hizo mbili.

    Kirby pia alionya kwamba China inaweza kushiriki katika ‘’shurutisho la kiuchumi’’ dhidi ya Taiwan na kusema kuwa, kwenda mbele, uhusiano wa Marekani na Uchina utategemea tabia na hatua za Wachina.

    Soma zaidi:

  6. Kenya yamkamata mtoro anayesakwa Marekani kwa biashara ya dawa za kulevya

    Polisi wa Kenya wamemkamata mshukiwa anayehusishwa na genge la kimataifa la ulanguzi wa dawa za kulevya na wanyamapori na ambaye alikuwa amefunguliwa mashtaka katika mahakama ya Marekani akiwa na wenzake watatu.

    Polisi nchini Kenya ilisema wapelelezi wa Kitengo cha Uhalifu siku ya Jumanne walimkamata Abdi Hussein Ahmed, almaarufu Abu Khadi katika kaunti ya Meru kufuatia taarifa kutoka kwa umma.

    Bw Ahmed alishtakiwa mwaka wa 2019 katika mahakama ya Wilaya ya Kusini mwa New York kwa kula njama ya kusafirisha pembe za faru na aina ya tembo wenye thamani ya $7m (£5.7m) na nia ya kusafirisha kilo moja ya kokeini.

    Alishtakiwa kwa pamoja na Moazu Kromah almaarufu Ayoub, Amara Cherif almaarufu Bamba Issiaka, na Mansur Mohamed Surur almaarufu Mansour.

    Inasemekana walikuwa wamepanga njama ya kusafirisha pembe hizo kutoka Kenya, Uganda, DR Congo, Guinea, Msumbiji, Senegal na Tanzania.

    Kukamatwa huko kumewadia baada ya afisa wa Ubalozi wa Marekani Eric Kneedler na mkurugenzi mkuu wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), George Kinoti, kutoa ombi la umma tarehe 26 Mei ili kupata taarifa zinazoweza kusababisha kukamatwa kwa Bw Ahmed.

    Mshirika wa Bw Ahmed, Badru Abdul Aziz Saleh, alikamatwa wiki moja baada ya ombi hilo.

    DCI ilisema kukamatwa kwa Bw Ahmed na Bw Saleh kuliashiria ‘’ushirikiano wa muda mrefu ambao kurugenzi imekuwa nao na Marekani katika kupambana na uhalifu uliopangwa baina ya mataifa mbalimbali duniani’’.

    Ilishirikisha taarifa kuhusu kukamatwa kwa mtu huyo kwenye Twitter

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Bandari za Kenya ndizo zinazoongoza kwa ulanguzi wa binadamu na dawa za kulevya, kulingana na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa ya Kulevya na Uhalifu.

  7. Jimbo la Kansas laidhinisha utoaji mimba, ushindi mkubwa kwa makundi yanayopigania utoaji mimba

    Getty

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Jimbo la conservative nchini Marekani la Kansas limeamua kwa kura ya maoni kulinda haki za utoaji mimba -katika ushindi mkubwa kwa makundi yanayopendelea kutoa mimba liwe chaguo la mtu.

    Wapiga kura walipiga kura kwa wingi kuamua kuwa wasingependa kurekebisha katiba ili pasiwe na haki ya kutoa mimba.

    Lilikuwa ni jaribio la kwanza kuhusu suala hilo tangu Mahakama ya juu ya Marekani iruhusu majimbo kuzuia utoaji mimba..

    Kama wapiga kura wangeafiki hilo, wabunge wangeweza kusonga mbele na kuweka masharti au kuzuia utaoaji mimba katika jimbo hilo.

    Swali la kura ya maoni katika Kansas limekuwa likisubiriwa tangu Mahakama ya juu zaidi ya Marekani ibatilishekensi ya Roe dhidi ya Wade, katika uamuzi wa mwaka 1973 ambapo uamuzi wa mahakama ulihalalisha kisheria utoaji mimba kote nchini Marekani.

    Inakadiriwa kuwa Wakazi wa jimbo la Kansas walipiga kura kwa zaidi ya 60% kuidhinisha haki ya jimbo ya kikatiba ya wanawake kupata huduma ya utoaji mimba.

    Ge

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Taylor Hirth akisherehekea na binti yake

    Wakati uamuzi wa kesi ya Roe dhidi ya Wade ulipobatilishwa, Rais Biden alisema haki za utoaji mimba litakuwa ni swala la wapiga kura. Kile kilichotokea katika Kansas kimebadili nadharia hiyo kuwa kweli.

    Donald Trump alishinda Kansas kwa pointi 15 miaka miwili tu iliyopita, lakini sasa imepiga kura kulinda upatikanaji wa huduma ya kutoa mimba katika kile kinachoonekana kama ushindi wa kihistoria.

    Unaweza pia kusoma:

    • 'Ni wasichana, sio kinamama': Nchi ambayo wasichana sita huavya mimba kila siku
    • Virusi vya corona: Wanawake ambao hawawezi kuavya mimba katika wakati wa amri ya kukaa nyumbani
    • Uavyaji mimba: Wachangisha fedha kupinga sheria ya Trump
  8. Uchaguzi Kenya 2022:Ruto abubujikwa na machozi kanisani;Wajackoya akana kumuidhinisha Odinga

    Maelezo ya video, Ruto anaonekana kujaribu kuzuia machozi wakati wa ibada

    Naibu Rais wa Kenya William Ruto Jumanne alijawa na hisia, huku akitoa machozi wakati wa ibada ya kanisa iliyofanyika katika makao yake rasmi huko Karen, Nairobi.

    Katika video hiyo inayonasa tukio hilo, Ruto anaonekana kujaribu kuzuia machozi wakati wa kikao cha ibada kilichoongozwa na Askofu Mark Kariuki kuombea uchaguzi wa amani huku Wakenya wakielekea kupiga kura wiki ijayo.

    Video hiyo ilizua hisia tofauti mtandaoni .

    Baada ya ibada ya kanisani Ruto alifanya mkutano wa kampeni katika Kaunti ya Nyeri ili kupigia debe azma yake ya urais .

    Hii si mara ya kwanza kwa Ruto kuonekana akitokwa na machozi hadharani. Mnamo mwaka wa 2013, Ruto aliangua kilio kanisani baada ya ushindi wake na rais Kenyatta

    ‘Sijamuidhinisha Raila’-Wajackoya

    th

    Chanzo cha picha, GEORGE WAJACKOYAH

    Kwingineko mgombeaji wa urais wa chama cha Roots George Wajackoya amekana madai kwamba amemuidhinisha mbombeaji wa muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga.

    Kupitia taarifa ,Wajackoya amedai kwamba video inayosambazwa mitandaoni ikimuinyesha akimuidhinisha Odinga imebadilishwa ili kuwapotosha wafuasi wake .

    Amesema bado yupo katika kinyang’anyiro cha kuchukua uongozi wa Kenya .

    TH

    Chanzo cha picha, ROOTS PARTY

  9. Uchaguzi Kenya 2022: Marekani yawatahadharisha raia wake dhidi ya kusafiri Kisumu kabla ya uchaguzi

    Chargé d’Affaires Eric Kneedler

    Chanzo cha picha, @Chargé d’Affaires Eric Kneedler

    Maelezo ya picha, Balozi wa Marekani nchini Kenya Eric Kneedler

    Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umetoa tahadhari kwa raia wake dhidi ya kusafiri kwenda katika mji wa magharibi mwa Kenya wa Kisumu, kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.

    Katika taarifa yake, ubalozi huo umesema “ umeweka masharti ya kusafiri” kwa wafanyakazi wake katika mji wa Kisumu “ongezeko la hatari'

    Mji wa Kisumu ni ngome ya Waziri Mkuu wa zamani na Mgombea wa Urais Raila Odinga .

    Taarifa ya Marekani inahusiana na maandamano na mikutano ya mara kwa mara inayofanyika kuelekea uchaguzi na ambayo inaweza kuendelea, ambayo wakati mwingine huzuia mikutano muhimu na kusababisha misongamano ya magari barabarani.

    “Maandamano wakati mwingine yanaweza kuwa ya ghasia, yanayohitaji polisi kuingilia kati. Harakati za Migomo na maandamano inayohusiana na hali za kiuchumi hutokea mara kwa mara.” Ilisema taarifa ya ubalozi.

    Hii inakuwa wakati serikali ikipeleka maafisa zaidi wa usalama katika eneo la Bonde la Ufa (Rift Valley) kutokana na hofu za usalama. Eneo hilo linachukuliwa kuwa ngome ya Bw Ruto

    Wanafunzi tisa wa chuo kikuu kutoka Uasin Gishu wanashikiliwa na polisi kwa madai ya kusambaza vijikaratasi vya chuki kupitia makundi yao ya WhatsApp.

    'Kisumu ni salama'

    Ga
    Maelezo ya picha, Gavana wa Kisumu Anyang Nyong'o (aliyeketi kushoto)

    Wakati huo huo Gavana wa Kisumu Anyang Nyong'o amesema kwamba Kisumu ina amani sana na kuongeza kuwa “anapuuza” tahadhari iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani.

    Taarifa zaidi kuhusu uchaguzi wa Kenya 2022:

    • Uchaguzi Kenya 2022:Nani yuko kwenye kinyang'anyiro cha kuiongoza Kenya ?
    • Uchaguzi Kenya 2022:Mfahamu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya
    • Uchaguzi Kenya 2022: Maafisa na taasisi zitakazohusika katika makabidhiano ya mamlaka
    Maelezo ya video, Gavana wa Kisumu Anyang Nyong'o asema Kisumu ina amani
  10. Vita vya Ukraine: Marekani yamuwekea vikwazo ‘mke wa siri' wa Putin

    GAVRIIL GRIGOROV/TASS

    Chanzo cha picha, GAVRIIL GRIGOROV/TASS

    Maelezo ya picha, Marekani haimuwekei vikwazo Kabaeva kwa kuhofia kwamba Putin ata "jibu kwa uchokozi," WSJ iliandika mwezi Aprili

    Wizara ya fedha ya Marekani imejumuisha Warusi 13 katika orodha ya watu waliowekewa vikwazo, akiwemo Alina Kabaeva, mcheza sarakasi wa zamani na ambaye sasa ni mkuu wa bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya vyombo vya habari ya Urusi , National Media Group, ambaye ana uhusiano na Vladimir Putin, na mabilionea sita, pamoja na vyombo vingine 30 vya kisheria.

    Hatua hii ya Marekani inakuja baada ya hatua kama hiyo kuchukuliwa na Uingereza pamoja na na Muungano wa Ulaya.

    Elena Kabayeva, anayejulikana kama "Mama taifa wa kisiri" nchini Urusi ameangaziwa tangu Urusi ilipovamia Ukraine.

    Hii ni kwa sababu Marekani iliwawekea vikwazo wandani wa karibu wa Rais Vladimir Putin, wakiwemo mabinti zake.

    REUTERS

    Chanzo cha picha, REUTERS

    Maelezo ya picha, Putin na Elena

    Elena Kabayeva ni nani?

    • Elena alishinda medali ya dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki ya Athens mwaka wa 2004. Alianza kufanya mazoezi akiwa na umri wa miaka 13 na kupata ushindi wake wa kwanza wa dunia mnamo 1998.
    • Tangu wakati huo ameshinda medali kadhaa zikiwemo za Mashindano ya Uropa ya 2001 na 2002. Pia alishinda Makombe kadhaa ya Dunia mnamo 2003.
    • Elena alijiunga na siasa za Urusi mwaka 2005, jina lake lilipohusishwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin.
    • Alichaguliwa kuingia katika Duma, bunge la Urusi. Mnamo 2014, alitunukiwa kuwa mmoja wa wanariadha kadhaa waliobeba mwenge wa Michezo ya Olimpiki ya Sochi.

    Unaweza pia kusoma:

    • Elena Kabayeva: Mfahamu mke wa siri wa Rais Vladimir Putin ni nani?
    • Elena Kabayeva: Mfahamu mke wa siri wa Rais Vladimir Putin ni nani?
  11. Uchaguzi Kenya 2022: Jamii ya Washona kupiga kura kwa mara ya kwanza Kenya

    Jamii ya Washona nchini Kenya watapiga kura kwa mara ya kwanza katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 9, 2022. Kundi la kwanza la jamii hii liliwasili Kenya kutoka Zimbabwe miaka sitini iliyopita na kukupewa uraia mwaka 2020. Oliver Mugererera Ndoro hakusita kuelezea BBC furaha yake.

    Maelezo ya video, Uchaguzi wa Kenya 2022: Washona kupiga kura kwa mara ya kwanza

    Video na Jeff Sauke

  12. Wanigeria sita wakamatwa juu ya wizi wa wavuti wa wapenzi wa jinsia moja

    Washukiwa wanasemakana kutumia wavuti wa kutafuta wenza wa jinsia moja kuwaibiawaathiriwa

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Washukiwa wanasemakana kutumia wavuti wa kutafuta wenza wa jinsia moja kuwaibiawaathiriwa

    Polisi nchini katika jimbo la kati mwa Nigeria la Nassarawa wamewakamata watu sita wanaowashuku kuendesha wavuti wa wizi wa kutafuta wapenzi kwa ajili ya wapenzi wa jinsia moja.

    Washukiwa hao wanasemekana kutumia wavuti huo kuwalaghai waathiriwa kabla ya kuwaibia.

    Kukamatwa kwa watu hao kulifuatia malalamiko ya muathiriwa ambaye alidai kuwa picha zake za utupu zilichukuliwa, kwa tisho la kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii iwapo asingewapatia pesa.

    Tukio hilo liliripotiwa katika eneo la Masaka, lililopo Karu, linalopakana na mji mkuu wa Nigeria Abuja.

    Msemaji wa polisi wa jimbo hilo Ramhan Nansel aliiambia BBC kwamba washukiwa - wanaume wanne na wanawake wawili – walidaiwa kutuma picha za watu wanaotafuta watu wanaoshiri mapenzi ya jinsia na kuwakaribisha wale wenye nia nao kwa kupanga tarehe ya kuwakutanishakupitia mchakato wa kumpata mpenzi unayemtaka.

    Hatimaye huwaibia waathiriwa au kuchukua mali zao kwa nguvu na kuwawekea vitisho ili kuwanyamazisha.

    Polisi walisema kwamba washukiwa watashitakiwa baada ya uchunguzi kukamilika.

    Nchini Nigeria mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja ni uhalifu, na wanaopatikana na hatia hiyo hukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 14 jela.

  13. Kupanda kwa bei ya mafuta Tanzania kwazua mijadala mitandaoni

    Mafuta

    Wananchi nchini Tanzania wameamka na bei mpya ya mafuta jumatano ikiwa imepanda kutoka bei ya awalibaada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) kutoe bei elekezi kwa mwezi Agosti.

    Kwa sasa bei ya rejareja kwa mafuta ya petroli katika jiji la Dar es Salaam itakuwa Shilingi 3,410 kwa lita kutoka shilingi 3,220 ya awali ikiwa ni ongezeko la kiasi cha shilingi 190.

    Kwa upande wa dizeli sasa yatauzwa kwa shilingi 3,322 kwa lita ambayo ni ongezeko la shilingi 179 ambapo mwezi uliopita bei elekezi ilikuwa ni shilingi 3,143

    Bei elekezi kwa mafuta ya taa ya sasa ni 3,765 kwa lita kutoka shilingi 3,442 ya awali.

    Kwa mujibu wa Mamalaka ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), bei hizo zimejumuisha ruzuku ya Sh100 bilioni iliyotolewa na Serikali.

    Ewura inabainisha kuwa bila ruzuku bei ya mafuta ingekuwa juu zaidi ambapo kwa lita ya petroli ngeuzwa 3,630 na dizeli ingekuwa shilingi 3,734 kwa Dar es Salaam.

    ‘Bei za mafuta katika soko la dunia zinaendelea kupanda na hivyo kusababisha bei ya mafuta katika soko la ndani pia kuongezeka. Ili kupunguza athari za ongezeko hilo kwa wenyeji, Serikali imetoa ruzuku ya TZS 100 bilioni kwa ajili ya mafuta ya Agosti 2022’, ilieleza taarifa waliyoitoa

    Kupanda huko kwa bei kumezua maoni mseto na mijadala katika mtandaoni:

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

    Ruka X ujumbe, 3
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 3

  14. Ayman al-Zawahiri: Marekani yaonya kuhusu uwezekano wa ulipizaji kisasi juu ya kifo cha kiongozi wa al-Qaeda

    Zawahiri has been al-Qaeda's most prominent spokesman and ideologue

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Zawahiri amekuwa msemaji maarufu maarufu zaidi wa fikra za al-Qaeda

    Marekani imewapa tahadhari raia wake dhidi ya uwezekano wa ghasia wanazoweza kuelekezewa katika nchi za kigeni kufuatia mauaji ya kiongozi wa Al-Qaeda Ayman al-Zawahiri.

    Kifo chake kinaweza kuwafanya wafuasi wa al-Qaeda au makundi mengine yenye uhusiano nalo kuyalenga maeneo ya Marekani na wafanyakazi wake, ilisema taarifa ya wizara ya mambo ya ndani.

    Zawahiri aliuawa katika shambulio la droni katika mji mkuu wa Afghanstan, Kabul Jumapili.

    Alikuwa amesaidia kupanga mashambulio ya 9/11/2001 nchini Marekani ambapo watu wapatao 3,000 walipoteza maisha.

    Ayman al-Zawahiri, aliyekuwa na umri wa miaka 71, daktari wa Misri alichukua uongozi wa al-Qaeda baada ya kifo cha Osama Bin Laden mwaka 2011.

    Mauaji yake yalithibitishwa Jumatatu na Rais wa Marekani Joe Biden, ambaye alisema kuwa Zawahiri alikuwa amepanga "msururu wa mauaji na ghasia" dhidi ya raia wa Marekani.

    Bw Biden alisema kuwa kifo cha Zawahiri kitawafariji waathiriwa wa mashambulio ya mwaka 2001, ambapo washambuliaji waligonga ndege za wasafiri katika majengo maarufu katika miji ya New York na Washington – yakiwemo majengo marefu ya ghorofa ya Manhattan.

    Bw Biden alisema kuwa Zawahiri pia alipanga mashambulio ya 1998 dhidi ya balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania, ambapo watu 223 waliuawa.

    Unaweza pia kusoma:

    • Ayman al-Zawahiri : Kiongozi wa Al Qaeda aliuawa vipi?
    • Ayman al-Zawahiri : Mshtuko Kabul baada ya Marekani kumuua kiongozi wa al-Qaeda
  15. Urusi yaishutumu Marekani kwa kuhusika moja kwa moja katika vita vya Ukraine

    TH

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Urusi imeishutumu Marekani kwa kuhusika moja kwa moja katika vita vya Ukraine kwa mara ya kwanza.

    Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Moscow alidai kuwa Marekani ilikuwa ikiidhinisha maeneo ya kulengwa na silaha za kivita za Himars zinazotumiwa na wanajeshi wa Kyiv.

    Luteni Jenerali Igor Konashenkov alisema simu za moja kwamoja kati ya maafisa wa Ukraine zilifichua uhusiano huo. BBC haikuweza kuthibitisha hili.

    Hapo awali Urusi iliishutumu Washington kwa kuchochea vita nchini Ukraine.

    Msemaji wa Pentagon alisema iliwapa Waukraine "taarifa za kina kwa wakati nyeti ili kuwasaidia kuelewa vitisho vinavyowakabili na kuilinda nchi yao dhidi ya uvamizi wa Urusi".

    Himars ni mfumo wa roketi nyingi ambao unaweza kurusha makombora ya yanayoongoza kwa usahihi katika shabaha hadi kilomita 70 (maili 45) mbali zaidi ya mizinga ambayo Ukraine ilikuwa nayo hapo awali.

    Pia wanaaminika kuwa sahihi zaidi kuliko Urusi.

    Bw Konashenkov alisema: "Ni utawala wa Biden ambao unawajibika moja kwa moja kwa mashambulizi yote ya roketi yaliyoidhinishwa na Kyiv kwenye maeneo ya makazi na miundombinu ya kiraia katika makazi ya Donbas na mikoa mingine ambayo ilisababisha vifo vingi vya raia."

    Mwezi Aprili, Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov alisema uamuzi wa Rais wa Marekani Joe Biden wa kuipatia Ukraine silaha zenye thamani ya mabilioni ya dola ulimaanisha "Nato, kimsingi, inahusika katika vita na Urusi kupitia wakala na inampa wakala huyo silaha".

    Wakati wote wa mzozo nchini Ukraine, Urusi imekuwa ikishutumiwa kwa uhalifu mwingi wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Wiki iliyopita, Ukraine iliishutumu Moscow kwa kulipua gereza la watu wanaotaka kujitenga lililofanyika Donetsk ili kuficha madai ya mateso.

    Unaweza pia kusoma

  16. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja hii leo Jumatano tarehe 3 Agosti 2022